Benzodiazepine
JF-Expert Member
- Oct 18, 2018
- 644
- 718
RAIS BADO YUPO KAZINI, MUDA WAKE WA URAIS BADO HAUJAISHA. HIVYO NI SAWA TU MUACHE AENDELEE NA MADARAKA NA MAMLAKA YAKE KAMA RAIS.Katika kampeni zinazoendelea, nimeona zinakibeba chama cha mapinduzi kwa sehemu kubwa, kwani viongozi wanaogombea bado wanako madarakani na wamekuwa wakiendelea kutoa maagizo kwa mamlaka zilizo chini yao,
Mfano: Unakuta mgombea urais anatoa maagizo ya kujenga barabara na pia kutoa pesa hadharani kama zawadi, Makamu wake akiagiza halmashauri kuongeza pesa za mikopo kwa vikundi mbalimbali, huku Waziri mkuu akiagiza kurejeshwa kwa baadhi ya mashamba huko Singida.
Hivi hao wapinzani wakitoa misaada wakati huu wa kampeni si watachukuliwa wanatoa rushwa?
Natamani katiba ibadilike tu, kikifika kipindi cha kampeni kila aliyekuwa na madaraka avuliwe ili waingie uwanjani wakiwa katika kiwango kimoja tofauti na sasa.
PIA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU NAO PIA BADO WAPO KAZINI VILE VILE. Hivyo acha wafanye kazi!
Cha muhimu ni kwamba Tusiishie Online tu na Kupayuka bali Tuzingatie Muda wa Kupiga Kura Ukifika basi Tukapige Kura.