Uchaguzi 2020 Nimegundua hizi kampeni zinafanyika kwa upendeleo “hazina usawa”

Uchaguzi 2020 Nimegundua hizi kampeni zinafanyika kwa upendeleo “hazina usawa”

Katika kampeni zinazoendelea, nimeona zinakibeba chama cha mapinduzi kwa sehemu kubwa, kwani viongozi wanaogombea bado wanako madarakani na wamekuwa wakiendelea kutoa maagizo kwa mamlaka zilizo chini yao,

Mfano: Unakuta mgombea urais anatoa maagizo ya kujenga barabara na pia kutoa pesa hadharani kama zawadi, Makamu wake akiagiza halmashauri kuongeza pesa za mikopo kwa vikundi mbalimbali, huku Waziri mkuu akiagiza kurejeshwa kwa baadhi ya mashamba huko Singida.

Hivi hao wapinzani wakitoa misaada wakati huu wa kampeni si watachukuliwa wanatoa rushwa?

Natamani katiba ibadilike tu, kikifika kipindi cha kampeni kila aliyekuwa na madaraka avuliwe ili waingie uwanjani wakiwa katika kiwango kimoja tofauti na sasa.

Tatizo la katiba ambalo aidha liliwekwa makusudi au kwa kupitiwa.
 
Mkuu wewe kuwa mataga siyo dhambi na wala usijisikie vibaya, pia wapi nimesema kuwa nimesoma shule za international?
Waziri mkuu au Makamu wa Rais anapomsindikiza JPM kwenye kampeni na kuanza kutoka maelekezo ya kiserikali, hapo wanakuwa wamesimama kama akina nani?
Upande wa upinzani, umewahi kusikia wakitoa maelekezo yoyote ya kiserikali?
Then ukiambiwa wewe ni mataga unabisha na kunigeuzia mimi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
ndugu Mataga bana. Umeshasema Waziri Mkuu na umeshasema Makamu wa Rais halafu unauliza tena anakuwa amesimama kama nani..
Mamlaka ya Prime Minister siku hizi yanaishia jimboni kwake tu ??
Na pia anaweza kwenda Wilaya Yoyote ile kama Mwanachama na kusaidia kunadi Sera za Chama Chake anachokiwakilisha.
Na hata akitoa tamko la kiserikali acha atoe. Vyote vyeo vyake.
Ndugu Mataga vipi bana.
Cha muhimu ni tusiishie vijiweni (online) tu humu basi, tuhakikishe Tarehe ya Uchaguzi ikifika twende tukapige Kura.
Chagua ambaye kwako utaona anafaa. That's it!!
 
Nimepanda mwendokasi hapa redio wameweka kampeni za mheshimiwa kigoma.
Ni baada ya kukaa kituoni Moroko zaidi ya nusu saa kuisubiria
 
Katika kampeni zinazoendelea, nimeona zinakibeba chama cha mapinduzi kwa sehemu kubwa, kwani viongozi wanaogombea bado wanako madarakani na wamekuwa wakiendelea kutoa maagizo kwa mamlaka zilizo chini yao,

Mfano: Unakuta mgombea urais anatoa maagizo ya kujenga barabara na pia kutoa pesa hadharani kama zawadi, Makamu wake akiagiza halmashauri kuongeza pesa za mikopo kwa vikundi mbalimbali, huku Waziri mkuu akiagiza kurejeshwa kwa baadhi ya mashamba huko Singida.

Hivi hao wapinzani wakitoa misaada wakati huu wa kampeni si watachukuliwa wanatoa rushwa?

Natamani katiba ibadilike tu, kikifika kipindi cha kampeni kila aliyekuwa na madaraka avuliwe ili waingie uwanjani wakiwa katika kiwango kimoja tofauti na sasa.
Kipindi cha uchaguzi hakiwaondoi walio kwenye madaraka au walio kazini kuacha kazi zao na majukumu yao. Wanaendelea na kazi na majukumu yao hadi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi atakapotangaza mshindi kwenye ushindani huu. Hivyo hao kufanaya wafanyayo ni sahihi kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kutimiza majukumu SIYO KUTOA RUSHWA!

Halafu, ni kweli kabisa hakuwezi kuwa na usawa ikiwa wengine wameingia kwenye kinyang'anyiro hiki wakitegemea pesa za ughaibuni ambazo hazijaja na hata waliozifuata hawakupewa kwani hawawezi kuingiza pesa chafu nchini; kwa hiyo wako mufilisi tofauti na wenye pesa zao safi. Kampeni siyo lelemama ni kazi ngumu yenye kuhitaji pesa na moyo.
 
