Nimegombana na Mke wangu leo mpaka nimeshangaa

Nimegombana na Mke wangu leo mpaka nimeshangaa

Mwambie asilalelale sana kupitiliza,jioni ukirudi toka nae atembee hata kidogo kama mazoezi,

Isije ikaleta shida
 
Nakumbuka mama kijacho wangu enzi hizo alinambia nirudi na sanamu la posta na alikua siriazi[emoji23][emoji23]
Nyie watu daaah[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama hakuwa na tabia hio kabla ya ujauzito kuwa mpole Acha hasira,
Cheza na mudi yake weka uanaume pembeni, Ili asimstress mtoto tumboni. Mvumilie akishusha kama sio tabia yake ataacha tu
 
1. Una umri gani mkuu?
2. Hii ni mimba ya kwanza?
3. Uliwahi kusikia habari za wajawazito?
4. Ulikuwa na haraka gani ya kupiga simu na
Uongee maneno mengi kiasi hicho?.

Makosa ni ya kwako umebwabwaja sana kwa mjamzito.

Uliposwa uwe na subra, ufike home mnaongea kirafiki huku ukipapasa kitumbo chake taratiiibu.
Feminist
 
Ushauri huu natoa bure sitaki hata mia yako. Rudi home, tulia, muombe msamaha kabisa!

Kesho wahi kutoka job, Rudi home mchukue nendeni Dukani, mpitishe kwenye ice cream ama pahala penye miti mingi, ama maji, aone ukuu wa Mungu na ajue mimba siyo ugonjwa.

Mkeo ana upweke sana ni vile hujajua tu, suala la ww kwenda job kurudi siyo issue kwa kipindi hiki

Kesho kutwa yake mpeleke akafanyiwe massage nzuri kabisa, atengeneze kucha, nywele ukiwepo, nasisitiza ukiwepo!

taratibu kabisa utashangaa na roho yako, utarudi kushukuru.

Umpeleke kwao ndo wamemtia mimba? em tuliza akili mwanaume
Feminist hii usiisikilize
 
Weacha tu mkuu sababu kuna dada nafanya nae kazi ofisi moja yule dada alikuwa mjamzito yule dada alikuwa anakuja kazini mbaka anajifungua ndo wakampa likizo ya uzazi lakin alikuwa na uwezo wa kuomba likizo before hata ya kujifungua akajifungulie hata kwao lakini wapi mbakatulikuwa tunamuonea huruma kazi nyingine za kiofisi tunamsaidia katoka kujifungua January mtoto wa kiume

Tabia ya kulinganisha watu itakupa tabu sana. Mkeo ni mkeo na huyo wa kazini ni wa huko. Tafuta namna ya kuongea na mkeo mrekebishane acha kulinganisha na watu wa nje.Mkeo akianza kukulinganisha na wanaume wengine wee utamuelewa? Acha hizo basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwa makini na ushauri unaopokea unaangukia pua Sasa hivi[emoji1787],anaekupa ushauri unakuta yupo kwake muda huu anapapasa kijacho wake,au ameamshwa saa nane usiku akatafute tikiti na ameenda,..mjitahidi sana kusoma majarida yanayohusu uzazi na ujauzito.hata wanaume yanatusaidia sana kuishi na wake zetu na kuwasaidia kwenye hii safari..maamuzi yako mabovu yanaweza muathiri mtoto pia

Hayaa mkuu
 
Kama hakuwa na tabia hio kabla ya ujauzito kuwa mpole Acha hasira,
Cheza na mudi yake weka uanaume pembeni, Ili asimstress mtoto tumboni. Mvumilie akishusha kama sio tabia yake ataacha tu

Sawa mkuu nimekuelewa
 
Sawa mkuu nimekuelewa
Jifanye fala kwa mda akubadilishie jina.
Mideko mingi sana kipindi hiki.
Wajawazito huwa na kichaa cha mda sababu ya formation ya process inayoendelea tumboni mwao
 
Nakumbukaga wangu alinitamkia "ww msenge" neno ambalo sijawahi tamkiwa na mtu yyte yule maishani mwangu, nilikasirika sana ila kwakuwa alikuwa amebeba mimba ya binti yangu mrembo wa kwanza niliamua kunyamaza tu maana kama ninge react basi bila shaka ningemtoa mimba pale pale ndani bila Miso Wala MVA.

Ujauzito una karaha zake issue ya kumpeleka kwao imekaa vizur .
 
Mimba chini ya miezi 3 inahitaji umakini, akipata stress inatoka hyo mzee baba.
 
