Nimefanyia kitendo hiki kwenye daladala

Nimefanyia kitendo hiki kwenye daladala

Juzi nakula mitaa fulani usiku nikaona mhudumu mmoja wa kike anajisogeza na kuanza kunipigisha story. Nimekula huku tukipiga story, nimemaliza nasikia sauti ya chini akisema "kaka ninulie basi sijui dragon au red bull."

Nikamwangalia nikamwambia, "dada sijatembea na bajeti hiyo usiku huu."

Basi akakaza sura. Nikajiuliza, sasa anakasirika nini wakati mimi ndio najua bajeti yangu ilivyo!!!? Duniani na watu...
 
Huu utamaduni wa kurudishana nyuma kwenye nauli ukome.

Usipoithamini 400 utawezaje kuithamini 10, 000 ambayo inaundwa na 400 mia nne nyingi???

Mtu unakuta anapanda gari tatu au nne na kila gari anakutana na anayemfahamu either anasali naye, anafanya nae kazi au alisoma nae, atalipia wangapi wakati hawakujua kama watakutana naye ili awalipie???

Wadada acheni kuwa BINADAMU MAKUPE.

Nakupongeza sana kaka. LIWE FUNDISHO KWA MAKUPE WOTE.
 
Umeonyesha ukomavu, ungemlipia angesema "unamsumbua kwa ajili ya 400 tu" uko vizuri saaana.... Ila yeye ndo kaonyesha udhaifu mno... Kujilipia kungemuongezea thamani Kubwa. Mule Mule tu..... [emoji121]
 
Hakuna baya ulilofanya, hiyo ilikuwa budget yako. Tatizo ni "mila zetu", zamani kule kwetu walikuwa wakipika chungu kubwa la kande, kila anayepita anakaribishwa kula na ilikuwa lazima ale.

Life's changed, ni mwendo wa budget. Kidogo kidogo tunakuwa "wachoyo" kama huko mbelez.
 
Back
Top Bottom