Nimegundua Bahati Ina mchango mkubwa kwenye Maisha yetu

Nimegundua Bahati Ina mchango mkubwa kwenye Maisha yetu

Katika universe hakuna bahati unachopanda utavuna hicho .

Mfano MTU anayetoa kwa nia njema pasipo kusubiri malipo huwa hapungukiwi .bali hupata zaidi.
 
Maisha ni mchezo wa bahati ambamo ni lazima kujasiri .

Jasiri haachi asili . Ijue asili yako ya kiroho , tayari utakuwa umeshinda mchezo wa bahati .
 
Hili swala nilikuwa nalijua ila leo baada ya message fulani hivi kutumiwa na kijana mdogo ambaye nilizoeana naye ambapo alikuwa mfanya usafi ofisini, baadae alipata kazi sehemu nyengine ila kwa wakati kadhaa alikuwa ananipigia simu na kunipiga vizinga.

Sababu nilikuwa najua hali yake, nikawa nampa tafu ila sometimes huwa namzingua kuhusu tabia yake. Ila leo nilivomchallenge kuhusu tabia yake ya kuomba omba alinipa jibu deep na la kutafakari sana.


Alivhoniambia anapambana na Hana Bahati nilitamani kulia sababu ni kweli anapambana sana. Kuna wenzake kama yeye ila atleast wanajitahidi ila yeye pekee ndio analia njaa. Usijione mjanja jua kuwa una Bahati.
Naomba umtumie huyo kijana pesa kama hujafanya hivyo.
 
Ngoja nirejee maandiko yasemavyo kuhusiana na hili

MHUBIRI 9:11

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Nausibili huu wakati na unifikie Aamin
 
hard work will put you in a place where good luck will find you.

Tusiache wala kuchoka kujibidiisha, kitu chochote ukikifanya kwa moyo wako wote na kujitoa lazima upate matokeo chanya. Kikubwa ni kutoa sadaka na kuwa na imani.
 
Wewe django unakataliwa hadi na mama ntilie 😂😂🙆‍♂️, wewe huu uzi unakuhusu
Nina balaa mkuu shida udomo zege pro max sijui nifanyeje kama sio hivyo ungekuta nishakula mtu na dadaake na mishangazi yote ya hapa mtaani udomo zege ni shida sana usikie tu kwa mtu usiombe ukutokeee
 
Kumechanganyika vitu vingi mno humo ndani kuita sio bahati na bahati, mwingine anasema hana bahati kumbe kuna watu wanatumia vibuyu au shida nyingine
 
Asilimia 100 ya makocha wote kwenye michezo duniani inapotokea kuwa wamepoteza mechi ilhali walikuwa wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao jibu huwa ni moja tu... " hatukuwa na bahati siku ya leo".

Hivyo katika maisha pamoja na jitihada tunatakiwa kuwa na bahati.
NA wahenga walisema heri ukose mali kuliko kukosa bahati. Wengine wakasema jitihada hazishindi kudra.
Albert ..... Namnukuu Eduardo La Volpe au La Volpiana moja ya Mtu anaeabudiwa na Guardiola kuwa ni matumzi ya Muda na nafasi Kama sio historia na presha (Intelijensia n saikolojia ) ndiyo huamua mchezo.
Hivyo nafasi inasimama mbadala was bahati.
 
Mungu anatoa riziki
Hutoa riziki kwa wakati autakaye yeye
Huyo Mungu anatoa riziki gani?

Unathibitishaje riziki uliyonayo amekupa Mungu?
Mungu ana rehema mbili hapa duniani humgawia anaye mtii na asiye mtii hapa duniani
Wapi wewe huyo Mungu alikugawia riziki?

Au ulipambana mwenyewe na kuhenyeka halafu unakuja hapa kutoa credit kwa Mungu ambaye hata hujui ni nini..!!
Swala la kusema mtu yule ana bahati au mtu huyu Hana ni Ukosefu Wa subra
Tujikite kwenye kusubiri
Watu wangapi wamesubiri kupata hiyo bahati na wametoka kapa?

Hakuna uhusiano wa Subra au kusubiri na kupata Bahati.

Bahati huja anytime.

Na hakuna uhusiano wowote ule wa bahati na Mungu.
Hakika mwenye kusubiri yupo karibu na mungu!
coockie monster
 
Back
Top Bottom