Habar wana JF,

Nashukuru mungu wote ni wazima
Mtanisamehe mimi sio muandishi mzuri sana wakuu.

Nimetoka kugombana na wife mpaka nimebaki nashangaa na kuwaza kwa maneno alioyasema wife, nikwamba wife ni mjamzito wa miezi 4 sasa anatimiza ikifika tarehe 13 sasa leo nimetoka kazini nikawa nimekaa kwenye gari nawaza sana kutokana na maisha na life style anayoishi wife sio kabsa kiupande mwingine.

Kutokana na maisha yalivyo toka wife amebeba mimba anaishi life style ambayo kwa upande mwingine bado haijanivutia lakin ni kawaida sana yeye ni 24hrs/7days yupo ndani amelala akichoka anafungua insta atashinda mitandaoni akichoka sebleni kuangalia TV tamthilia zake mwenyewe.

Ni vizuri kupata muda wa kupumzika kwa hali yake lakini mimba sio mzigo au mimba sio ugonjwa ukufanye ushinde ndani 24hrs. Nikampigia sim kumjulia hali kashindaje leo then nikamuuliza unafanya nini akajibu yupo kitandani amelala.

Nikamwambia kiupole sana na kiutaarabu kuwa mkewangu em bas uwe unatoka na kuchakarika kuna duka la biashara now yupo kijana uwe hata unakwenda basi kuangalia mambo yanaendaje sio hadi mimi nitoke kazini nimechoka nipitie tena huko wakati wewe upo tu nyumbani umetulia vituvingine ni kuichangamsha akili na kupambana kuliko kushinda tu ndani mamaangu wewe sio mgonjwa.

Kusema kwamba huwez kutembea mbona kuna wanawake wana mimba lakini wanachakalika wengine unakutana nao anatumbo kubwa kabeba beseni lake la mboga anatembeza mitaani wengine wanakimbiza maofisi na matumbo yao tena makubwa lakin wanachakalika asubuh na mapema kashafika ofisi nikamwambia hayo siyo maisha uyaotaka kuishi.

Sijajua nihilo tu au kuna mengine ila Alivimba na kuanza kuongea kwa hasira na kuongea maneno mengi sana ambayo sikutegemea na kusema kuwa namnyanyasa mara kisa kubeba mimba naanza kumuona mjinga so nisimfananishe na hao wajinga ye anaakili zake na anajua anachofanya, mara nimeanza kumuona mzigo kwangu kwakuwa kabeba mimba duuh wakuu nilibaki nimeishiwa nguvu maana sikutegemea kama ndo yangekuwa hayo mara sasa ataondoka ataenda kukaa kwao duuh.

Kiukweli sikumjibu chochote nikaamua kutumia hekima tu maana yeye teali alishapanda kaamua kushuka nakumuacha nikakata simu yangu nikawaza sana huyu skuiz amekuaje kwamba ndo mimba inampeleka hivyo au nikaacha kama yalivyo lakin narud nyumbani njiani ninawaza sana yale maneno Nikafika home nikaingia ndani nikamkuta kakaa sebleni, sikumsemesha chochote nikapitiliza jikoni nikamkuta beki 3 anapika nikamuuliza kuwa dadaako kala akasema ndio alikula na saivi ndio napika chakula cha usiku nikasema powa nikapitiliza chumbani nikaingia bafuni nikaoga nikamaliza nikapanda kitandani nikapumzika.

Dakika 3 akaja chumbani kimya sikumsemesha kakaa nikamwambia jiandae kesho nakupa nauli yakuendea huko kwenu iliuepuke hayo manyanyaso unayosema.

Nikainuka nikavaa nikafungua mlango kabla sijatoka nikamwambia natoka napiga simu kwenu kesho wakupokee nikaondoka zangu now nipo somewhere nimetulia kwanza ila kweli nimewaza huyu kesho namsafirisha kweli sioutani acha aende kwanza kwao akatulie akikaribia kujifungua nitamfata wakuu kwasababu najitahdi sana anapopanda namimi nisipande maana minajijua nina hasira sana
Kama umejitahidi kuongea naye vizuri ikashindikana, mpeleke kwao.
Muda mwingine mnahitaji umbali ili mambo yakae vizuri.
 
Mkuu ukitaka kufa kabsa funga nae ndoa , kaa nae bila ndoa mkuu umsikilize mpka ajifungue ,pia usisite kupima dna kudhibitisha mtoto kama ni wako
 
Ila mimba za siku hizi zimegeuka fimbo kwa wanaume jamani,
Mengine ni makusudi hamna mtu hasumbuliwi na mimba ila kuna mda inabidi ujikaze
 
Back
Top Bottom