Ukisoma maandiko inaonyesha MUNGU ni roho, ni roho inayopatwa na hasira, huzuni, kusononeka, furaha n.k
Mfano Mwanzo 6:5-22 kwenye gharika biblia imeweka wazi kuwa BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu, akahuzunika moyo.
Hii ni kawaida boss, hata wewe hapo kazini unajua utalipwa mshahara na ukilipwa unafurahi kweli. Hata MUNGU anajua utakalofanya na ukilifanya linampa raha au huzuni.
Mwanzo 6: 6 inasema " Mungu alijuta kwanini alimuumba mwanadamu".
Hiyo ni lugha ya kiroho imetumika hapo wala haimaanishi kwamba eti Mungu alijutia kumuumba mwanadamu. Je Unataka nikwambie maana yake?
1. Mungu hawezi kuhuzunika.
2. Mungu hawezi kupatwa na hasira.
Mungu hawezi kuhuzunika kwa sababu nothing surprises him. He lives above the time. In the realm of the spirits, the past, present and future exist in the same now..
Mungu hawezi kuhuzunishwa na chochote kwa sababu yeye ni mwanzo na mwisho. Mambo yote alisha yaona hata kabla hayajatokea. So hakuna kinacho msurprise. Ili uweze kuhuzunishwa na jambo ni lazima kwanza uwe hujui nini kitatokea mbele..
Mungu hawezi kupatwa na hasira. Hakuna kitu kinacho weza kumkasirisha Mungu kwa sababu;
1. Ili jambo liweze kukukasirisha ni lazima iwe kitu ambacho hukukitarajia. Mungu anajua kila kitu utakacho kifanya hata kabla haujazaliwa. Unapo fanya jambo baya unakuwa hujamsurprise Mungu kwa sababu tayari alisha jua. So hawezi kukasirika..
Pili : Kama wewe mwanadamu unaweza kumfanya Mungu akasirike basi tafsiri yake ni kwamba wewe unaweza ku control " emotions" za Mungu. Unaweza ku control how God think. Jambo ambalo haliwezekani.
Wewe mwanadamu huna uwezo wa kumfurahisha wala kumkasirisha Mungu.
Hupaswi kujipa umuhimu huo kwa Mungu kabisa.
Kuna mlokole mmoja alikuwa na imani hiyo basi siku moja akawa anasali anamtishia Mungu kwamba endapo hato mpa mtaji wa biashara basi atakuwa shoga.