Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Ben na hicho kigugumizi chako utachangia hoja gani bungeni? we endelea kutumwa tumwa chips mayai na Mbowe hapo Ufipa

Yamekuwa hayo tena nyumba ndogo yenu waliposema juzi Ben ana hamia kwenye nyumba ndogo yenu mulishangilia kwa nderemo na vifijo,mbona mmeanza kugeuka tena?.
 
Ndo maana watu wako tayari kufia CCM. kwa mawazo yako na utaifa ulionao ungesha pewa UKUU WA WILAYA kwani tunashuhudia zinahongwa tu. MAANA SHIDA YAKO WEWE NI HELA ZA FASTA FASTA TU. HUKU CDM UBUNGE MNAENDA PIGANA JUJU TU.

BTW HILO JIMBO UNALOENDA ,,WAMEKWAMBIA WENYE NALO WAMELICHOKA.

DAHHH. KILA LAKHERI BANA BILA SHAKA UKOO WAKO UMEIAFIKI HATARI HII KUBWAA MBELE YAKO.
 
Gooo go Ben kama itakuwa jimboni kwangu nitakupa kura hata kama ni jimbo jingine nakuunga mkono. Ungenisikitisha sana kama ungehamia huko wapi sijui.
 
apo mmoja lazima aingie ACT its the matter of tym; anatangazia jimbo la mtu wa CDM kwanza uyu jamaa msaliti ha ha haaa
 
"Naelekea Bungeni"
Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni. Naam, naelekea bungeni.
Mkuu Ben Saanane, kwanza naunga mkono hoja, pili nakukubali kwa ujasiri sio tuu wa kutangaza nia bali pia kutangaza vita na aliyepo!. Nakupongeza kwa dhati kwa vile hakuna jimbo ambalo ni mali ya mtu, wala hakuna mbunge yoyote aliyepo mwenye hati miliki ya jimbo lolote hivyo ni haki yako kutangaza nia na kugombea jimbo lolote!.

Pili nimefurahishwa sana na uamuzi wako wa kutangaza nia baada ya kufanya utafiti!. Nilipokutana na Dr. Slaa mahali ile 2012, nilimweleza kuwa kuna maeneo CCM imechokwa mpaka basi kiasi kwanza kama Chadema ingesimamisha hata jiwe, jiwe lingechaguliwa!, hivyo nikatoa wito kwake kuhakikisha 2015, Chadema inasimamisha wagombea kila jimbo!.

Jaombo la pili nilimsisitizia, Chadema isisubiri hadi wagombea ndio wajitokeze, bali ifanye utafiti kila jimbo iweke competent man na hata ikitokea jimbo fulani wakajikuta hawana kabisa competent men wa kuwasimamisha, then wafanye head hunting ya grooming watu ili wasikose mtu wa kumsimamisha, hivyo nyinyi ambao ni competent mnavyojitokeza mapema mnakirahisishia chama kazi ya kutafuta watu!. Nlishauri watu wawe encoraged kutangaza nia mapema ili mpate muda wa kuwachambua, kuwapima na kuwashindanisha kile aliye bora zaidi na mwenye chance ya kuleta ushindi ndie apitishwe!.

Na tatu nilimshauri, kuwa miongoni mwa wabunge wa Chadema waliomo bungeni, kuna wabunge wazuri bungeni lakini ni hopeless kwenye majimbo yao, hivyo Chadema ifanye utafiti kwa wabunge wake wote waliomo bungeni, chances zao za kuchagulika majimboni mwao zikoje, ili kuzui kupoteza baadhi ya majimbo na kutolea mfano jimbo langu mimi nililopo jimbo la KAWE, ambalo mbunge wangu ni Mhe. Halima Mdee. 2015 CCM inamsimamisha mtu very competent kupambana na Mdee, hivyo nikashauri Chadema don't just sit and watch jimbo la KAWE likirudishwa CCM, bali lifanya utafiti wa chances za Mdee kuchaguliwa tena na kikiona risk, then Chadema ndio kimreplace Mdee na kuleta mtu more competant atakayelitetea hili jimbo, vinginevyo kama Chadema itabweteke na kutosimamisha watu competent kwenye majimbo kinayoyasikilia kwa hoja ya kutowaingilia wabunge waliopo, kitayarudisha baadhi ya majimbo!. Hivyo naamini kwenye jimbo lako, umeishafanya utafiti wa electability ya incumbent na ukajiridhisha kusipofanyika mabadiliko ya mgombea wa Chadema, jimbo linarudi CCM!, na ndio maana umeamua kujitosa!. Lakini kama mbunge aliyepo amefanya makubwa, na bado anakubalika, kitendo cha wewe kutangaza kuliwania huo sio tuu ni uchokozi bali ni kutaka kuletea fujo kwa mgombea na kuletea fujo kwa chama. Fujo za aina hii ni ZZK Style watch out usijekuitwa msaliti!.

Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang'anyiro
cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kwanza, nimesukumwa na maono, uwezo na umahiri wa kiuongozi, pamoja na dhamira ya dhati ya kuwa kiongozi wa watu, niliye tayari kutumia kila fursa, mikakati na mbinu zote za kiuongozi kuboresha maendeleo ya wananchi. Nawiwa kuwa mwakilishi tofauti wa wananchi, nitakaye tengeneza tofauti yenye tija kwenye maisha yao, nikitumia weledi na karama zangu za kiuongozi
Hapa Mkuu Ben Saanane haya ni majisifu ya egotistically driven by egotistic desires from egotisim!. Hapa huna tofauti na ZZK!, kutanguliza umimi!. Unaonekana wewe tayari umeisha determine lazime uwe, sasa ikitokea ukakatwa, unaweza kabisa kuamua kuwa kwa vile umeisha determine, ikishindikana kugombea kupiti Chadema, then utagombea kupitia njia nyingine yoyote!. Hii ni hatari!. Nilishauri ili mtu uwe kiongozi bora sio wewe kujiona una sifa, una uwezo na unaweza, bali tekeleza tuu majukumu yako kama kiongozi kwa kuonyesha uwezo, kisha watu waliokuzunguka, wauone huo uwezo wako, wao ndio waje kukushauri kuwa kija unaweza!, njoo huku utusaidie kwenye nafasi hii ya uongozi!. Hii haina maana ukijiona unaweza usijitokeze bali usijisifu kuhusu uwezo, onyesha huo uwezo usifiwe, ushauriwe gombea, ndipo utangaze nia!.
tangazo langu hili la "Naelekea Bungeni" linazingatia ukweli kuwa mpaka sasa nimeshafanya kazi kubwa iliyozaa matunda ya kuimarika kwa mtandao wa chama changu katika jimbo ninalokusudia kugombea na kuchangia kwa kiasi kikubwa chama changu kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kama kilivyofanya vizuri pia maeneo mengi nchini. Naomba tuendelee kuidumisha nguvu hii kubwa ya uungwaji mkono kuelekea kura za maoni na hatimaye nitaunda timu ya kampeni kabambe kuelekea Bungeni Oktoba 2015.

Najua bado sijatii kiu yenu maana sijaweka wazi jimbo ninalokusudia kugombea!. Naomba tuvute subira katika hilo. Nimeshaamua kwa uhakika, ni jimbo gani nagombea! Baada ya kutimiza masharti yote yaliyobaki ya kikanuni,kiitifaki na kikatiba, ndani ya kipindi kisicho kirefu nitawatangazia wananchi wa jimbo husika na mikakati yangu katika nyanja zote muhimu nanyi mtasikia, na hatimaye kuomba ridhaa ya chama changu kuipeperusha bendera ya chama kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2015.Kwa sasa, itoshe kwenu ninyi kujua ya kuwa Naelekea Bungeni.

Natambua safari hii sio nyepesi,ni safari yenye miiba na mabonde, lakini naweza kusema jambo moja tu, kwamba safari hii ni ya uhakika na nimejipanga sawasawa. Na ninaaamini kupitia ninyi marafiki zangu safari hii itakua nyepesi nay a uhakika zaidi.

Nawaomba kwa moyo mkunjufu na kwa unyenyekevu mkubwa Mnisindikize Bungeni;Mwenyezi Mungu atangulie mbele ya safari yetu .

Twende Bungeni na Ben Saanane!
Hii pia ni muendelezo wa ile ile strong determination yako kwenda bungeni, ningeomba pia utupe na options zako iwapo Chadema haitakupitisha kugombea jimbo hilo ambalo tayari ni ngome ya Chadema, jee uko tayari kugombea jimbo jingine lolote ambalo sio ngome mathalan ka Kinondoni?!, au umepania lazima ugombee hapo hapo ulipoamua, na kama Chadema haitakupitisha unaweza ku jump ship na kulitwaa jimbo hilo?!.