Nimepanda mwendokasi hapa redio wameweka kampeni za mheshimiwa kigoma.
Ni baada ya kukaa kituoni Moroko zaidi ya nusu saa kuisubiria
Hayo ndiyo mambo ya maendelo, zamani tulikuwa tukisubiri daladala SAA 3! Leo unasubiri nusu saa tu bado unalalama, vipi ndugu yangu?
 
ndugu Mataga bana. Umeshasema Waziri Mkuu na umeshasema Makamu wa Rais halafu unauliza tena anakuwa amesimama kama nani..
Mamlaka ya Prime Minister siku hizi yanaishia jimboni kwake tu ??
Na pia anaweza kwenda Wilaya Yoyote ile kama Mwanachama na kusaidia kunadi Sera za Chama Chake anachokiwakilisha.
Na hata akitoa tamko la kiserikali acha atoe. Vyote vyeo vyake.
Ndugu Mataga vipi bana.
Cha muhimu ni tusiishie vijiweni (online) tu humu basi, tuhakikishe Tarehe ya Uchaguzi ikifika twende tukapige Kura.
Chagua ambaye kwako utaona anafaa. That's it!!
Mkuu kwa nini waniita mimi Mataga?
Anyway kifupi wakiwa kwenye jukwaa la kampeni hawatakiwi kutoa maelekezo ya kiserikali. Ni vizuri kama tukiishia hapa, naunga mkono hoja ya tarehe ikifika tukapige kura. Hivi jamaa wewe kweli ni Mataga au unazuga tu?
 
Miaka 59 ya UHURU tuna vyote hivi;

Mount Kilimanjaro

Serengeti National Park

Mikumi

Ziwa Victoria, Tanganyika

Makaa ya mawe Songea

Bandari ya DSM

Gesi ya Mtwara

Almasi

Tanzanite

Dhahabu

Bado CCM imeshindwa kumpa mwananchi MAJI ya kunywa safi na salama tu
 
Tatizo lililopo ni kuwa ni kazi ngumu sana kumwondoa kiongozi mbaya kutoka kwenye mamlaka au hata kukionfoa chama kibaya kama CCM kutoka kwenye uongozi wa nchi.

Ni rahisi sana kumwondoa kwenye madarka kiongozi mzuri, na mara nyingi akilalamikiwa, huweza hata kujiondoa nwenyewe lakini siyo kiongozi mbaya.

Viongozi wabaya, na vyama vya kifikteta kama CCM huondolewa kwa sululu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafikiri udikteta wa viongozi wa CCM haujawa critical.Bado ni udikteta uchwara ukifikia critical wananchi hawana budi bali kuandamana mpaka kieleweke.Sasa hivi Hali sio mbaya sana hakuna vikwazo!
 
Serikali ya awamu hii ndoyo imekithiri! Afadhari Kikwete alipoanza kampeni alikaimisha mtu lakin hawa wa sasa wamejibeba wazimwazima na mivyeo yao hata fedha sidhani kama wanato mifukoni mwao ni lazima serikali ndio inaumia! Yaani hadi manaibu waziri hadi leo bado wanatoaga maagizo na matamko ya kutenga fedha ili tu wawashawishi wananchi kuwapigia kura! Vitendo hivi vyote shida yake ni katiba, apite Lissu au Magufuli lazima tudai katiba mpya! Mambo ya kuanza kusema suala la katiba sio kipaumbele hatutakubaliana tena. Maana wanaobisha kuandikwa katiba mpya kumbe wanayategemea madhaifu yake yawavushe mbele! Tunataka katiba mpya ambayo pamoja na mambo mengine itapiga marufuku mambo yafuatayo:-

1 .Marufuku mgombea wa chama chochote kupita bila kupingwa, bora uchaguzi uhairishwe mpaka wapatikane washindani.

2. Marufuku kurudia uchaguzi kama mgombea amejiuzulu kwa sababu zozote zile labda kifo tu! Mgombea akijiuzulu iwe kwa hiari au kununuliwa, ateuliwe na kuapishwa yule aliyeshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi mkuu.

3. Marufuku kiongozi yeyote kusalia madarakani baada ya kupitishwa na chama chake kugombea urais, ubunge au udiwani. Vyeo vyote vya kiserikali vikome siku ile bunge linapovunjwa. Wizara zote zibakie chini ya makatibu wakuu na wakurugenzi, hawa wote wabakie chini ya katibu mkuu kiongozi.

4 .Marufuku rais, au mbunge, au diwani au chama kimoja cha siasa kutwala zaidi ya miaka 10 mfululizo, ikifika miaka 10 kiongozi au chama kama bado anataka kuongoza anakaa pembeni miaka 5 ndipo arudi tena.
5. Marufuku kwa kiongozi wa serikali kuwa na wadhifa mwingine mkubwa eg. Mwenyekiti au Katibu mkuu ndani ya chama cha siasa.
6. Pia ni marufuku kutumia rasilimali za serikali kwa shughuli za chama cha siasa.
 
Mhutu hawezi kukubali lkn atapigwa hivyo hivyo na mbeba maono wa twaifa hili Tundu Lissu
 
Akiwa kwenye JUKWAA LA KAMPENI,

SHERIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI ZINAMKATAZA KUTOA MAAGIZO YA KI - RAIS,

HATA MAKAMU WA RAIS HARUHUSIWI KUAGIZA ( KUAMURU) CHOCHOTE AKIWA KWENYE JUKWAA LA KAMPENI.

