Habari zenu,
Nina jambo ambalo linanitatiza jamani. Mimi ni mkazi wa Dar na asili yangu ni mkoa fulani ukanda wa pwani. Nimetokea kwenye familia za kiswahili, baadhi wamenielewa familia za namna gani.
Naomba niende straight to the point ni hivi nimegundua ndugu yangu wa damu ni mshirikina yan mchawi au mwanga. Mimi nilikuwa naandamwa na mitihani mingi ya kiswahili magonjwa ya ajabu, vifungo yan kila aina ya nuksi imeniandama. Sasa huyu ndugu yangu alikuwa mstari wa mbele kunipeleka kwa waganga kutafuta suluhu. Na huko tulikuwa tunaambia watu fulani wananifanyia hivi. Sasa kumbe huyu mtu na yeye ni mshirika mkuuu na ila alikuwa ananizunguka kwa hao waganga.
Kisa ni kirefu sana na kuhusu kujihakikishia hili jambo nimejihakikisha kabisa mpaka nimefika kuandika hapa., ila sasa baada ya kugundua nimepata uoga sana maana ni ndugu wa damu na tunaishi nyumba moja.
Nahofia maisha yangu sina amani, na hapa nilipo nimepigwa kombora mwili wote unauma yaani nimekuwa kama mzee hata kutembea kwa dakika 10 siwezi.
Naomba mnisaidie ushauri japo kwa ufupi.
Wale wa matusi na kejeli naomba mnihurumie mpite kimya kimya