Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naelekea Bungeni
Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo.
"Naelekea Bungeni"
Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.
Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo;
Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics).
Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi.
Duh,
wale waliokuwa wanarusha marusi???? kama walevi sijui wataanzia wapi sasa.
Ben Saanane nakushauri ufanye editing ndogo sana lakini ya msingi katika huu uzi wako.
Ben,hebu mshirikishe mungu japo kidogo kwa kuongeza neno/maneno haya: "mungu akipenda nitaelekea bungeni" au vyoyoye vile utakavyoona inafaa kwani mungu ndio muweza wa yote na hakuna mwenye uhakika wa kuiona kesho.