Nimegundua kusudi lililo nileta duniani. Nimeanza kuliishi kusudi hilo na linanilipa

Nimegundua kusudi lililo nileta duniani. Nimeanza kuliishi kusudi hilo na linanilipa

Kusema tumeumbwa kuabudu ni sawa na kusema mzazi amezaa ili asalimiwe.

Salamu ni heshima, mzazi akiipata anafarijika ila ukimnyima anasononeka hakuna zaidi ya hapo. Haiongezi wala kupunguza chochote zaidi ya kufarijika na kusononesha.

Inawezekana kwa MUNGU ni hivyo hivyo. Ibada inamfariji, inamfurahisha. Kutokufanya ibada kunamsononesha na hakuna zaidi ya hapo.(HII NI KWA WANAOAMINI, KAMA HUAMINI KUHUSU MUNGU HAIKIHUSU)

Kuhusu kuja duniani kufanya starehe ni sawa na kusema mtoto yupo ili acheze. Ukishasalimia na kuzungumza na mzee au mama unaenda kicheza kwa raha zako na mzazi anakutazama unavyocheza na anafarijika. (HII NI KWA WANAOAMINI, KAMA HUAMINI KUHUSU MUNGU HAIKIHUSU)

Ukishafanya ibada au kusali nenda kastarehe kwa raha zako huku ukizingatia miongozo ya dini uliyochagua kuiamini.
Wewe umekwishajipata jamaa
Baba kampa yote mwanae
Baba kavuta Kiti ametulia
 
Hapungukiwi lolote, umepewa uhuru wa kuchagua cha kufanya hapa duniani, ila ukirejea kwake yeye ndiye mwenye maamuzi juu yako kama alivyo amua kukuleta hapa duniani.
Mungu sio mwanadamu mkuu. He doesn't think the way you think. He doesn't need anything from you.

wacha kujipa umuhimu huo kwa Mungu.
 
Mungu sio mwanadamu mkuu. He doesn't think the way you think. He doesn't need anything from you.

wacha kujipa umuhimu huo kwa Mungu.
Umuhimu upi nimejipa kwa Mungu? Wapi nimesema Mungu ni kama mwanadamu?
 
Dini ya ukweli ni UPENDO Mungu ametuumba ili tujifunze na tukifa tunarudi nyumbani yaani tunarudi tulipotoka kabla hatujazaliwa, kwahiyo kwenye kujifunza ukifaulu utaishi maisha mazuri na kustarehe uki fail utakumbana na msoto mkali wa ugumu wa maisha hapo hata starehe haitowezekana lakini as long as binadamu tumepewa akili inabidi akili itumike fully ili mambo yawe sawa.
 
BTW, heaven will be the most boring place to be. Imagine utakuwa unaabudu 24/7, unaimba 24/7, kula asali, matunda na maziwa....really boring!!
😆😆😆....unataka starehe na wew ukaoe malaika .....
 
Wewe ndo umeharibu kabisa mkuu yani ume mu-humanize Mungu. Mungu na kusononeka wapi na wapi mkuu?

Mungu anahitaji faraja?
Ukisoma maandiko inaonyesha MUNGU ni roho, ni roho inayopatwa na hasira, huzuni, kusononeka, furaha n.k

Mfano Mwanzo 6:5-22 kwenye gharika biblia imeweka wazi kuwa BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu, akahuzunika moyo.
Mungu anayajua maisha yako yote hata kabla hujaumbwa. Chochote utakacho kifanya sasa hivi, hawezi kuwa surprised kwa sababu alisha kijua hata kabla hajazaliwa. He is not a human being.

Please stop thinking of God like that.
Hii ni kawaida boss, hata wewe hapo kazini unajua utalipwa mshahara na ukilipwa unafurahi kweli. Hata MUNGU anajua utakalofanya na ukilifanya linampa raha au huzuni.
 
Ng'ombe hajui dhumuni la mfuga ng'ombe
Naamini pia sisi hatujui dhumuni
Lakini kwa kuwaza nje ya box nadhani

Sisi ni kama mazao tu tukiishi kwa kutenda mema roho wa Mungu anapata kuwa imara au kushiba hata ukifa kama ni mtenda mema ina maana ni faida kwa Mungu amepata mazao ile roho yako njema ni kama chakula kwake anazidi kuwa strong ndiyo maana tunaimizwa kutenda wema, pia tuijaze dunia (mazao)
Kutenda dhambi ni faida ya shetani anapata msuli wa kutunisha huko unakuwa chakula yake
 
Kabisa mkuu, MUNGU NI UPENDO. Huo UPENDO uwe wa kweli real love, unconditional love( AGAPE )
Mungu ni Pendo na hana upendeleo, wote katupa pumzi, wote anatunyeshea Mvua, wote anatuangazia jua, shida ni sisi tu tunajistukia sana na kuanza kutengeneza mungu wetu wa visasi eti usipofanya hivi atakufanya vile (that's not love)
 
imeandikwa kwenye vitabu vya imani " enendeni mkazaliane muijaze dunia" .

Elewa maana ya neno " mkazaliane"
Kwahiyo mkuu uzinzi ndio starehe? Unatia aibu bro, ulikuwa unaheshimika sana humu JF ila unazidi jitia aibu tu.
 
Back
Top Bottom