Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

sawa Ben ila kumbuka kuna michujo wa ndani ya vyama dhidi ya watia nia ndani ya chama pindi ukiachwa usikate tamaaa bali mbinu na uwezo wako ujumuike na mgombea kwenye kampeni ilimpate ushindi.naushindi huo utakua ni furaha kwako...
 
Ruttashobolwa

Jiongoze kaka uzi umefika page ya sita mkuu wewe umebaki na hoja moja tu "Kwahiyo Ben saanane siyo msaliti tena"..!! Huna hoja nyingine zaidi ya hiyo? Mbona wewe ni mtu mzima mwenye akili timamu, nini tatizo lililopo kwenye uelewa wako? Eti unachochea kuni..!! Ili ikusaidie nini ndugu yangu? Hivi utakula hizo kuni unazochochea hapa..?

Angalau Ritz mwenzio kamtakia heri Kamanda na kijana mwenzake kwenye malengo yake,wewe hata kufungua mdomo kukubali tu kile kilichocndikwa na Ben hapa umeshindwa..!! Umebaki kushabikia vitu visivyo na Msingi Vitakusaidia nini KJ...!!??

Anyway ngoja tumsubiri Ritz hapa amesema anaanza kushisha.matusi yaliyotukanwa na Bavicha kwa Ben Saanane, Ila mimi namuomba aonyeshe pia Namna Vijana wa Ccm,Act na wengineo wasikubaliana na Chadema jinsi walivyokhwa wakimsifu Ben kwamba ni kijana makini amabaye hajawahi kutokea Tanzania na Chadema yote..!! Hapa aanze na post zako zote ulizotoa kumuhusu Ben..

Alitukanwa Yesu alipokuwa ktk harakati za kuwaletea ukombozi itakuwa Ben ndani ya Cdm? Mume na Mke hugombana na kufukuzana itakuwa Ben na Makamanda wenzake tena wasiofahamiana kabisa? Lakini kubwa kuliko yote Wewe inakuwashia nini kwa kutukanwa kwa Ben? Unapungukiwa na nini hasa?

Watu wengine bwana..!!!

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
kamanda mabere malando alisema, mshauri mkuu wa zzk ni huyu mmiliki wa jf so, huenda kunaukweli hapo, nyuzi za uongo wanazoleta ccm=act, hata kama ni za kuchafua mtu, hakuna ushahidi zitaachwa hata siku nzima, sasa leta maada yenye ushahidi inayohusu ccm=act, au zzk, ndani ya sekunde 5 imenyofolewa na ukicheza una kula ban, kwa kweli jf inaelekea kuwa kama mitandao minginze ya hovyo kabisa;
sasa act wanatoa wapi ujinga wanao andika. Mods mko wapi au tuamini mnaibeba act?? Taarifa nyingi zinazoletwa na hawa mamluki ni za uongo. Tumeona hata zitto akitoa taarifa za uongo na mnazipokea. Hata pale walengwa wanapokanusha mods mnakaa kimya
 
Yericko Nyerere, Asante sana komredi wangu

Ha ha ha ha umewaacha ACT wavizia mizoga midomo wazi,maana yake wamegeuka mafisi wavizia mizoga inayotupwa na wenzao.

Wakisikia mwanachama yeyote wa CHADEMA anataka kuchukua maamzi magumu,maamzi magumu wanaoyajua wao ni kwenda ACT,mwisho watameza na visivyo mezaka.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwahiyo ile sumu sasa ni direct kwa spika siyo zitto tena lakini mlangoni pale bungeni kunamashine sijui kama utaingia nayo ndani.

Bora wewe umejitambua na kuunga mkono nakwenda Bungeni Ben sanane! Hayo ya sumu ni uzushi tu.
 
Ben akigombea namfuata katika jimbo hilo nami nikagombee, najua madhaifu yake huyu mkaanga Sumu.

Jimboni wagombea wanaenda kujinadi namna watakavyoshirikiana na wananchi wa jimbo husika katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi wewe unaenda kunadi madhaifu ya watu?

BTW mbona umekomaa mno kutoa comments nyingi katika uzi huu, ni mahaba binafsi kwa huyu mtoa nia au wivu? Hueleweki kabisa!
 
