Nimefika Tabora, nawaambia wanipeleke mjini wanasema ndio hapa tulipo!

Hahah
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
ni wale wale mm kwetu Dar kumbe kwao mpaka upande bus, Kisha Bodaboda dk 50 mpaka 90 Kisha upande mtumbwi Ili kuvuka mto na Kisha upande mlima...hahaha ...
 
Geita nimetoka juzi hela ipo yakutosha tu ukiwa ma connection
 
Tatizo mnakalilishwa na nyie mnameza hivyo hivyo ngoja tukuambie tangu uhuru wa Tanganyika 1961 mpaka 1990 Tabora ndio ulikuwa mji ambao ukitoka dar es salaam na Tanga basi nenda Mboka manyema kila kitu unakipata kumbi za burudani sehemu za starehe zilikuwepo na wazee walienjoy maisha uliza Tabora jazz miaka hiyo ikipiga ule ukumbi wa mtaa wa rufita jirani na kina ismal aden rage sawa kulikuwa na hotel nyota tano Tabora hotel ikiwa chini ya shirika la railway bonge la hotel vijana walicheza disco hapo miaka hiyo kulikuwa kuna rufita club ikimilikiwa na shirika la railway kulikuwa na swimming pool, viwanja vya Table tennis, michezo ya squashi, ukumbi mzuri wa burudani kaunta nzuri ya kisasa aisee muulize mr teacher kaka yake na Prof jay enzi hizo baba yao mzee haule yupo shirika la posta na simu pale Tabora

Umeona kwaiyo Tabora ilikuwa dubai ya mikoa ya kigoma, mpanda, mwanza, singida, Musoma, Bukoba uko watu wa uko walikuwa wakifik Tabora wanajihisi wapo Newyork City maana mji ulichangamka kutokana kupitiwa na railway hivyo, mashirika yote ya umma yalikuwepo Tabora hivyo watumishi kutoka mikoa yote Tanzania walikuwepo Tabora

Watumishi wa shirika la national miling, kulikuwa na kampuni ya usafirishaji Tabora KAUTA, posta na sm, Railway, jeshi la wainchi kambi kubwa tz ya milambo blanks, shirika la ndege air Tanzania, Tabora ilikuwa ya moto balaa watumishi wa umma kibao

Upande wa elimu kuna chuo cha uhazili enzi hizo ukitaka kuwa secretary haina uende chuo cha uhazili Tabora, haya chuo cha uwalimu Tabora wauize kina mzee Rukuvi wamepita hapo kuna shule za serikali milambo boys, Tabora boys, Tabora girls, pia kuna seminari ya itaga kule kina Dr slaa, kina marehemu membe wamesoma hapo so Tabora ilikuwa ya moto shule ya private uyui vijana kutoka kigoma mwanza musoma walikuja Tabora kukaa magetoni wanasoma hapo maana uko mKwao poring shule hizo hazipo

Kuhusu burudani ndio balaa sasa kulikuwa na disco la Tabora hotel, mwana isungu, muungano mess, na ukitaka sinema basi nenda pale Diamond umeona yani mambo ambayo mnasema sijui dad wapi leo hii miaka hiyo mikoa yenu mapori umeme haupo wanyawezi wa Tabora wanayo nini sasa kinafanya mseme Tabora haibadiliki


Baada ya nyerere kuachia madaraka mwaka 1985 na mzee mwinyi kuchukua inchi na kusema ruksa basi kuanzia 1990 mkoa wa Tabora ukaanza kupigwa gape na miji kama mwanza, dar nasema mwamza dar ilia za kukuwa kwa kasi sana kwaiyo kuanzia 1990 mpaka 2010 Tabora ilipowa sana ikawa haibadiliki


Ila kuanzia 2010 mpaka sasa Tabora imeanza jirudia kihakisia wake mji umebadilika sana tena sana anayesema Tabora haibadiliki aijui Tabora vizuri ila Tabora imebadilika sana

Na ambao wanasema ule mji wa kimwinyi sijui hawataki kazi jamani nimewambia huo ndio ulikuwa mji wa bata na starehe miaka hiyo ina maana gani wakazi wengi wa Tabora mjini mnaowaona siyo wanyawezi asilimia mia wengi wao ni wakuja wazazi wao walikuja miaka ile kufanya kazi katika mashirika ya umma niliyosema kwaiyo Tabora mjini pale kuna mchanganyiko wa makabila yote unayoyajua inchi hii so wazazi walikuja wakazaa wengine hawakurudi makwao wakaacha vizazi vyao hapo kwaiyo wanajiita wanyawezi ila siyo wanyawezi utakuta wangoni, waha, wahaya, wakulya kakua kwao hawakujui basi wanasema wao wanyawezi wa Tabora na huo uvivu umetokana na asili za familia zao wazazi wao miaka ile walikuwa wajiriwa wengine vibarua kwaiyo mahitaji nyumbani yalikuwepo so vijana hawakufanya kazi hii sawa na leo hii angalia wazaliwa wa kinondoni au ilala hapo vijana wengi wajanja wajanja tu shule hakuna kujituma hakuna sababu wamezaliwa mijini walitegemea wazazi wao watafute wao wale ndio maana unakuta dada wanazalia nyumbani hivyi hivyo the same na Tabora pale umjini ndio umesababisha pale vile mama malaya mtoto malaya shule hawataki sababu ya umjini

Hiyo hata wewe Kama upo mjini omba mungu kizazi chako watoto wa mjini wengi kazi hawataki shule hawataki yani tuombe mungu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…