Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Nimefanya Maamuzi Sahihi na Makini Niliyoahidi Takribani Saa 72 zilizopita, Naelekea ....

Bensa8 mimi siwezi kukutakia safari njema au mbaya ya kisiasa bali niseme tu Mungu akupe unachostahili katika harakati zako huku ukikumbuka kwamba What goes around comes around.
 
Kama utasimama jimboni kwangu, kura yangu nitakupa. Kama utasimama jimbo ambalo sitawezafika kupiga kura, support yangu nitakurushia kwenye m-pesa/tigo pesa. Kila la kheri Ben
 
Bado Ben una mtihani mmoja tu, ikiwa hautapitishwa na chama kugombea hiyo nafasi je? Utakubali au ndio hapo utachukua uamuzi mwingine.
 
Pasco
Ninashangaa kweli,kama unafikiri vizuri,Mdee amesaidia kutatua migogoro ya ardhi kinondoni,
Mdee amesaidia wananchi wa Mabwepande kupata stahiki zao,

Mdee,amefanikisha ujenzi wa barabara za kawe,
Mdee,amesaidia kumbana aliyekuwa waziri wa ardhi hadi pamoja nasakata la Escrow,ameiweka ccm njia panda,
Mdee,ziara yake ya Magu alisababisha chadema mitaa 14,na ccm 4,ziara yake ya kigamboni pale vijibweni imesababisha uchaguzi wa mitaa ccm1,chadema5 utasimama kweli kueleza kuwa Mdee hafai KAWE?, Haya ccm leteni huyo material wenu! Ushauri huu unafaa kutolewa kwa Diwani wa ccm wa Buguruni na si kwa Dr.Slaa Katibu Mkuu wa chadema
 
Ben Saanane nakushauri ufanye editing ndogo sana lakini ya msingi katika huu uzi wako.

Ben,hebu mshirikishe mungu japo kidogo kwa kuongeza neno/maneno haya: "mungu akipenda nitaelekea bungeni" au vyoyoye vile utakavyoona inafaa kwani mungu ndio muweza wa yote na hakuna mwenye uhakika wa kuiona kesho.
 
Last edited by a moderator:
Hongera muhimu usiwasahau wananchi utakapopata madaraka
 
Haya nenda mwenyewe, mie sina muda wa kukusindikiza!Msomi kumbe buuuree kabisa, itabidi tuwaombe TCU wa verify degree hizo,maana akili kubwa haiwezi kusombwa na kuongozwa na ndogo hata kwenye upuuzi!Kwa ushauri Nenda ACT wazalendo achana na ndio mzee za kwa Mbowe!
 
“Naelekea Bungeni”



Mathalan, kwa kipindi kifupi sana tumeweza kuzindua sera tano mpya za chama ambazo ni Sera ya Elimu(ambayo zaidi ya 75% serikali ya CCM imeinakili na kuifanya sera yake ya elimu),Sera ya Maendeleo ya Vijana,Sera ya Afya,Sera ya Uchumi na Sera ya Nishati na Madini. Sera hizi mpya zimetoa mwelekeo bora kabisa wa serikali ijayo ya itakayoundwa na chama chetu kama sehemu ya Serikali ya Umoja wa UKAWA, serikali inayosubiri kuapishwa miezi saba ijayo.

umesoma kijijijini na asilimia 80 ya watanzania waliowengi ni wakulima lakini hamna sera ya kilimo. vipaumbele vyenu ni kwenye kura (sera ya ajira kwa vijana ) na kwenye pesa (nishati na madini).
 
Tupo pamoja kamanda ben karibu mbeya vijijini safari yetu ni moja kuelekea magogoni!!
 
"Naelekea Bungeni"

Ndugu marafiki zangu wa karibu na wa mbali, Baada ya kupitia taarifa ya kamati za kiutafiti iliyokamilisha kazi yake jana kutoka jimboni mniwie radhi kwa kukawia dakika kadhaa kuitimiza ahadi hii niliyoidokeza takribani saa 72 zilizopita kutokana na dharura iliyojitokeza ya kiutendaji katika majukumu yangu ndani ya chama ngazi ya taifa,majukumu yaliyokua na maslahi mapana zaidi kwa chama chetu na taifa kwa ujumla.

