Unatolewa kwenye makundi pengine kwa sababu stori yako ni moja tu ya Sykes
Huchangii mada nyingine, wewe ukiamka ni Sykes, ukishinda ni Sykes, Ukilala ni Sykes. Kiufupi pengine unateka makundi kwa mjadala mmoja.
Hebu jirekebishe uanze kuchangia mada nyingine za kijamii n.k
Unawachosha watu na mjadala "mono"
Missile,
Historia ya Sykes ni ya ukoo mmoja lakini imebeba historia ya wazalendo wengi na mambo mengi sana.
Inakwenda nyuma miaka 100 na imethibitishwa na matukio ya kihistoria.
Inaanza na Shaka na kutoka kwake Afrika ya Kusini unakuja Mozambique Imhambane kijiji cha Kwa Likunyi hapa unamsoma Hermann von Wissmann.
Huyu ndiye aliyewaleta Sykes Pangani, Germany Ostafrika mwishoni mwa 1800 kama askari mamluki.
Hapa Sykes unawasoma pamoja na Abushiri bin Salim na Mtwa Abdallah Mkwawa katika vita.
Unakuja Vita Vya Kwanza Vya Dunia unakutana na Kleist Sykes na Von Lettow Vorbeck wanapigana na Waingereza Mwele Juu, Tanga.
Kleist anakutana na Dr. Kwegyir Aggrey mwaka wa 1924.
Naamini unaijua historia ya Dr. Aggrey.
Historia hii yote Kleist kaiandika.
Abdul Sykes anakutana na Jomo Kenyatta Nairobi 1950.
Abdul anakutana na Earle Seaton.
Unaujua mchango wa Earle Seaton katika uhuru wa Tanganyika?
Abdul Sykes anakutana na Julius Nyerere nyumbani kwake Dar es Salaam Mtaa wa Stanley baadae ukawa Mtaa wa Aggrey 1952.
Naamini unamjua Julius Nyerere katika historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Afrika.
Hii si historia ndogo.
Nimeandika kitabu na yaliyo ndani ya kitabu hiki ndiyo haya tanayojadili hapa sasa zaidi ya miaka 10 na kila siku historia hii inawavutia wasomaji wapya.
Hakuna aliyechoshwa na historia hii mngechoshwa mngekuwa kimya.
Yule anaeisoma historia hii kwa mara ya kwanza hawi kimya lazima ataniandikia.
Hii ndiyo sababu ya mimi kurejea hapa tena na tena na historia ya Sykes.
Hii ndiyo sababu ya kitabu cha Sykes kuchapwa mara nne kwa Kiingereza na Kiswahili toka kichapwe London 1998.
Kitabu kimewagusa wengi.
Historia hii si ya kawaida hasa kwa kuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni sehemu ya historia ya Abdul Sykes.
Hii ndiyo sababu vyombo vingi vya habari kunifanyia mahojiano BBC, SABC, DW, Al Jazeera, TBC1, AZAM na stesheni nyingi za TV Online.
View: https://youtu.be/9wacS4y7IBY?si=WPDjgd-97bzHXa-n