Ha ha ha ha umewaacha ACT wavizia mizoga midomo wazi,maana yake wamegeuka mafisi wavizia mizoga inayotupwa na wenzao.

Wakisikia mwanachama yeyote wa CHADEMA anataka kuchukua maamzi magumu,maamzi magumu wanaoyajua wao ni kwenda ACT,mwisho watameza na visivyo mezaka.

Hahahaha ACT harakat zao kama za futuhi
 
MODS WANAENDEKEZA SANA UPUUZI WA HAWA CCM=ACT KWA KWELI, SIJUI WANAPEWA MLUNGULA AU VIPI?? SHUTUMA ZA UONGO KABISA ZINAACHWA HAPA, LAKINI JANA NIMEMSHAURI MAKENE AJITAHIDI KUWA SHARP, WATU WA CHAMA WANAPOKUWA ATTACKED BILA USHAHIDI AJE MARAMOJA KUTOLEA MAELEZO, OTHERWISE, HILI SUALA LA BEN NA LA SILINDE NA WENJE, NA DADA ROSE LIMESHANGAZA SANA WATU, NA KUNA WATU WAMEVUNJIKA SANA MIOYO, COZ YA KUTOPATA UKWELI WA TAARIFA; MODS HAWAKO FAIR AT ALL.....[QUOTE=Mzito Kabwela;12419399]Mkuu, nafurahishwa na viongozi wa Chadema kuendelea kunyamaza kimya.. kurugenzi ya habari, Mohamedi Mtoi na wadau muhimu wamenyamaza. Kurugenzi ya Usalama ya Chama itakuwa iko busy kuinvestigate huu mchezo wa kuigiza ulioanzishwa na ACT kwa kushirikiana na CCM. Huenda watu wetu wanashiriki...[/QUOTE]
 
"Naelekea Bungeni"

Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo;

Kwanza, nimesukumwa na maono, uwezo na umahiri wa kiuongozi, pamoja na dhamira ya dhati ya kuwa kiongozi wa watu, niliye tayari kutumia kila fursa, mikakati na mbinu zote za kiuongozi kuboresha maendeleo ya wananchi. Nawiwa kuwa mwakilishi tofauti wa wananchi, nitakaye tengeneza tofauti yenye tija kwenye maisha yao, nikitumia weledi na karama zangu za kiuongozi kama ifuatavyo;

Malezi yangu kisiasa ndani ya CHADEMA ndiyo yaliyochochea kiu na dhamira yangu ya muda mrefu katika kuwatumikia wananchi wenzangu bila kutetereka, nikiakisi misingi ya kifalsafa,kiitikadi na kisera ya chama chetu. Ni katika malezi hayo hadi sasa chama chama chetu kimeniamini kuwa ninatosha na kunikabidhi majukumu mbalimbali likiwemo jukumu jipya la kuongoza Idara ya Sera na Utafiti chini ya Kurugenzi husika katikaMakao Makuu ya Chama.Nimeutumikia wadhifa huu na ninaendelea kuutumikia kwa uaminifu mkubwa na kwa dhamira na moyo wa kizalendo kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo.

Naamini, ninao uzoefu wa kutosha kitaaluma na kiutendaji pamoja na ukomavu unaostahili kisiasa katika kubeba wajibu huu wa kuwatumikia wananchi jimboni na pia kubeba ajenda za kitaifa na kutekeleza wajibu wa ziada mbali na wajibu wa mbunge kama ilivyo kikatiba.

Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics).

Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi.

Ninaelewa adha wanayopata watoto kutoka familia za masikini,kwa kuwa nimesoma na kukulia katika mazingira hayo. Na nina uhakika kuwa adha na dhiki zote zinazowasibu Watanzania wenzangu hazitokani na mapenzi ya Mungu, nuksi wala kurogana, bali zinatokana na udhaifu wa kisera na kiuwajibikaji katika mfumo wa utawala wa nchi yetu; mfumo uliolea mataifa mawili ndani ya nchi moja katika sekta ya Elimu,Afya,Ajira na nyinginezo – taifa la mafukara na taifa lenye nacho; taifa la wale wanaoweza kusomesha watoto wao kwenye shule bora hasa English Mediums na kutibiwa kwenye hospitali za ughaibuni, na taifa la akina siye tunaosomesha kwenye shule za kata na kutibiwa kwenye zahanati chache zilizo mbali na zisizo na dawa.

