Twende zetu wote na kura yangu ipo tayari kabatini inakusumbilia.
swissme
Ben....
wewe ni kijana makini.
elimu yako, mtazamo wako na nia yako inaelezwa na juhudi zako kujiendeleza wewe binafsi kwa ajili yako na taifa lako....
nilitaka kushangaa eti uingie ACT??? hapana ... ukiingia kwenye kinyanganyiro siku zote kuna kushinda au kutokutimia kwa kura.........kushindwa chaguzi zilizopita haina maana kuwa haupendwi.....na si kwamba huna mchango...au si kwamba system imekutema..... ni muda tu haujafika...
watu wengi wenye jitihada kama wewe wanahitajika....tunajua yuko selasini kule rombo...na kimbunga cha rombo kila mtu anakijua......hasa kwenye chaguzi za serekali za mitaa juzi.... na mwamko mkubwa wa kisiasa.....lakini HII HAINA MAANA USIINGIZE JINA....na hata akibakia kuwa yeye kwa kura za maoni..haina maana kuwa ndio mwisho wako kisiasa...
naamini kabisa chadema, ukawa na tanzania kwa ujumla bado inahitaji elimu yako na ujuzi wako....wewe sio kama wale AJIRA SIASA.......
hata kura zisipotosha sasa.....
kama ni pesa elimu yako itakupa pesa hadi uchanganyikiwe....wewe maliza shule halafu ingia front....
utagombaniwa tuuu....na kisha unawezza kukisaiidia chama na taifa kwa namna bora zaidi...
kuna umoja wa mataifa kuna international forums na platforms...na mashirika....
kila sehemu tunalaumiwa watanzania hatutafuti fursa.....
nashukuru nimekufahamu leo...
wewe sio kama wale wachumia tumbo....wewe ni mchumia kichwani.....
siasa kwako haiwezi kabisa kuwa ajira...
watanzania tunataka tutoke huko...siasa isiwe ajira....bali tu huduma ya uongozi kwa umma...
uchaguzi ukiisha wote tunarudi kwenye ajira zetu na profession yetu..
maana watanzania tumekalia siasa na siasa...
kwani siasa ina sehemu gani kwa GDP ya taifa??
waachie wachumia tumbo wahangaike....
wewe chapa raba......wewe ni mweledi..
hongera sana Sanane...Mungu mbariki Sanane, Mungu ibariki Tanzania