Nimefuta na kublock namba 50 kwenye simu yangu za wanaojiita marafiki zangu

Nimefuta na kublock namba 50 kwenye simu yangu za wanaojiita marafiki zangu

Kama una marafiki 50 basi wewe ni tatizo kuu. Pia mkuu badili fikra zako kuhusu haya maisha. Tambua una wajibu wa kupigania maisha yako kwa 100% bila kumlaumu mtu yeyote kwa namna yoyote. Kuwa-block watu 50 inaonyesha udhaifu mkubwa sana kwa upande wako. Elewa hapa duniani hakuna wa kukuonea huruma zaidi ya wazazi wako hasa MAMA. Ukipatwa na tatizo pambana na mwombe Mungu atatenda muujiza.
 
Pole umechelewa kujua, ila haujachelewa kufanya maamuzi....wafyekelee mbali tu
 
Ujue mkuu,kusaidia mtu sio mpaka utoe hela onyesha hata kuguswa tu.jitu unaliomba msaada linakuzimia simu kweli?
Kuna mwingine haelewi mguso wako bila kumpa hela

Wanasema panapohitaji hela usitumie maneno😅😅😅
 
Mkuu sio lazima utoe msaada wa kifedha.Muda mwingine unaweza kumsaidia mwenzio kwa kumpa tu msaada wa kisaikolojia Kama ushauri nasaha na mengineyo.
Sasa mtu anakwambia niko polisi nahitaji 50,000 au nahitaji 100,000 nina emergency unaanza kutoa nasaha zitasikilizwa kweli?😅😅😅😅
 
Last week siku ya tarehe 31 December, nilipanga nifanye tathmini ya aina ya marafiki zangu nilionao. Kiukweli mimi ni mtu wa kujitoa sana when it comes to matatizo ya wenzangu wanaonizunguka...
Usikute na wao wamekublock kwamba umezidi kuombaomba
 
Umenikumbusha mbali kidogo 2016 ,nilikuwa na jamaa angu yeye alikuwaa na kazi kwenye kampuni fln ya mikopo , opportunity finance LTD bas jamaaa akanimbia anapa posho nyingi Sana na pia wateja wakopaji wanamuonga Sana pesa ,bas na mm nilikuwa namiliki bajaji mpya hvyo kwa kila week ilikuwa napata elf 90 na kwa kuwa Nina bint angu nilikuwa namsomesha shule za kulipia bas ilikuwa January HV HV nikamuomba mshikaji anikopeshe laki moja ili siku wanavyofungua shule nipeleke Kama ada huku najipanga kutafuta namna ya kufanya I'll nipate kulipa Deni lake ,jamaa yule akanikubalia kuwa siku ambayo naenda kulipa ada nimcheki ananipatie hyo laki namm niongeze nyingine nikalipe ada ya mwanangu siku hyo imefika nampigia jamaa akagomaa kbsa kupokea piga wapi wapi andika msg Wala hajibu nikakausha nikamuendee mwalimu akanielewa nikampa hyo nilinayo bas jamaa akawa ananitafuti Tena namm nikakausha huku natafuta ajira mungu huyooo nikapata kazi ndani ya mwezi huo huo nikapewa na pesa za kuazia maisha Kama laki Tisa HV ,siku moja Niko zangu kwenye ukilumbi wa maombi nikishikuru mungu kwa kupata Kaz nikamuona jamaa nikamuona jamaa akaona aibu fln mm nikakausha ,tumetoka ndio anifata ananimbia mwanangu ile kazi yangu s imearibika ndio maana Niko hapa napiga maombi ,alikaa Muda hanioni mtani Wala hajui Niko wapi ndipo alillposikia kuwa nimeajiriwaa kampuni fln Tena mkoani akanataka kurejesha urafiki huku akiniomba link nimtumie nae aombe kazi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Marafiki hamsini wa nini kwenye maisha?Hao waliokusaidia wala sio marafiki zako bali ni watu tu ambao walikuwa na hela zinawawasha na wameshakula zako nyingi kuliko hizi wakaamua tu kuendelea kukuweka karibu.

Pili kuwa na namba ya simu ya mtu haimaanisha ni marafiki zako hio ni connection yako tu.

Tatu mtu kukusaidia au kutokukusaida haina uhusiano na urafiki wala haina uhusiano na wewe kumsaidia au kutokumsaidia.Aina kubwa na kiwango kikubwa cha watu ambao huwa wananisaidia sio wale ambao mimi huwa nawasaidia na wala sio wale ambao ni marafiki zangu au ndugu.

Mwisho siku ukiwa na shida kweli ndipo utajua marafiki wa kweli ila ukiwa na shida ya kutunga utajidanganya tu.

Mwaka mwema wa 2023
 
Watu kama nyie naonaga akili zenu ni finyu sana.
Unapomsaidia mtu unategemea na wewe kusaidiwa au unasaidia kwakua uwezo huo unao bila ya kuathiri uchumi wako!?

Utapoteza wengi mwisho hadi wazazi wako utawacancel kwakua sio rahisi mtu kukusaidia kama hana kitu.
Mtu hana mchuzi, wewe unaomba pesa anakwambia hana unafuta namba yake kama sio akili fupi hiyo ni nini!!?
 
The Monk, naomba soft copy ya hiki kitabu

Sina ndugu yangu. Hichi nilinunua Mlimani City Kuna bookshop ya Mak nafikiri. Kinaitwa The 80/20 principle.