Pamoja sana!.

Pasco
 
Kk ben,kwanza ongera kwa uamuzi wako mzr,pili ongera kwa kukaa kimya kuto jibu ile thread ya kipuuzi,binafsi sina chama ila nakukubali sana,na pia kwa moyo wote umepongezwa na kk ritz pia kwa moyo wake wote bila kujali tofauti zenu za kichama,hii inaonesha ni jinsi gani unathaminiwa kwa michango yko na mategemeo mengi toka kwako,lkn pia nikwambia kitu ndani ya chama chochote lazima kuwe na makundi hasimu,laxima uwe na marafiki na maadui pia coz hata mungu anao maadui sembuse binadamu sisi?.Hayo makundi yasikurudishe nyuma,lkn pia ndani ya ma pro cdm,nadhani umewaona wanafiki zako kupitia ile thread ya kipuuzi,watu kama akina shardcole ni watu mhm sana kwako,hawakuvunjika moyo,lkn pia wale wengne ma pro cdm wenzako waliokuponda,usiwahukumu wote kwa mabaya wanakupenda,wanajua umhm wako na walikuwa wanaumizwa na kuhama kwako so wakakosa uvumilive kama shardcole hawakuwa na njia nyingne zaidi ya kukulalua ili kukilinda chama chao,ni ndg zako hao. Lkn pia nakuhakikishia ukijitambua na kuwa na hoja presentation siyo kz ni uzoefu tu na baadaye utakuwa vzr so usiogope wanaosema ben wa jf hawezi jukwaani,mda ukifika ntakupa support yang ya mali,binafsi wewe na pasco humu jf nawakubali sana.

ntamwangah,

Asante sana sana.Ninaelewa sana.Nilisoma comments zote.Siasa inahitaji ngozi ngumu.Maudhui ya Ushauri wako nimeyazingatia sana sana hadi sasa
 
Last edited by a moderator:
Karibu jimboni kwetu na tunakutakia kila kheri bro. You have my vote as well as your presidential candidate!
 
Ben ni mtu anayeitajika sana bungeni kwa kijana anayependa hamsha hamsha. Kama nilivyosema jana chadema iangalie namna ya kumpa nafasi huyu mchizi
 
Swali langu kuu Ben, Mzee Serasini ni Senior ndani ya Jimbo lako...Je natumaini mtacompromise nae kwa faida ya wanarombo? Wazee wetu hawa wa enzi ya Mwalimu wakati mwingine uwa na misimamo fulani hivi rigid [Stubborn] na kusimamia wanavyoamini wao kwa namna ambayo walivyojengwa na mfumo wa kipindi chao....ni wakati huu sasa chama chenu makao makuu kuandaa nafasi za watu ambao ni SENIOR na Muhimu kwenye mambo ya Chama chenu kupata nafasi za kutumikia Chama chenu lakini wakiwa backbench.

Tunaitaji vijana wengi mjengoni, wenye mawazo mapya, mawazo mbadala, changamoto za usasa. Wakati mzee wa enzi zile Bungeni wanakimbia na hawapendi marumbano ya hoja, kijana wa sasa suluhu kwa stahiki ya pande mbili ikishindikana kwa njia ya kucompromise basi hata kwa marumbano ya hoja kisha wananchi wanaamua kupitia marumbano ya hoja zao.

Vijana wa zamani, wazee wa leo marumbano kwao ni uchuro, wehu, ni utovu wa nidhamu kubishana bungeni, wakati bunge la Uingereza ambako wao walikopi mfumo wa serikali na demokrasia wao leo hii wana boooooo...bungeni.Dunia imechange kumeingia siasa za ukinzania [Opposite] yani kwenda kwa hoja tofauti na hoja ya mwingine na hoja zikishindana ni hoja hipi bora zaidi ya nyingine.Sasa kama kizazi kile cha wazee wetu bado kiko kwenye ndio mzee, yes sir, wakimuona mzungu wanatetemeka, hawawezi kubishana na mzungu ikibidi kufoka kama kama kakosea ili kumuonyesha hisia za kimaumbile kuwa Umekasirika kwa tendo lake hilo lililopelekea wewe kufoka.

Wazee wetu umefika nyakati sasa wakae nyuma, wawe mafuta ya vilainishi pale vijana wanapoonekana kwenda kwa speed kubwa basi watoe ishara kuwa hapa mwendo ni 50/Per HR na Pale ni 80/Per HR.

