Ulitaka mkulima kila mwaka awe wa kulia machozi tu? Ulitaka wakulima kila mwaka wauze kwa Bei ya hasara ili wewe ufurahi? Ulitaka kuona kila mwaka wakulima Ni wakuteseka na kuvuja jasho huku nyinyi mkilia kimvulini, Nenda na wewe ukalimee ujuwe uchungu wake, Nenda ukalime uje uuze hiyo Bei ndogo unayoitaka, Nenda ukalime ujuwe adha ya kilimo, nenda ukalime ujuwe mkulima anahangaika vipi juani na kwenye mvua, nenda na wewe ukalimee ujuwe ugumu wake,
Msitake kuwafanya wakulima wa nchi hii kuwa daraja lenu ninyi wanyonyaji wakubwa, Tunamshukuru Sana mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kutujali sisi wakulima wanyonge, Sasa tunaona faida ya kilimo chetu, Sasa tunafaidi jasho letu
Mh Bashe songa mbele fanya kazi uliyooaminiwa na mh Rais wetu mpendwa, Msaidie kwa nguvu zako zote, usimuuangushe Rais wetu tunayempenda kwa dhati ya mioyo yetu, Fanya kazi chapa kazi Leta matumaini kwa watanzania Kama ambavyo mh Rais wetu ameongoza njia hiyo