Nimegombana na Mke wangu leo mpaka nimeshangaa

Nimegombana na Mke wangu leo mpaka nimeshangaa

Usimrudishe kwao ,leeni wote huyo kiumbe . Jaribu kumuelewa huyo mama, kipindi cha ujauzito ni kipindi kigumu sana na hutofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine , hivyo msitoke kwenye mstari
 
Pole mkuu lkn mie kwa uzoefu wangu kuhusu ujauzito ni kwamba
Mimba ya miezi michanga yaani 3/4/5
hii husumbua zaidi kuliko mimba ya miezi 6/7/8/9 kwakuwa miezi hyo mitatu ya mwanzo. hapo ndyo mtoto hufanyik
lkn pia ujauzito wa miezi hyo mtoto huwa achez tumbon hpo ndyo huwa pana kero sana

ushauri
Vumilia vituko vyake vya kpnd kifupi.......
..,heri wapatanishi

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Weacha tu mkuu sababu kuna dada nafanya nae kazi ofisi moja yule dada alikuwa mjamzito yule dada alikuwa anakuja kazini mbaka anajifungua ndo wakampa likizo ya uzazi lakin alikuwa na uwezo wa kuomba likizo before hata ya kujifungua akajifungulie hata kwao lakini wapi mbakatulikuwa tunamuonea huruma kazi nyingine za kiofisi tunamsaidia katoka kujifungua January mtoto wa kiume
Ndiyo mimba siyo ugonjwa lakini simfananishe mkeo mjamzito na wanawake wajawazito unaokutana nao huko mtaani, ni watu wawili tofauti hao, kila mtu hormones za kimba zinamfanya awe kivingine.
 
siku ya kujifungua aanze tena kulalamika, mpe nauli aende akapambane na mama ake mbona atafanya tu mazoezi.
Akiwa kwao wala hatajilaza hivyo.hio anakufanyia wewe tu. Makazin walimu wana.mimba sisi miaka flan mwalim wetu .mwalim galawika ilikua yupo darasan lakin mjamzito na anafubdisha vizuri tu.tenq kasimama.
 
Shukuru hata huyo anayelala. kuna mtu kisa kapata mimba hata hataki kumuona mumewe, hataki walae kitanda kimoja, yaani hata harufu ya mumewe hataki kuisikia. Yakikukuta si utazimia jamaa
 
Inaonesha kichaa cha Mimba umekibeba wewe,
Huwezi ukampigia simu mke wako na kumwambia mijineno yote hiyo na bado umerudi eti umenuna humsemeshi halafu unamwambia kesho unamsafirisha sijui asinyanyasike, lol

Wewe ndie una matatizo jitafakari msije mkamtesa huyo Malaika kwa ujinga wenu.
 
Ndiyo mimba siyo ugonjwa lakini simfananishe mkeo mjamzito na wanawake wajawazito unaokutana nao huko mtaani, ni watu wawili tofauti hao, kila mtu hormones za kimba zinamfanya awe kivingine.
Eti Mama anabeba beseni la Mboga anatembeza wanadhani wanapenda hayo maisha na je wale wanaoandikiwa completely bed rest wanajifanyisha?

Waafrika roho zetu!
 
Mimba changa huwa zinawatesa wanawake wengi sana ukiweza kuuvuka mtihani wa mimba chnga unakuwa mwanaume kamili.
 
Labda utwambie hii tabia imejitokeza tu wakati wa ujauzito au hata kabla amekuwa na tabia hizi. Na hujatuambia hii mimba ni ya ngapi na je km tayari mna mtoto mimba hiyo pia ilileta changamoto km hizi za leo.

NB.
Kabla ya kuoa, mwanaume yakupasa kuwa makini sn hasa kuonesha muelekeo wa maisha wako, misimamo yako na matamanio yako ya maisha waziwazi ili MKE ajue nini unapenda na nini hupendi. Usiogope kumpoteza km utamuweka wazi na akaona hamuendani.

Mimi binafsi huwa nakataa katakata habari za kuhusisha mwanamke kuwa mjamzito na vitendo vitokanavyo na ujauzito huo. Ujauzito sio ugonjwa, sio mzigo, na sio msalaba kwa mume.

Eti wengine wakishika mimba wanasema waume zao wananuka hadi Wana hana vyumva au kulala chini. Serious kweli mimba inaweza kusababisha mume kunuka. "Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe".

Vijana acheni kuishi kizungu eti mwanamke akiwa mjamzito analelewa km yai na ku-misbehave kisa mimba. Na wao wamekuwa wakitumia huu mwanya kufanya vitendo na kutoa majibu ya hovyohovyo kwa waume zao eti kisa mimba inamtuma hivyo. Narudia, kataeni ujinga huo, vinginevyo mtajikuta nyie ndio mmeoolewa.

Mbana sisi tumekuwa tukiona mama zetu wakienda kulima na kufanya kazi tena ngumu huku wakiwa wajawazito, wengine walikuwa wanafanya kazi ngumu hadi siku ya kujifungua. Kwani hao hawakuwa binadamu au wao walitoka sayari gani. Na hadi sasa wanawake km hao wapo wengi na ndoa zao zipo imara.

Hii tabia ya vijana wa kiume kwenda kuoa wanawake wa kishua, wapenda kuvaa vitu artificial mwili mzima, kujikwatua hadi sura zao kubadilika, na wavivu wa kufanya kazi haya ndio matokeo yake. Kijana unaoa kwa kuangalia matako, sura, na umbo kwa kudhani sifa hizo zipo pia kichwani mwa mwanamke. Hatimae ndio unajikuta unaoa mvivu, mzururaji, jeuri, kisirani, katili, kauzu na kila sifa zote za hovyo.

