Nimegundua Bahati Ina mchango mkubwa kwenye Maisha yetu

coockie monster

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
373
Reaction score
724
Hili swala nilikuwa nalijua ila leo baada ya message fulani hivi kutumiwa na kijana mdogo ambaye nilizoeana naye ambapo alikuwa mfanya usafi ofisini, baadae alipata kazi sehemu nyengine ila kwa wakati kadhaa alikuwa ananipigia simu na kunipiga vizinga.

Sababu nilikuwa najua hali yake, nikawa nampa tafu ila sometimes huwa namzingua kuhusu tabia yake. Ila leo nilivomchallenge kuhusu tabia yake ya kuomba omba alinipa jibu deep na la kutafakari sana.


Alivhoniambia anapambana na Hana Bahati nilitamani kulia sababu ni kweli anapambana sana. Kuna wenzake kama yeye ila atleast wanajitahidi ila yeye pekee ndio analia njaa. Usijione mjanja jua kuwa una Bahati.
 
Ngoja nirejee maandiko yasemavyo kuhusiana na hili

MHUBIRI 9:11

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
 
Tukiachana na kuomba omba Kusema kweli naungana na Mustapha maisha ni bahati mpaka kwenye bible imeandikwa, jambo lolote likifanikiwa huonekana mfanyaji alitumia sana akili! Kumbe wapo wanaofanya kwa namna ile kama huyo aliofanikiwa ila hawajabahatika ndo tunasema hawana akili/hawajitumi nk
Wazungu wanasema "

History Is Written by the Victors​

Haijalishi umepambana au hujapambana kikubwa ushindi na ushindi ndo bahati.
 
Hakuna kitu kinaitwa bahati! Apandacho mtu ndicho avunacho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…