labda madaktari waje watuambie, uliugua moto miaka 14 iliyopita, umekuja kuungua sasaivi tena, hapo utakuwa nao kweli? ungekuwa umesavaivu hadi leo kama unao? manake hadi unaugua moto ina maana kinga zimepungua mwilini fourteen years ago, ungeshakufa mzee. hapo nenda tu kapime na unaweza usikutwe nao.
Pili, hata kama ukikutwanao, sio mwisho wa kuishi, na hata ukifa, shukuru Mungu atakuwa amekupatia nafsi ya kutengeneza mambo yako na Mungu. Kufa kunauma kibinadamu ila kiroho kufa ni kuzuri kama unakufa mikononi mwa Mungu, though ni hatari na hasara ukifa nje ya mikono ya Mungu, maana yake, Mungu amekuachia opportunity hii badala ya kuhangaika kwenye google, unatakiwa kuhangaika kuokoka, tubu dhambi zako kabidhi maisha yako kwa Yesu ili kama ukiishi uishi mikononi mwake na kama ukifa ufe mikononi mwake. wapo waliokufa gafla hata nafasi ya kutubu hawakupata na wameenda moja kwa moja motoni, usiwe mmojawapo. usichezee opportunity hiyo uliopewa ya kutengeneza mambo yako na Mungu. wengi wanakebehi, wanang'ang'ania dini badala ya wokovu, wanategemea wakifa waombewe na padre ili wasamehewe dhambi, Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu, kuan nyakati mwanadamu ukikamatikaaa kwenye kona ukanona hamna namna hapa unakufa, solution inatakiwa kuwa KUTENGENEZA NA MUNGU ili huko unakoenda uende kuzuri. zingatia sana hili.
Ufunuo 14:13 inasema, Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, andika, heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao, kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
hapo mwishoni anasema, "matendo yao yafuatana nao", manake, yale uliyoyatenda duniani ndiyo yatakayokuchagulia wapi uende ukifa, motoni au uzimani. na kama matendo yako yatafuatana nawe, manake ukifa hata padre aombe usamehewe dhambi ukiwa maiti anajisumbua tu, wewe umeondoka na matendo yako, utaenda kuhukumiwa kwa yale uliyoyatenda. kama ulitenda maovu, haukutubu kabla ya kufa, utaenda nayo. wengi wanadharau njia ya wokovu, hawajui kwamba hio ndio njia ya kuwasaidia maisha ya baadaye. dini zimewakaa,wameendelea kuabudu maria, kuabudu wafu, na masanamu, wameacha njia ya wokovu ile ambayo mitume walikua nayo kitabu cha Matendo. katoliki kwa mfano wamefungia watu nira sana kwasababu wanaamini ukifa watakuombea utasamehewa huko uendako, kumbe hakuna kitu kama icho, wanaomba kwa maria, wanaomba kwa wafu, hata humu kuna watu hawatafurahi hiki nilichoandika kwasababu wanaipenda dini yao kuliko ukweli wa Neno la Mungu. cha muhimu mmesikia, na nimenawa mikono.