Vijana wa kiume tambueni mwanamke wa kuoa ni tofauti sana mwanamke wa mahusiano ya kimapenzi mnae enda kukutana baa, disko, gesti na sehemu zote za starehe na chafu. Mwanamke wa kuoa hawezi kuwa na sifa zote uzipendazo. Note my words " huwezi kupata mke ,wala mume Bora wa maisha yako mwenye sifa zote unazohitaji, labda umuoe dada yako au uolewe na kaka yako". Kuoa/kuolewa sio jambo la mzaha km mapenzi ya kiurafiki kabla ya ndoa

Pole sana kwa yaliyokukuta mleta mada, maamuzi yako ndio yataleta furaha yako. Kazi kwako ila usikubali kuburuzwa kwa sababu za hovyohovyo km mimba. Wanawake waheshimuni waume zenu acha visingizio vya hovyohovyo km mimba.
Nashawishika kukuona ni miongoni mwa wanaume wakatili Kwa wake zao.Tuwahurumie wake ZETU haswa kipindi Cha ujauzito ukiwa unamsumbua na wakiwa wanaumwa!
 
Habar wana JF,

Nashukuru mungu wote ni wazima
Mtanisamehe mimi sio muandishi mzuri sana wakuu.

Nimetoka kugombana na wife mpaka nimebaki nashangaa na kuwaza kwa maneno alioyasema wife, nikwamba wife ni mjamzito wa miezi 4 sasa anatimiza ikifika tarehe 13 sasa leo nimetoka kazini nikawa nimekaa kwenye gari nawaza sana kutokana na maisha na life style anayoishi wife sio kabsa kiupande mwingine.

Kutokana na maisha yalivyo toka wife amebeba mimba anaishi life style ambayo kwa upande mwingine bado haijanivutia lakin ni kawaida sana yeye ni 24hrs/7days yupo ndani amelala akichoka anafungua insta atashinda mitandaoni akichoka sebleni kuangalia TV tamthilia zake mwenyewe.

Ni vizuri kupata muda wa kupumzika kwa hali yake lakini mimba sio mzigo au mimba sio ugonjwa ukufanye ushinde ndani 24hrs. Nikampigia sim kumjulia hali kashindaje leo then nikamuuliza unafanya nini akajibu yupo kitandani amelala.

Nikamwambia kiupole sana na kiutaarabu kuwa mkewangu em bas uwe unatoka na kuchakarika kuna duka la biashara now yupo kijana uwe hata unakwenda basi kuangalia mambo yanaendaje sio hadi mimi nitoke kazini nimechoka nipitie tena huko wakati wewe upo tu nyumbani umetulia vituvingine ni kuichangamsha akili na kupambana kuliko kushinda tu ndani mamaangu wewe sio mgonjwa.

Kusema kwamba huwez kutembea mbona kuna wanawake wana mimba lakini wanachakalika wengine unakutana nao anatumbo kubwa kabeba beseni lake la mboga anatembeza mitaani wengine wanakimbiza maofisi na matumbo yao tena makubwa lakin wanachakalika asubuh na mapema kashafika ofisi nikamwambia hayo siyo maisha uyaotaka kuishi.

Sijajua nihilo tu au kuna mengine ila Alivimba na kuanza kuongea kwa hasira na kuongea maneno mengi sana ambayo sikutegemea na kusema kuwa namnyanyasa mara kisa kubeba mimba naanza kumuona mjinga so nisimfananishe na hao wajinga ye anaakili zake na anajua anachofanya, mara nimeanza kumuona mzigo kwangu kwakuwa kabeba mimba duuh wakuu nilibaki nimeishiwa nguvu maana sikutegemea kama ndo yangekuwa hayo mara sasa ataondoka ataenda kukaa kwao duuh.

Kiukweli sikumjibu chochote nikaamua kutumia hekima tu maana yeye teali alishapanda kaamua kushuka nakumuacha nikakata simu yangu nikawaza sana huyu skuiz amekuaje kwamba ndo mimba inampeleka hivyo au nikaacha kama yalivyo lakin narud nyumbani njiani ninawaza sana yale maneno Nikafika home nikaingia ndani nikamkuta kakaa sebleni, sikumsemesha chochote nikapitiliza jikoni nikamkuta beki 3 anapika nikamuuliza kuwa dadaako kala akasema ndio alikula na saivi ndio napika chakula cha usiku nikasema powa nikapitiliza chumbani nikaingia bafuni nikaoga nikamaliza nikapanda kitandani nikapumzika.

Dakika 3 akaja chumbani kimya sikumsemesha kakaa nikamwambia jiandae kesho nakupa nauli yakuendea huko kwenu iliuepuke hayo manyanyaso unayosema.

Nikainuka nikavaa nikafungua mlango kabla sijatoka nikamwambia natoka napiga simu kwenu kesho wakupokee nikaondoka zangu now nipo somewhere nimetulia kwanza ila kweli nimewaza huyu kesho namsafirisha kweli sioutani acha aende kwanza kwao akatulie akikaribia kujifungua nitamfata wakuu kwasababu najitahdi sana anapopanda namimi nisipande maana minajijua nina hasira sana.
Umemkosea sana aisee
Muombe radhi😆😆😆
 
Ndo huyo huyo mkeo aliyeaga kwenda singida akalala Dodoma mara mbili mwaka jana?! Mbona ni kama una go through a lot na huyo mwanamama🙂
 
Back
Top Bottom