Nitaongeza idadi ya wabunge makini bungeni katika kuvunja matabaka haya mawilina kubakisha taifa moja lenye kusimamia fursa na mgawanyo wa rasilimali kwa usawa katika kuwawezesha wananchi kujiendeleza!
Katika kupanga na kutekeleza Mikakati na vipaumbele vyangu kwa jimbo nitazingatia zaidi maoni na matakwa ya wananchi na ushauri wa kitaalamu.

Ninaamini ninao uwezo wa kubuni,kupanga,kuchanganua,kusimamia na kuandika Ripoti za Miradi ya Maendeleo kutokana na uzoefu wangu wa kiutendaji katika taasisi za Fedha, Asasi za Kiraia na Sekta binafsi. Mathalan, hadi sasa nimeshavuka hatua ya awali ya kushirikiana na taasisi ya ''Yunus Social Business-Global Initiatives(YSB)'' yenye makao yake nchini Frankfurt,Ujerumani iliyoanzishwa na Profesa Muhammad Yunus na kubadili hali ya uchumi na maisha ya mamilioni ya watu nchini Bangladesh kwa kutoa mikopo ya ujasirimali kwa wanawake na vijana katika sekta mbalimbali.

Nitashirikiana na asasi kama hizi za ndani na nje ya nchi yetu katika kuhakikisha mikakati nitakayoipanga kwa ajili ya wananchi inatekelezeka huku tukiendelea kuibana Halmashauri katika matumizisahihi ya fedha za umma.

Nitajenga hoja na kuaibnisha mikakati kukishawishi chama changu kwanini tunaweza kufanya vizuri zaidi.Tutawashawishi wananchi kwanini tunaweza kufanya vyema zaidi kuliko miaka mingine yote iliyopita katika uwakilishi wa nafasi ya ubunge

Nikipewa ridhaa na chama changu,sitapeleka bungeni ajenda ya kuongezewa posho kwa kisingizio chochote kile, bali nitaainisha vipaumbele, nitashauri na hata kuishinikiza serikali kwa hatua za kibunge na kiharakati nje ya bunge kuhakikisha wananchi nitakaowawakilisha wanapata haki wanayostahili.

Sitajisikia fahari kuhudhuria misiba mingi ya wananchi,bali nitajivunia rekodi ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana na kuokoa vifo visivyo vya lazima.Hiki ndicho nitakachojivunia baada ya miaka mitano

Ninasikitika sana kuona kwamba nchi maskini kama Tanzania inachezea fedha za umma kwa kutoa Fedha majimboni bila utaratibu wa ukaguzi na udhibiti wa fedha hizo, zinazotolewa kwa jina zuri la Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo(CDF) ambao unakua chini ya Mbunge.

Je,Wabunge watakapotumia fedha hizo kwa manufaa yao na hasa kipindi hiki cha uchaguzi ambacho wabunge wengi wanazitumia fedha za umma majimboni kuwaghilibu wananchi kwa misaada ya mifuko ya bati na Saruji na kuwahadaa kuwa zimetoka mifukoni mwao sio ufisadi? Ni lazima tupiganie misingi ya uwajibikaji kuanzia ngazi za chini ili pia tuweze kujenga hoja za kuiwajibisha serikali katika masuala ya maadili hasa dhidi ya tatizo sugu la ufisadi, uzembe na kuacha tabia ya kulindana.

Sheria kandamizi zisizokua za haki na zilizopitwa na wakati zitakua adui yangu mkubwa ndani ya chombo hicho kutunga sheria nchini.Ni lazima nihakikishe kwa nafasi yangu Bunge letu linasimama na kutetea haki ya watanzania na kurejesha heshima ya kibunge na kitaifa miongoni mwa mabunge mengine duniani.Sitatetea sheria hata kama ina maslahi binafsi kwangu.

