Swali langu kuu Ben, Mzee Serasini ni Senior ndani ya Jimbo lako...Je natumaini mtacompromise nae kwa faida ya wanarombo? Wazee wetu hawa wa enzi ya Mwalimu wakati mwingine uwa na misimamo fulani hivi rigid [Stubborn] na kusimamia wanavyoamini wao kwa namna ambayo walivyojengwa na mfumo wa kipindi chao....ni wakati huu sasa chama chenu makao makuu kuandaa nafasi za watu ambao ni SENIOR na Muhimu kwenye mambo ya Chama chenu kupata nafasi za kutumikia Chama chenu lakini wakiwa backbench.
Tunaitaji vijana wengi mjengoni, wenye mawazo mapya, mawazo mbadala, changamoto za usasa. Wakati mzee wa enzi zile Bungeni wanakimbia na hawapendi marumbano ya hoja, kijana wa sasa suluhu kwa stahiki ya pande mbili ikishindikana kwa njia ya kucompromise basi hata kwa marumbano ya hoja kisha wananchi wanaamua kupitia marumbano ya hoja zao.
Vijana wa zamani, wazee wa leo marumbano kwao ni uchuro, wehu, ni utovu wa nidhamu kubishana bungeni, wakati bunge la Uingereza ambako wao walikopi mfumo wa serikali na demokrasia wao leo hii wana boooooo...bungeni.Dunia imechange kumeingia siasa za ukinzania [Opposite] yani kwenda kwa hoja tofauti na hoja ya mwingine na hoja zikishindana ni hoja hipi bora zaidi ya nyingine.Sasa kama kizazi kile cha wazee wetu bado kiko kwenye ndio mzee, yes sir, wakimuona mzungu wanatetemeka, hawawezi kubishana na mzungu ikibidi kufoka kama kama kakosea ili kumuonyesha hisia za kimaumbile kuwa Umekasirika kwa tendo lake hilo lililopelekea wewe kufoka.
Wazee wetu umefika nyakati sasa wakae nyuma, wawe mafuta ya vilainishi pale vijana wanapoonekana kwenda kwa speed kubwa basi watoe ishara kuwa hapa mwendo ni 50/Per HR na Pale ni 80/Per HR.
Nasubilia kuona vijana wa CCM, wakianza kuwapumzisha wazee wao....ili safu ya vijana pande mbili UKAWA vs CCM wakabukue vifungu ili miswada na hoja makini ndio zipate kibali kwa faida ya umma wa Watanzania.TUMECHOKA NA WANAOSEMA NDIO WASEMA NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO WANAOSEMA SIO WASEME SIOO.
WANAOSEMA NDIOOOOOOOOO... WAMESHINDANA.......YANI KIPINDI HICHO UWA NASIKIA UCHUNGU MPAKA BASI.