Mohamed Said, ukiona umefukuzwa pahala ujue watu wamechoka na ujumbe wako ulioupeleka. Tangu nikufahamu ndani ya jf kila wakati unaandika negativity za Nyerere dhidi ya Waislam. Kifupi unapalilia udini!! Si kwamba watu wanakuchukia, hapana, wanachukia jumbe zako.
Glenn...
Hapana huwezi kuchoka kusoma historia hii.
Si kama najisifu ''track record'' inaonyesha hivyo.
Niko full booked ''Nyerere Day.''
Ukipenda ingia You Tube angalia video za nyuma Nyerere Day nimezungumza stesheni ngapi?
Sioni hiyo ''negativity'' labda utuwekee hapa kila mtu ashuhudie.
Kusahihisha historia iliyofuta ni kupalilia udini?
Vipi kufuta historia ya Waislam hicho ni nini?
Mimi sijahisi hata siku moja kama nachukiwa.
Sijua wewe hili kuwa nachukiwa umelipata wapi?
Naandikiwa na watu wengi sana wakiomba kunitembelea.
Hapa JF nimekuwa Mwandishi Bora Jukwa la Historia mara mbili mfululizo mwaka wa 2021 na 2022.
Maktaba yangu ni kati ya Maktaba tatu bora zilizosheheni historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Maktaba ya Salim Ahmed Salim, Brig. General Hashim Mbita na yangu Mohamed Said.
Haya yameandikwa kwenye kitabu: ''Nyerere Biography'' (2020).
Je, hizi ni dalili za mtu anaechukiza?