Nimegundua Bahati Ina mchango mkubwa kwenye Maisha yetu

Bahati lazima uipambanie haiwezi kuja kirahisi inabidi mtu awe anajituma kwenye kila kitu mfano hapa mtaani kuna jamaa hapa mtaani kwetu yeye humwambii kitu kwenye kubeti na mwezi wa nne mwaka huu alishinda million 60+ saivi ashakuwa mtu mwingine kabisa.Kwahiyo inabidi kupambana wakati mwingine ndo bahati ije.
 
Hakuna kitu kinaitwa bahati! Apandacho mtu ndicho avunacho!
Mnamaliza wote shule, wote mmefaulu vizuri, halafu mwenzio siku moja anakutana na mtu kwenye daladala wanaketi pamoja na kubadilishana mawazo, kupitia huyo mtu anapata kazi nzuri na anaacha kupanda daladala wewe upo tu unapanda daladala kila siku unaishia kuambiwa nyanyua miguu niingize mzigo hukutani na connection. Huyu aliyepata connection kwenye daladala amepanda nini cha tofauti kama si bahati tu?
 
Mkuu,

Bila mimi kudogosha sehemu ya jitihada binafsi za kila mtu, ambayo nayo ni kubwa tu, ukweli ni kwamba, watu wengi wanaidogosha sana sehemu ya bahati.

Huchagui utazaliwa wapi, huchagui utazaliwa na wazazi gani, huchagui utarithi genes zipi, na hata mambo unayochagua, kama kukutana na nani, wapi, huna control nayo.

Fikiria hivi, nchi unayozaliwa tu ina mchango mkubwa sana wa ku dictate maisha yako yataendaje.

Na hilo huchagui.

Wazazi wanaokuzaa tu wana mchango mkubwa sana wa kunshape maisha yako yatakavyokwenda.

Na huchagui wazazi.

Hata yule Nyerere unaweza kumuona kichwa, lakini kulikuwa na vichwa zaidi yake tatizo hawajazaliwa famikia za kichifu tu, na kwa sababu hiyo, walikosa nafasi ya kusoma, Nyerere akaipata.

Yani asingekuwa na bahati ya kuzaliwa familia ya Chifu, asingesoma na historia ingekuwa tofauti sana.

Ila, kitu muhimu ni kuishi kwa kujiandaa vilivyo, when preparation meets opportunity, good luck happens.
 
😍 noted kaka
 
Naam!
 
Hakuna anae panga maisha , kila kitu kinachokoea kwenye maisha ya mtu kimetokea kwa matokeo ya mpangilio wa matukio ya nyuma ya kistoria ambayo ni kama bahati tu .
Matukio ya nyuma yalisha pita, matukio yajayo hayajulikani, wote tuliopata nafasi ya kuwepo hapa duniani ni kwa sababu maalum wala sio bahati mbaya
 
[emoji16][emoji16]
 
Uko sahihi kbsa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…