Naam, naelekea bungeni. Nimeamua kwa uhakika kabisa kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia chama changu – Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tangazo langu hili limezingatia mambo yafuatayo;


Nimekulia na kusoma katika mazingira ya kawaida kabisa ya vijijini ambako wanaishi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Nimesoma Shule ya Msingi Hiti iliyopo Kijiji cha Mrere Wilayani Rombo na kujiunga na Shule ya Sekondari Lyamungo kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Galanos Mkoani Tanga. Mwaka 2005 kwa udhamini wa Serikali ya Tanzania nilijiunga na Chuo Kikuu cha Allahabad nchini India na kusomea Shahada ya Biashara nikibobea katika masuala ya fedha. Mwaka 2008 nilijiunga na Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Uchumi(M.A Economics).

Kutokana na mapenzi yangu katika fani ya Diplomasia na siasa za kimataifa nilijiunga na Chuo kikuu cha Annamalai na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Kwa sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sera na Uongozi (Ph.D in Governance and Policy Analysis) kwenye Chuo cha Maastricht nchini Uholanzi.

Nakuunga mkono kwenye endevour yako mpya kasoro hapo kwenye nyekundu. Kimoja kita-suffer, ama hiyo elimu unayoenda kuchukua au wanajimbo wako. PhD is what people interested in academic research pursues,other than that it is useless outside the Academic world. whichever tools you need, can be had at Master level.

Huu utamaduni wa kurundika PhD just for the sake of it, is slowly becoming a national tragedy. Nafasi uliyoichukua huko Uholanzi, ingeweza kwenda kwa mtanzania mwengine ambaye ang-dedicate muda wake na energy zake zote wakati wa kufanya PhD na mara baada ya kumaliza into academic research. If i were the department processing an application of such a student i would flat out deny you enrollment. and if i were a voter in Rombo i would question where your focus lies.

Just recently we were having discussions on research impact of PhD holders in Tanzania and if you go ahead and take this route, i will not expect anything on research impact from you.The only consolation will be if you have impact to your electorates, for which you do not really need a PhD to have.

You could raise a point that, you need skills necessary to negotiate your way around governance and policy making, well, you do not a PhD to do that.

That is just my humble opinion.
 


At least sasa wengine siye wenye kuona uchungu na Nchi hii tunaweza kupumua.
Mkuu Ben Saanane Hongera kwa ujasiri huo naamini umepima kila angle katika kufika uamuzi huu.


Jamabo moja muhimu-uamuzi wako huu wa kuwa Mbunge lazima uendane na mkakati wa Jumla wa Idadai ya kutosha ya Wabunge wa UKAWA wauhakikia na watu wenye misimamo moja ya Maendeleo ya Majimbo yao ,lakini kubwa masilahi mapana ya Nchi kwa 100yrs to come.
 
Last edited by a moderator:
Will support you all the way. You go bro!
 
good boy hayo ndio maamuzi ukiyasikia unapata afya.
 
Hayo yote yawe na impact kwa maisha ya watanzania,isiwe kama CV ya Muhongo kwenye Kabati na majigambo
 
Excellent! Bilashaka wananchi jimboni watakuelewa.....watatusaidia kuwa nawe bungeni! ......Naliona bunge la 2016 likiwa 'analytical'......ndiooooooooo.....za magamba zikipotea.
 
Kumbe waliosema unahamia ACT ni wazushi!!! Washindwe na walegee
 
Ni jambo lakutia moyo sana na Mungu akuongoze katika njia makini Ben Saanane
 
Last edited by a moderator:
Ben Saanane nakushauri ufanye editing ndogo sana lakini ya msingi katika huu uzi wako.

Ben,hebu mshirikishe mungu japo kidogo kwa kuongeza neno/maneno haya: "mungu akipenda nitaelekea bungeni" au vyoyoye vile utakavyoona inafaa kwani mungu ndio muweza wa yote na hakuna mwenye uhakika wa kuiona kesho.


Chadema wanjitapa kuwa wameanza na Mungu, Mungu gani wanayeshindwa kumtambua ktk mabandiko yao na kazi zao kwa ujumla.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom