Nimegundua Bahati Ina mchango mkubwa kwenye Maisha yetu

Nimegundua Bahati Ina mchango mkubwa kwenye Maisha yetu

ukijua kufungua code hii ndio umefungua hayo mabahati na nyota yako
1703915003551.jpg
 
Hizi mambo zina ukweli. Kuna jamaa kila nikimuona naumia sana. Mbunifu, ana akili sana na sio mchoyo wa maarifa. Cha ajabu kilekile anachofanya yeye hafanikiwi naona anapiga tu mark time na maisha, ila kwa mbinu hizohizo akiwapa wengine wanatoboa. Inatafakarisha!
Namna ya kupima mafanikio hapo ndo changamoto, discipline yetu kwenye pesa nikipengele....
 
Asilimia 100 ya makocha wote kwenye michezo duniani inapotokea kuwa wamepoteza mechi ilhali walikuwa wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao jibu huwa ni moja tu... " hatukuwa na bahati siku ya leo".

Hivyo katika maisha pamoja na jitihada tunatakiwa kuwa na bahati.
NA wahenga walisema heri ukose mali kuliko kukosa bahati. Wengine wakasema jitihada hazishindi kudra.
 
Hili swala nilikua nalijua ila Leo baada ya message flani hivi kutumiwa na kijana mdogo ambae nilizoeana nae ambapo alikua mfanya usafi ofisini,Baadae alipata kazi sehemu nyengine ila Kwa wakati kadhaa alikua ananipigia simu na kunipiga vizinga sababu nilikua najua hali yake(ni Malawian) nikawa Nampa tafu ila sometimes hua Namzingua kuhusu tabia yake. Ila Leo nilivomchallenge kuhusu tabia yake ya kuomba omba alinipa jibu deep na la kutafakari sana. View attachment 3035866

Alivoniambia anapambana na Hana Bahati nilitamani kulia sababu ni kweli anapambana sana,Kuna wenzake kama yeye ila atleast wanajitahidi ila yeye pekee ndio analia njaa. Usijione mjanja jua kua una Bahati.
Kila mtu Ana mda wake
 
Asilimia 100 ya makocha wote kwenye michezo duniani inapotokea kuwa wamepoteza mechi ilhali walikuwa wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao jibu huwa ni moja tu... " hatukuwa na bahati siku ya leo".

Hivyo katika maisha pamoja na jitihada tunatakiwa kuwa na bahati.
NA wahenga walisema heri ukose mali kuliko kukosa bahati. Wengine wakasema jitihada hazishindi kudra.
Bahati ni jambo jema au baya linalokuja bila wewe kutarajia, ila ukichunguza vizuri kuna mlolongo wa matukio mengi mno yanajipanga ili uone hiyo ni bahati.
 
Ila ili hiyo kitu uonee ni bahati nyuma kuna malolongo wa mpangilio wa matukio sema unaona kama ni bahati tu lakini kuna mpangilio mkubwa wa matukio.

Maisha hayana formula mkuu ,hizo series za matukio ya nyuma wengi wamefanya na hawajatoboa.

Tuliambiwa soma ili ufanikiwe ila % kubwa waliofanikiwa hawana kisomo kikubwa ,sizungumzii utajiri wa kibongo nyumba na gari ndogo ,nazungumzia fortune(Kutoboa).

Hata hao waliosoma na kufanikiwa utajiri wao haukutokana na kisomo bali ni njia za panya walizotumia kujitajirisha ,wapo waliofanya ufisadi ,weezy,rushwa etc.

Ebu Pata picha Sativa ametupwa pembeni ya bwawa lenye mamba na viboko ,pori lenye mbwa mwitu na simba ,kisha akapigwa risasi lengo kufumua medula oblangata lakini ikapiga pembeni na akaziduka saa 9 usiku akaijikokota hadi barabara akaonwa na askari wa porini na akatoboa ,hizo ndizo tunazosema bahati ,hauwezi kufanya wewe kama wewe au series of event ili zijenge bahati.
 
Back
Top Bottom