Mkuu,
Bila mimi kudogosha sehemu ya jitihada binafsi za kila mtu, ambayo nayo ni kubwa tu, ukweli ni kwamba, watu wengi wanaidogosha sana sehemu ya bahati.
Huchagui utazaliwa wapi, huchagui utazaliwa na wazazi gani, huchagui utarithi genes zipi, na hata mambo unayochagua, kama kukutana na nani, wapi, huna control nayo.
Fikiria hivi, nchi unayozaliwa tu ina mchango mkubwa sana wa ku dictate maisha yako yataendaje.
Na hilo huchagui.
Wazazi wanaokuzaa tu wana mchango mkubwa sana wa kunshape maisha yako yatakavyokwenda.
Na huchagui wazazi.
Hata yule Nyerere unaweza kumuona kichwa, lakini kulikuwa na vichwa zaidi yake tatizo hawajazaliwa famikia za kichifu tu, na kwa sababu hiyo, walikosa nafasi ya kusoma, Nyerere akaipata.
Yani asingekuwa na bahati ya kuzaliwa familia ya Chifu, asingesoma na historia ingekuwa tofauti sana.
Ila, kitu muhimu ni kuishi kwa kujiandaa vilivyo, when preparation meets opportunity, good luck happens.