Kwa mfano sheria na kanuni zinazoruhusu wabunge kulipwa mafao yao baada tu ya kumaliza muda wao wa kibunge ni sheria chochezi kiatika ufisadi na rushwa kwenye uchaguzi.Ni kwanini wabunge wasilipwe baada ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa hakuna mianya ya rushwa katika chaguzi zetu?Watumishi wa umma hasa walimu na madaktari wanalipwa mafao yao miezi sita baada ya kustaafu na wanavumilia,je kwanini wabunge wasivumilie?

Katika bunge linalomaliza muda wake,miongoni mwa wabunge waliotekeleza kwa weledi wajibu wao wa kibunge ni wabunge vijana. Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.

Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata ridhaa ya wananchi katika safari hii mpya tunayoianza,safari ya utumishi wa kweli kwa wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla.

Pili, ninazo sifa za jumla na vigezo vyote vilivyotajwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 67(1).

Tatu, tangazo langu hili la "Naelekea Bungeni" linazingatia ukweli kuwa mpaka sasa nimeshafanya kazi kubwa iliyozaa matunda ya kuimarika kwa mtandao wa chama changu katika jimbo ninalokusudia kugombea na kuchangia kwa kiasi kikubwa chama changu kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kama kilivyofanya vizuri pia maeneo mengi nchini. Naomba tuendelee kuidumisha nguvu hii kubwa ya uungwaji mkono kuelekea kura za maoni na hatimaye nitaunda timu ya kampeni kabambe kuelekea Bungeni Oktoba 2015.

Ninapotangaza uamuzi wangu huu,ninasimama juu ya mabega ya baadhi ya kaka na dada zangu waliotuwakilisha vyema ndani ya bunge la 10 linaloelekea ukingoni.Wengi wao nimefanya nao kazi kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kibunge kulingana na nafasi yangu.Ni muda wangu sasa kuomba ridhaa ya chama changu ili niweze kupata ridhaa ya wananchi katika safari hii mpya tunayoianza,safari ya utumishi wa kweli kwa wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla.

Mwaka 2010 tulikua na wagombea vijana,wengine wakiwa fresh kutoka vyuoni.Nilishiriki katika kampeni zile na pia katika kukusanya raslimali kwa ajili ya kampeni za ubunge hasa jimbo la ubungo.Uzoefu ule ule na wa ziada ndio huo huo tutakaoutumia.Tutapokea michango isiyokuwa na masharti ya kifisadi kutoka kwa marafiki wa ndani na nje ya kwa kuzingatia pia sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010. Sitatoa Rushwa.

Najua bado sijatii kiu yenu maana sijaweka wazi jimbo ninalokusudia kugombea!. Naomba tuvute subira katika hilo. Nimeshaamua kwa uhakika, ni jimbo gani nagombea! Baada ya kutimiza masharti yote yaliyobaki ya kikanuni,kiitifaki na kikatiba, ndani ya kipindi kisicho kirefu nitawatangazia wananchi wa jimbo husika na mikakati yangu katika nyanja zote muhimu nanyi mtasikia, na hatimaye kuomba ridhaa ya chama changu kuipeperusha bendera ya chama kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2015.Kwa sasa, itoshe kwenu ninyi kujua ya kuwa Naelekea Bungeni.

Natambua safari hii sio nyepesi,ni safari yenye miiba na mabonde, lakini naweza kusema jambo moja tu, kwamba safari hii ni ya uhakika na nimejipanga sawasawa. Na ninaaamini kupitia ninyi marafiki zangu safari hii itakua nyepesi nay a uhakika zaidi.

Nawaomba kwa moyo mkunjufu na kwa unyenyekevu mkubwa Mnisindikize Bungeni;Mwenyezi Mungu atangulie mbele ya safari yetu .

Twende Bungeni na Ben Saanane!
Ben, Kwanza nikupe hongera kwa maamuzi yako, lakini ukweli tuuzungumze hapa mapema. hakuna mgombea uchaguzi atakayekuwa akiwakilisha Chadema isipokuwa UKAWA na lazima ukubalike na mfumo watakao uweka. Aidha mfumo huo tayari bado haujatangazwa ama bado UKAWA hawajafikia maridhiano juu ya Uwakilishi. Mkigawana Majimbo lazima uwe umepewa jimbo tayari kama mgombea na kupitishwa maana yaonyesha kuna kugawana hakuna uchaguzi mdogo halali muda huo uko wapi?

