Kasanzu The Great
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 310
- 223
Jana nilifarijika Sana kuona Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan akiwa amesarika na kuona hadharani wale wote wanaotafuna Mali za nchi. Alilazimika mpaka kutumia neno '' Stupid'' katika hotuba yake.
Siku za nyuma nilikuwa naingia na wasiwasi juu ya kauli zake za ' 'sitafoka" sitaki nidhamu ya woga nataka nidhamu yandhati'" kwa kauli hizi niliona kama vile Mama alidhani JPM aliwaonea wabadhirifu na wapigaji.
Nilidhani kuwa wale waliokuwa wanafokewa na JPM pengine aliona wanaonewa. Jambo la pekee lililonitia faraja nikwamba alikuwa bado hajajua mambo mengi ya hovyo katika nchi yetu kwasababu taarifa nyingi za kijasusi zilikuwa hazipitii kwake bali kwa Rais Wa kipindi chake.
Sisi wabara hatujawahi kuwa na nidhamu ya ukweli ukweli mbele ya hela, hatujawahi kuwa waadilifu mbele ya hela, sisi hatujawahi kutii mtu bila kumuogopa, taratibu watu walianza kukuona kama mama zaidi Kuliko Rais.
Watu lazima wajue kwamba wewe ni Rais sio Mama. Wanapotekeleza majukumu yako watambue kwamba hawatabembelezwa wala hawatanong'onezwa bali watakabiliwa na adhabu kali za kimaadili na kisheria. Kupitia hivyo nchi itapona.
Mama endelea kufika, ukifoka na ukaonesha vitendo hata yule Mtendaji kata aliyeko mtu kula au mganga aliyeko Tunduma atajua kwamba hii sio zama ya Mama, bali ni zama za Kazi na Rais Wa Jamhuri ya Muungano. Heri kusifiwa na wanyonge kuliko kusifiwa na manyang'au yanayojikomba kwako ili yapate kula.
Mwisho Mama waambie watu wapunguze mahafula na Makongamano yasiyo na tija ili pesa iende kuhudumia wananchi. Mfano Kuna haja gani kuita walimu wa Sayansi kutoka Kagera, Mara, Simiyu nk na kuwakusanya Butimba TTC kwenda kuwasimulia mambo ambayo yako Ndani ya majukumu Yao kila siku kwa wiki moja na kuondoka na fedha za walipakodi? Unahaja gani ya Kuwaita sijui maafisa Habari kuwalundika Dodoma kuwaambia mambo ambayo hata kwenye emails zao ungewatumia tu wakatekeleza?
Mama Asante kwa kutuinesha sura ya Urais