Nimefukuzwa tena kundini

Nimefukuzwa tena kundini

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NIMEFUKUZWA TENA

BAADA ya kuweka video hii ya TBC nikatolewa kundini:


View: https://youtu.be/-bwoz3jI7RA?si=rJdx_0PlMIHxm4Wm

Nilikuwa kwenye group moja nikafukuzwa naamini wengi mlisoma makala ile.

Bahati nikawa nimebakia katika group kwa no. yangu nyingine ambayo siitumii sana na kwa sababu hiyo ikawa sijui kama bado niko kundini.

Nikajiambia mwanzo hapa nimetimuliwa kwa makala niandikazo na moja ya sababu nilielezwa sielezi vizuri historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Nikaamua kuanzia sasa hapa kundini nitaweka vipindi nilivyofanya na TBC, AZAM na stesheni nyingine na vikarushwa kwa wananchi wote wa Tanzania.

Niliamini kwa kufanya hivyo nitakuwa nimewadhihirishia viongozi wa group kuwa Mohamed Said anakubalika hadi na vyombo vikubwa ikiwemo TBC.

Nikaweka video kama tatu hivi nazungumza historia ya Baba wa Taifa. Haikunisaidia kitu.

Nadhani nimedumu kundini kwa siku kama tatu hivi leo wamenifukuza.

Inaelekea historia ya Mwalimu Nyerere itakiwayo ni ile ya zamani yuko peke yake wasitajwe wenzake
 
Kuna watu historia ya Nyerere wanavyoielewa kuwaambia mambo mengine ni sawa na wewe kuambiwa hiyo Dini Yako ni feki kamwe huwezi kukubali.

Taratibu wataelewa Mzee wangu. Kama Kuna haja tuanzishe group letu huko unashusha mizigo unavyoweza.
 
Wanamwachaje Abdul Sykes 😁 😁

Pole Mzee Wangu
Syllog...
Ukimwacha Abdul Sykes utafikaje kwa Dr. Kwegyir Aggrey aliyemtia hima baba yake Abdul Mzee Kleist kuunda African Association 1924?

Utamwingizaje Julius Nyerere katika TAA Dar-es-Salaam 1953?
Utapataje kadi tatu za mwanzo za TANU?

TANU Card No. 3 Abdul Sykes, No. 2 Ally Sykes na No. 1 Territorial President Julius Nyerere.
Utafikaje katika mitaa hii?
 
Kuna watu historia ya Nyerere wanavyoielewa kuwaambia mambo mengine ni sawa na wewe kuambiwa hiyo Dini Yako ni feki kamwe huwezi kukubali.

Taratibu wataelewa Mzee wangu. Kama Kuna haja tuanzishe group letu huko unashusha mizigo unavyoweza.
Puna,
Nina wanafunzi hapa JF sijui idadi yao.
Huko niliko post zangu zinasukumwa mbali kwa kasi ya kushangaza.

Hatuhitaji group letu.
Ahsante kwa fikra yako.
 
Glenn,
Unadhani Maaskofu wameelewa?
Msikiti una uhusiano gani na DPW?

Masheikh ni tofauti na Maaskofu hawana uwezo wa kuikaripia serikali wala kumfukuza mtu msikitini wala kufuta dhambi zake.
1. Msikiti una uhusiano sana na DPW, kuna fununu kuwa watajenga msikiti mkubwa sana Mbeya, hii imekaaje?

2. Ni ajabu sana karibu waislam wote wameuelewa mkataba wa bandari kuliko wanasheria...hii imekaaje? (PAMOJA NA ELIMU YA MASHEIKH NI TIA MAJI TIA MAJI LKN MKATABA WAMEUELEWA KWA HARAKA SANAA)

3. Masheikhe wengi wametoa matamshi tata ya kuwakemea na kuwakejeli TEC waliochagua kulinda maslahi ya nchi...hii nayo imekaaje?

Kuna HARUFU YA UDINI ULIOJIFICHA CHINI YA DPW.

Nikwambie tu, moto huwezi kufunikwa na kipande cha khanga mzee Mohamed, tusubiri, tuombe uzima
 
Wewe mzee nakufikiria sana enzi zako ulikuwa mjanjamjanja sana.

Una mambo fulani hivi hutaki yakupite licha ya umri wako.

Kumb. Sisi wengine ni wajukuu zako kwahiyo kwenye uzi wako usishangae tukaleta utani utani wa mjukuu na babu.

Nakuja kukuibia mke mzee wangu
 
Back
Top Bottom