Screenshot_2023-01-06-18-44-12-96_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Last week siku ya tarehe 31 December, nilipanga nifanye tathmini ya aina ya marafiki zangu nilionao. Kiukweli mimi ni mtu wa kujitoa sana when it comes to matatizo ya wenzangu wanaonizunguka, nikisikia msiba wa rafiki ntaubeba kama wetu vile, rafiki akiniomba kitu kama kiko ndani ya uwezo wangu lazima nimsaidie.

Lakini recently kuna viashiria niliviona vikanistua mpaka nikaamua kuwafanyia tathmini marafiki zangu.

So tarehe 31 December 2022, nilijifungia ndani siku nzima, nikaanza kuwapigia rafiki zangu simu kuwaomba msaada kuwa nimepatwa na majanga flani nimetaitiwa na polisi so kuna kiasi flani cha kama elfu 50 kimenipelea hivyo naomba msaada then next day narudisha.

Ebana huwezi amini wale niliokua nawachukulia kama washkaji zangu hakuna hata aliyejigusa na mimi. Ila kuna mdau mmoja tena ni fundi ujenzi nae niliona nimpime coz huwa ananipiga vizinga vya hapa na pale ndiye aliyejitutumua akanitumia elfu 10 akaniambia hiyo nyingine hana nijaribu kucheck wadau wengine.

Na kuna demu mama ntilie nae nilikua nagonga kipindi flani huko nyuma nae akaniwezesha elfu 15, ila hawa washkaji tunaokaa nao kwenye viti virefu hakuna hata aliyeuliza hao polisi wamenitait kwa issue gani!

Kwa kweli hili jambo lilinitafakarisha sana aina ya watu ninaomingle nao katika maisha yangu. Nilichoamua niliblock number zao na kuzifuta kabisa, maana haina haja ya kuendelea kuongozana na watu wa aina hiyo.
Bila screenshot hainogi
 
Ckuiz masnitch Ni wengi Sana kwa kweli.
Kuna watu wanazugaga kuwa marafiki zako ila ukiondoka wanaanza kukudiss kwa watu.
Ikija Kwenye suala la msaada ndio kabisa huwaoni Tena.

Let's choose our friends wisely.
Kabisa
 
Mtu kukusaidia sio kipimo cha Urafikii ila ni kipimo cha mtu ulienae anakujali kiasi gani...! Ukimuomba mtu asikupe sio kwamba kapenda sometimes ni kweli Hanaa.. wengine walishawahi tendwa na waty waliowakopeshaa yani kuna mambo mengi so tuishi kwa kuchukiliana hela ni shetani...!!
 
Imagine mtu una mtongoza dem wake kwa no nyingine na dem ana jibu yuko single [emoji28][emoji28]ndo mwanzo wa kupunguza upendo
Haya mambo ya kujaribiana hayafai kabisa. Unatakiwa umwamini mtu namna alivyo. Tunatakiwa duniani kuishi kwa furaha. Kuanza kuchunguzana chunguzana ni kujipa stress na kufa mapema.
 
Last week siku ya tarehe 31 December, nilipanga nifanye tathmini ya aina ya marafiki zangu nilionao. Kiukweli mimi ni mtu wa kujitoa sana when it comes to matatizo ya wenzangu wanaonizunguka, nikisikia msiba wa rafiki ntaubeba kama wetu vile, rafiki akiniomba kitu kama kiko ndani ya uwezo wangu lazima nimsaidie.

Lakini recently kuna viashiria niliviona vikanistua mpaka nikaamua kuwafanyia tathmini marafiki zangu.

So tarehe 31 December 2022, nilijifungia ndani siku nzima, nikaanza kuwapigia rafiki zangu simu kuwaomba msaada kuwa nimepatwa na majanga flani nimetaitiwa na polisi so kuna kiasi flani cha kama elfu 50 kimenipelea hivyo naomba msaada then next day narudisha.

Ebana huwezi amini wale niliokua nawachukulia kama washkaji zangu hakuna hata aliyejigusa na mimi. Ila kuna mdau mmoja tena ni fundi ujenzi nae niliona nimpime coz huwa ananipiga vizinga vya hapa na pale ndiye aliyejitutumua akanitumia elfu 10 akaniambia hiyo nyingine hana nijaribu kucheck wadau wengine.

Na kuna demu mama ntilie nae nilikua nagonga kipindi flani huko nyuma nae akaniwezesha elfu 15, ila hawa washkaji tunaokaa nao kwenye viti virefu hakuna hata aliyeuliza hao polisi wamenitait kwa issue gani!

Kwa kweli hili jambo lilinitafakarisha sana aina ya watu ninaomingle nao katika maisha yangu. Nilichoamua niliblock number zao na kuzifuta kabisa, maana haina haja ya kuendelea kuongozana na watu wa aina hiyo.
Ndo unaambiwa kufa kivyako.

Unaenda church umelala njaa siku mbili watu umewaambia lakini kila mtu anasema mtegemee Mungu 😀, kibaya zaidi sadaka na michango kwa siku ni milioni kadhaa sasa unashangaa shangaa tu
 
Haya maisha bwana unaweza kudhani mtu amekunyima kumbe hata yeye hana labda unaejua mishe zake hawezi kukosa cash
 
Back
Top Bottom