Nimegundua Bahati Ina mchango mkubwa kwenye Maisha yetu

Nimegundua Bahati Ina mchango mkubwa kwenye Maisha yetu

Bahati ni jambo jema au baya linalokuja bila wewe kutarajia, ila ukichunguza vizuri kuna mlolongo wa matukio mengi mno yanajipanga ili uone hiyo ni bahati.
Na hayo matukio hufuatana na jitihada,lakini pia bahati tukiiweka wa ubaya( bahati mbaya) tunakosea. Lolote kinalokuja kwa ubaya tuite mkosi si bahati mbaya. Bahati ni ile chanya inayokuja kwa matokeo mazuri.

Kinyume :
Bahati- Mkosi
 
Maisha hayana formula mkuu ,hizo series za matukio ya nyuma wengi wamefanya na hawajatoboa.

Tuliambiwa soma ili ufanikiwe ila % kubwa waliofanikiwa hawana kisomo kikubwa ,sizungumzii utajiri wa kibongo nyumba na gari ndogo ,nazungumzia fortune(Kutoboa).

Hata hao waliosoma na kufanikiwa utajiri wao haukutokana na kisomo bali ni njia za panya walizotumia kujitajirisha ,wapo waliofanya ufisadi ,weezy,rushwa etc.

Ebu Pata picha Sativa ametupwa pembeni ya bwawa lenye mamba na viboko ,pori lenye mbwa mwitu na simba ,kisha akapigwa risasi lengo kufumua medula oblangata lakini ikapiga pembeni na akaziduka saa 9 usiku akaijikokota hadi barabara akaonwa na askari wa porini na akatoboa ,hizo ndizo tunazosema bahati ,hauwezi kufanya wewe kama wewe au series of event ili zijenge bahati.
Ni bahati kwa sababu haukutarajia imekua hivyo akilini, ila kuna mapangilio mkubwa wa matukio mpaka sativa akapona , yani hata ukaokota burungutu la pesa itakua ni bahati kwako kwa sababu hukutarajia ila kulikua na mpangilio mkubwa wa matukio huko nyuma mpka ukaokota pesa.
 
Na hayo matukio hufuatana na jitihada,lakini pia bahati tukiiweka wa ubaya( bahati mbaya) tunakosea. Lolote kinalokuja kwa ubaya tuite mkosi si bahati mbaya. Bahati ni ile chanya inayokuja kwa matokeo mazuri.

Kinyume :
Bahati- Mkosi
Mkuu bahati ni kitu chochote kiwe kizuri au kibaya kinachokuja bila wewe kutarajia ,kikiwa ni kizuri unaita bahati nzuri kikiwa kibaya unaita bahati mbaya.
 
Juna dogo tukupiga naye o level akapiga buyu.... 0 sasa baada ya kupambana...akaruka zake Holland ndio akaupiga mwingi....japo maisha hayana kanuni nazidi kumuombea...ana maisha kuliko mimi niliyepiga div one.

Najua chochote kinaweza kikatokea
 
Ni bahati kwa sababu haukutarajia imekua hivyo akilini, ila kuna mapangilio mkubwa wa matukio mpaka sativa akapona , yani hata ukaokota burungutu la pesa itakua ni bahati kwako kwa sababu hukutarajia ila kulikua na mpangilio mkubwa wa matukio huko nyuma mpka ukaokota pesa.
Kwanini wengine waliopita kwenye hiyo barabara hawakuona burungutu? Why burungutu uokote wewe? Hizo ndizo tunazosema BAHATI.
 
Riziki ni kila neema ambayo mwanadamu anaipata kutoka kwa Mungu wake/wetu. Pumzi, afya, kipato, watoto, kipaji, n.k
Mkuu ni matokeo ya fikra , zamani Africa tulikua tunachezea almasi bao ,wazungu wakaja na fikra tofauti kuhusu almasi wakafanikiwa na almasi ikawa kitu cha dhamani na wakatajirika .

Maisha wakati mwingine hutofautiana kutokana na tofauti za kifikra.
 
Mkuu bahati ni kitu chochote kiwe kizuri au kibaya kinachokuja bila wewe kutarajia ,kikiwa ni kizuri unaita bahati nzuri kikiwa kibaya unaita bahati mbaya.
Hapana ni mazoea tu lakini si sahihi, ukisema bahati tu ujue ni matokeo chanya yasiyotarajiwa yale mazuri.

Matokeo mabaya ni mkosi.
 
Mkuu ni matokeo ya fikra , zamani Africa tulikua tunachezea almasi bao ,wazungu wakaja na fikra tofauti kuhusu almasi wakafanikiwa na almasi ikawa kitu cha dhamani na wakatajirika .

Maisha wakati mwingine hutofautiana kutokana na tofauti za kifikra.
Almasi na mali zote za ardhini sio za mwanadamu, tumezikuta na tutaziacha
 
Kwanini wengine waliopita kwenye hiyo barabara hawakuona burungutu? Why burungutu uokote wewe? Hizo ndizo tunazosema BAHATI.
Inawezekana waliopita walikua na mawazo , au walipita bila kuangalia chini na wewe ukapita kwa sababu nyingne iliyokupitisha pale ukaangalia chini ukaokota na Inawezekana hao wengine hawakupita kabisa wewe ndio ukapita kwa sababu nyingne kabisa ukaokota na aliye dondosha hilo burungutu ikawa ni sababu ya wewe kuota ,hakuna kitu kinatokea bila mpangilio wa matukio kwanza .

Wewe akili yako inakuambia ni bahati ile kiuhalisia kuna mpangilio mkubwa wa matukio .
 
Back
Top Bottom