Mzee Said bila kuutaja ukoo wa kina Sykes hasikii raha wala amani mwenyewe ana mahaba mazito na huo ukoo nikipata rafiki wa hivi sio hawa wa sasa.
Njumu...
Si mimi niliyeona umuhimu wa Sykes katika historia ya Tanganyika.
Tuanze na John Iliffe 1968 yeye ndiye aliyesababisha maisha ya Kleist Sykes yawe documented na kuwekwa kama seminar paper Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam East Africana.
Mwaka huo huo akaandika paper kuhusu African Association akitumia nyaraka za Sykes.
Mwaka wa 1970 John Iliffe akaandika historia ya Dar es Salaam Dockworkers Union na kumtaja Abdul Sykes.
Kisa Cha kusisimua sana
John Iliffe 1973 akatoa kitabu, "Modern Tanzanians," ndani Kuna sura nzima kuhusu maisha ya Kleist Sykes.
1924 Kleist Sykes anakutana na Dr. Kwegyr Aggrey.
Ukiwa humjui Dr. Aggrey ingia Google.
1950 Abdul Sykes anakutana na Jomo Kenyatta Nairobi.
1950 Abdul Sykes anakutana na Earle Seaton.
Ikiwa humjui ingia Google
1963 Abdul Sykes anakutana na Lady Judith Listowel.
Ikiwa umfahamu ingia Google.
1952 Abdul Sykes anakutana na Julius Nyerere.
Hapa kuna historia ndefu sana.
Ipo katika kitabu cha Abdul Sykes.
1953 Ally Sykes anaandikiana na Kenneth David Kaunda. wa Northern Rhodesia.
2008 Prof. Emmanuel Akyeampong wa Harvard anamuomba Mwandishi aandike maisha ya Kleist Sykes kwa ajili ya Dictionary of African Biography.
Siwezi kuandika yote.
Si mimi peke yangu mwenye mapenzi na historia ya Sykes.