Kwa nini sisi wengine tunakuwa na hasira na Chadema? ni kwa sababu hizi, sababu ambazo chama kimevutwa ktk ushirika ambao chama kimeshindwa kutangaza sera zake, maono yake juu ya mabadiliko wanayokusudia kuwapelekea wananchi isipokuwa lengo limebadilika kuwa ubishani bungeni. Wewe hapa umeeleza vizuri sana nia yako ya kugombea Ubunge lakini haya ni maono yako leo yapo JF lakini wananchi vijijini hawafahamu hilo wamepumbazwa na katiba Mpya. Na ni maono yako sio sera za UKAWA hivyo mbunge hawezi badilisha maisha ya wananchi ikiwa sio lengo la UKAWA. Na unapogombea kujaza Bunge huwezi waahidi wananchi mabadiliko maana hutaongoza nchi ila mnaahdi kubishana juu ya maamuzi ya CCM.

Tumezisikia hadithi hizi miaka mingi toka wabunge wa CCM wakiahidi wananchi kwa uchungu kabisa wakielewa nini matatizo ama mahitaji yao lakini hakuna lilofanyika. Ahadi za Wabunge na mipango ya chama hutofautiana kwa mbali kabisa, hivyo maadam UKAWA hawana sera ya pamoja isipokuwa ahadi za Katiba ya Wananchi, UKAWA hawana mpango maalum juu ya mambo muhimu yanayowakwaza wananchi isipokuwa kupitia mapungufy ya CCM inanipa shida sana kukupongeza kwa sababu hii ni ahadi tu kama ahadi nyinginezo. Kwa bahati mbaya sana tupo wengine tunaojua serikali hufanya vipi kazi zake, na tumeona wabunge wa Upinzani wakibakia kulaumu tu CCM juu ya ukosekanaji wa maji, barabara au huduma bora katika majimbo yao maana wao hawana jukumu wala meno ya kupeleka maendeleo hayo majimboni ila lugha za udanganyifu tu wapewe kura.

Tunakutakia kheri kwa maamuzi yako lakini fikra zako zitabakia hapa JF kwa sababu sio fikra za pamoja zinazounda umoja wa UKAWA. Na kibaya zaidi ni kwamba mpango wa kugawana majimbo ili UKAWA iwe na viti vingi Bungeni ni mpango wa kusadikika haswa ukizingatia kwamba bado tunatumia katiba ya zamani. NEC ipo chini ya CCM, TISS sio chombo huru, Polisi sio chombo huru, mahakama na jaji mkuu sio mtu huru. Hawa wote watalazimka kukitumikia chama. Na iwapo CCM watataka kuhakikisha UKAWA hawapati asilimia 50 bungeni UKAWA hawatapata, na bakora mtacharazwa! Kama leo mmeshindwa kwenye katiba Mpya mkainua mikono na kubakia kulaumu, mtaweza vipi kufanya tofauti ikitangazwa mmeshindwa Uchaguzi!
 
We mbeba sumu nani akupeleke bungeni, badala ya bungeni utaelekea Jela Magereza
 
Mi nilifikiri maamuzi magumu kweli kumbe upuuzi tu. Jimbo la Rombo lisahau wanarombo bado wanampenda Selasini
 
Ben na hicho kigugumizi chako utachangia hoja gani bungeni? we endelea kutumwa tumwa chips mayai na Mbowe hapo Ufipa
 
Sasa ACT wanatoa wapi ujinga wanao andika. Mods mko wapi au tuamini mnaibeba ACT?? Taarifa nyingi zinazoletwa na hawa mamluki ni za uongo. Tumeona hata Zitto akitoa taarifa za uongo na mnazipokea. Hata pale walengwa wanapokanusha mods mnakaa kimya

Mkuu, huu mchezo haufanywi kwa bahati mbaya.......Mods, watu wetu na hao wazushi wa ACT wote ni 'mazganyanza'
 
Alichokifanya Ben ni kitu kibaya sana japokuwa baadhi mnafurahia kwa Ben kukanusha na kutangaza nia. Kulikuwa na tatizo gani kwa Ben kuja kukanusha taarifa kabla ya watu kuanza kufunguka kwa kauli chafu?
 
Back
Top Bottom