Nasubilia kuona vijana wa CCM, wakianza kuwapumzisha wazee wao....ili safu ya vijana pande mbili UKAWA vs CCM wakabukue vifungu ili miswada na hoja makini ndio zipate kibali kwa faida ya umma wa Watanzania.TUMECHOKA NA WANAOSEMA NDIO WASEMA NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO WANAOSEMA SIO WASEME SIOO.

WANAOSEMA NDIOOOOOOOOO... WAMESHINDANA.......YANI KIPINDI HICHO UWA NASIKIA UCHUNGU MPAKA BASI.
 
Waisrael walipokuwa wakitoka Misri kuelekea Kanani,walitanguliwa na nguzo ya moto usiku na wingu mchana.Na iwe hivyo kwako Ben katika safari yetu kuelekea Bungeni.Amen!
 
hii singo haiuzi . iliyouza ni ile ya kuhama. bora ungehama tu. every one predicted this. so it is not news at all. and on top.of that. hivi ni lazima kila mtu anayetaka kuonesha mchango wake kwa taifa awe mbunge?? we all know it ia not about that. its about. money . power and fame. unaweza jenga nchi hata ukiwa nje ya bunge.



Nafikiri watu wenye Calibra ya Ben wa Saanane wanahitajika Bungeni; sio mafala kama livingstone Lusinde au Hawa Ghasia...Ben Bunge la Tanzania linakuhitaji na sio wewe kulihitaji Bunge...!! Tuko pamoja
 
Wewe utaendelea kuwa Mbunge wa jamiiforum. Mitandao mingine huwezi kutoa hoja zaidi ya mtandao wenu wa JF kwa wananchi ndiyo utaweza kweli?

Acha wivu wa kike,ninyi ndiyo mlioeneza kwenye JF kwamba anahamia ACT,sasa aibu imekushika unatoa povu mdomoni.
 
Nenda mwanangu ukawachakaze hao magamba.
Nakutaa kila la kheri safari yako hiyo.
 
Amakweli Bavicha hamna akili kabisa,mlimtukana matusi nakumkejeli baada yakusikia anahamia Act,sasa mnamuona wa maana.
Leo nimefurahi sana yaani natamani ungekuwa karibu yangu
_Eti ben aende chama la wasaliti kwa kweli ningeshangaa sana Ben Mungu muweza utashinda baba mimi zangu sala tu!!!
 
Last edited by a moderator:
Tsafurd ,

Ni kweli CAG hukagua.



Kuna malalamiko juu ya baadhi ya wabunge ku-collude na DED na kuelekeza matumizi ya fedha kwa mrengo wa upendeleo

Mswada wa sheria hii mwaka 2009 ulipingwa na wanaharakati na mabalozi.Tuangalie namna ya kufanya marekebisho.Kuna mfumo mzuri kwa baadhi ya nchi kama Mauritius
Inawezekana wakati mwingine kuwa na mgongano kati ya Mbunge na wataalam hasa DED kuhusu namna ya matumizi ya fedha za CDCF hasa pale wanapokuwa na mitizamo tofauti lakini msingi wake unabaki pale pale kuwa ni fedha zaserikali na matumizi yake (yaani vipaumbele vya matumizi ya fedha za CDCF) hupangwa/huletwa na Kamati ya Mfuko wa Jimbo Wilayani ambapo Mbunge ni mjumbe wa kamati hiyo. Mwenyekiti wake ni Diwani mmojawapo kati ya madiwani ambao ni wajumbe wa Mfuko. Kamati ile inaundwa na Madiwani 2, DED, Afisa Miapngo (ambaye ndiye katibu wa kamati), watendaji kata 2 na wawakilishi 2 wa asasi za kiraia.
Hata hivyo fedha za Mfuko wa Jimbo ni fedha kidogo sana ukilinganisha na fedha zinazopelekwa katika Halmsahuri zetu kwa ajili ya maendeleo na kazi kubwa ya Mbunge ni kusaidiana na Madiwani na wataalam katika kibua miradi na kusimamia matumizi ya fedha za umma. Mbunge ana kazi ya ziada ya kufanya lobbying and advocacy serikali na kwa wafadhili ili kupata miradhi ya kuwaletea maendeleo wananchi. Mbunge hatakiwi kutofautina na wataalam. Akitofautiana tu na Wataalam hamna kitakachofanyika maana wataalam ndo watekelezaji wakuu wa shughuli za kila siku za serikali.
 
Back
Top Bottom