KUELEKEZA/KUAGIZA CHOCHOTE AKIWA KWENYE JUKWAA NI RUSHWA.

WAKITOKA KWENYE MAJUKWAA YA KAMPENI RUKSA KUAGIZA/KUELEKEZA CHOCHOTE.

WAZIRI MKUU NI MGOMBEA UBUNGE KULE RUANGWA,

SI MGOMBEA WA URAIS,

ANAPATA WAPI UHALALI WA KUZUNGUKA NCHI NZIMA AKIOMBA KURA KWA AJILI YA MGOMBEA WA URAIS?

ASUBIRI MGOMBEA WA URAIS AKIWA KWENYE JIMBO ANALOGOMBEA AMUOMBEE KURA HUKO RUANGWA.

AU

AFUATANE NA MGOMBEA URAIS KAMA MJUMBE WA CC YA CCM NA SIYO WAZIRI MKUU.

WAGOMBEA UBUNGE WANAMWOMBEA KURA MGOMBEA URAIS KWENYE MAJIMBO YAO TU.

MJUMBE WA CC HANA MAMLAKA YA KUAMRISHA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YOYOTE KUFANYA CHOCHOTE.

SHERIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI ZINAELEKEZA HIVYO.

TUME YA UCHAGUZI TOENI MWONGOZO.

Umesema kweli, ilahiyo tume si imetumwa na mkuu? Hivyo itafanya kazi kulingana na maazigizo ya aliyeituma.
Ni vizuri kuonesha kutokubaliana na hili kwenye sanduku la kura
 
Mfumo kama huo upo nchi gani?
Kwani mfumo wa Rais kukataza vyama vya Siasa kufanya kazi za Siasa lakini chama chake kikiwa kinafanya hizo siasa ni mfumo unaofanywa na nchi ipi?
Yaani mkuu unategemea kua kila kitu lazma tuige kwa wenzetu ila wao awawezi kuiga kwetu.....Ebu fikiria basi zaidi
 
Unaona sasa yani tatizo yote hayo tunayafikiria kwa sababu ya kuikomoa ccm na Magufuli wake na ndio maana mfumo huo sehemu zengine hakuna.
 
Kwa hiyo mtu akiwa Mgombea kwenye jimbo flani basi haruhusiwi kwenda Mkoa mwingine wowote kumpigia Debe Mgombea Mwingine?
Je ni kweli kwamba Wagombea Urais wa Vyama Vyote kwa TZ hawazunguki kunadi sera zao na watu wa Majimbo mengine??
Waziri Mkuu pia ni Mtanzania NA ana haki yake Kikatiba kwenda Mkoa wowote kama RAIA Mwingine wa Tanzania.
Cha muhimu ni Kuwa Tujitahidi Tarehe ya Uchaguzi Ikifika Twende Tukapige Kura. Chagua Unayemtaka!
Humu Jukwaani (online) na Vijiweni tutapiga makelele kimaandishi bure tu. Just mark the date, when the time comes go and cast your vote!!

ELEWA:-

Waziri Mkuu:- ni Mtendaji Mkuu wa Serikali, na AKIFANYA ZIARA YA KISERIKALI anakutana na Watendaji ngazi za MIKOA na WILAYA Watumishi ambao wako chini ya MAMLAKA yake (wako wanaccm na wa VYAMA tofauti na ccm) ambapo WAKURUGENZI wa HALMASHAURI ni Wasimamizi wa Uchaguzi,

anapoanza kupiga KAMPENI KWA CHAMA HADHARANI ni wazi kwamba WAKURUGENZI kwa kulinda AJIRA ZAO watapindisha SHERIA na KANUNI za uchaguzi ili KUFANIKISHA KAMPENI YA BOSS WAO.

NDIYO YALE YALIYOTOKEA KWA KUENGUA WAGOMBEA WA VYAMA PINZANI KWA CHAMA CHA WAZIRI MKUU.

Hivyo basi, Waziri Mkuu akitaka KUMPIGIA KAMPENI BOSS WAKE, AACHE MAJUKUMU YA WAZIRI MKUU, AFUATANE NA MGOMBEA URAIS KAMA ANAVYOFANYA POLEPOLE.

Akiona kuna JUKUMU LA WAZIRI MKUU AACHE msafara wa KAMPENI ili akatekeleze au kutoa MAELEKEZO YA KIWAZIRI MKUU. Kisha arudi kwenye mikutano ya KAMPENI.

AU AKAFANYE KAMPENI KWENYE JIMBO ANALOGOMBEA.

WAZIRI MKUU SIYO MTENDAJI WA CHAMA.

WAPO WATENDAJI WA CHAMA.
 
Kwahiyo kama sasa kipindi hiki cha kampeni nchi ingetakiwa iwe haina rais?
Hawajiamini, kipindi chote cha miaka mitano kazi yao kususia vikao vya bunge halafu leo hii wanakuja na kisingizio cha rais kuwa na faida ya chama chake kuwa ni chenye madaraka.
 
Back
Top Bottom