Nimefukuzwa tena kundini

Nimefukuzwa tena kundini

Wanakubali kiaina
View: https://x.com/HistoriaYetu/status/1705320440720245240?s=20

Hapa historia inatuonyesha Ali Sykes ndie alietoa wazo na kumpa Nyerere, cha ajabu wachangiaji wote wanamsifia Nyerere Ali Sykes ahatajwi kabisaa.


HISTORIA ITAKAYODUMU MILELE KWENYE SEKTA YA AFYA TANZANIA.

➡️ Mapema tu baada ya Tanganyika kupata uhuru wake 1961, wauguzi wengi wakizungu walianza kuondoka na kurudi kwao Uingereza, walipoulizwa kwanini wanaondoka katika wakati ambao raia wa Tanganyika wanawahitaji sana kwenye sekta ya afya, wakajibu hawako tayari kuwa chini ya serikali ya mtu mweusi.

➡️Likawa piga kubwa kwa Mwalimu Nyerere na Watanganyika, Mwalimu aliketi chini ya Ally Sykes, mtu aliyeaminiwa mno na Mwalimu kwa akili na maarifa yake. Enzi hizo, walimwita Ally Sykes ‘The Godfather of Dar Exiles’ kwa uwezo wake mkubwa wa kupanga mipango.

➡️Ally Aykes na Mwalimu waliafikiana kwamba wakazungumze na Oliver Thambo, wakati huo Thambo alikuwa uhamishoni Jijini Dar es Salaam, na alikuwa kiongozi wa ANC wakipigania uhuru wa Afrika Kusini kutoka ukimbizini Tanganyika.

➡️Oliver Thambo alikubali kuchukua wauguzi wa Afrika Kusini waje kusaidia kutoa huduma Tanganyika. Ni wauguzi hao waliokuwa chini ANC ambaoo ANC kwa muda mrefu, iliwekeza kwenye maeneo mbalimbali ili kuwa na wataalamu wake.

➡️Oliver alituma ujumbe haraka kwa wenzake Afrika Kusini. Kisha mpango ulianza kusukwa kwa umakini ili kutobainuka na Serikali ya kikoloni.

➡️Wauguzi 20 waliandaliwa. Wakiwa bado wasichana vijana, walikubali kuweka rehani maisha yao wakati wa kusafiri kuja Tanganyika. Kwa vyovyote vile walijua kuwa kuvuka mipaka ya Afrika Kusini inaweza kuwa salama au si salama kwani serikali ya kikoloni ilikuwa makini kona nyingi za nchi hiyo.

➡️Katika orodha yao waliwepo Edith Tunyiswa, Kholeka Tunyiswa, Nomava Ndamase, Eduth Ncwana, Mary Soconywa, Natalie Masimang na wengine.

➡️Wauguzi hao walitoka Afrika Kusini kwa basi ndogo na kupita mpaka wa Botswana. Dereva wa bas hilo alichukuliwa kijana mzungu wa Chuo kikuu cha Wits ambaye alikuwa amejipambanua kama Padre na hivyo kuwa rahisi kuvuka. Maakini ya Mungu askari wale mpakani hawakujua kuwa wameingizwa mjini na Mwalimu Nyerere na Ally Skyes kupitia Oliver Thambo.

➡️Walifanikiwa kuvuka na kuendelea na safari hadi kwenye ngome ya chama cha ANC iliyokuwepo Botswana. Ni katika jumba la Kaitseng House eneo la Labatse. Hapakuwa na maiba wowote na hivyo hawakwenda kwenye mazishi kama alivyoeleza dereva wakiwa mpakani. Hapo kilikuwa kituo chao cha kwanza tangu watoke Afrika Kusini.

➡️Walipumzika hapo kwa muda wa mwezi mmoja wakiwa wanapata mafunzo ya ziada kuishi ugenini. Kwa sababu waliacha ndugu zao, wapendwa wao, mali zao na mambo mengine kisha kukubali kuja Tanzania kuokoa afya za Watanganyika.

➡️Mwalimu Nyerere na Ally Skyes kupitia Oliver Thambo waliweka mkakati kwamba wawacheleweshe kidogo wauguzi hao ili kuwazuga maafisa wa serikali ya Afrika Kusini wakati huo. Basi baada ya mwezi mmoja waliokuwa nchini Botswana, ilikuja ndege maalumu kutoka Tanzania. Ndege ilikuja kwa kazi maalumu ya kuwachukua wauguzi hao hadi kuwasili Tanganyika salama.

➡️Ikawa hatua kubwa ya mafanikio makubwa ya Mwalimu Nyerere na Ally Skyes katika sekta afya ingawa idadi ilikuwa ndogo lakini walikuja kutumia mbinu nzuri ya kwamba wauguzi hao wakiwa wanafanya kazi yao, pia watumike kutoa mafunzo Watanganyika wengine waliojiunga na fani hiyo.

➡️Kholeka Tunyiswa alipelekwa Tanga. Baada ya kufanya kazi kwa muda huko Tanga, alihamishiwa Iringa. Baadae alipelekwa hospitali ya Mwananyamala iliyopo Dar es Salaam. Pia, alifanya kazi hospitali ya Mnazi Mmoja na Magomeni zilizoko Dar es Salaam.

➡️Edith Tunyiswa alipangwa Mbeya. Huko Mbeya sifa zake zikawa za kutukuka sana. Alifanya kazi kwa ziada ya pale alipotakiwa kuishia. Alitumia pia mshahara wake kusaidia watu waliokuwa na shida mbalimbali. Aliwasaidia chakula na malazi Waafrika Kusini walioingia nchini kuomba hifadhi Dar es Salaam kupitia Mbeya. Sifa zake ziliwavutia wengi. Kijana mmoja wa Tanzania alijitosa na kumposa Edith kisha walifunga ndoa hapa hapa Tanzania. Vilevile Kholeka Tunyiswa aliolewa Dar es Salaam.


F6qD5NnWsAAXyMA.jpg
F6qD5NmXUAAYPZR.jpg
 
Glenn,
Unadhani Maaskofu wameelewa?
Msikiti una uhusiano gani na DPW?

Masheikh ni tofauti na Maaskofu hawana uwezo wa kuikaripia serikali wala kumfukuza mtu msikitini wala kufuta dhambi zake.
ila wana uwezo wa kufuga majini na kuandika kombe huku wamekariri Quran kama makasuku
 
Back
Top Bottom