Nimegundua ndugu yangu wa damu ni mshirikina

Nimegundua ndugu yangu wa damu ni mshirikina

N
Habari zenu,

Nina jambo ambalo linanitatiza jamani. Mimi ni mkazi wa Dar na asili yangu ni mkoa fulani ukanda wa pwani. Nimetokea kwenye familia za kiswahili, baadhi wamenielewa familia za namna gani.

Naomba niende straight to the point ni hivi nimegundua ndugu yangu wa damu ni mshirikina yan mchawi au mwanga. Mimi nilikuwa naandamwa na mitihani mingi ya kiswahili magonjwa ya ajabu, vifungo yan kila aina ya nuksi imeniandama. Sasa huyu ndugu yangu alikuwa mstari wa mbele kunipeleka kwa waganga kutafuta suluhu. Na huko tulikuwa tunaambia watu fulani wananifanyia hivi. Sasa kumbe huyu mtu na yeye ni mshirika mkuuu na ila alikuwa ananizunguka kwa hao waganga.

Kisa ni kirefu sana na kuhusu kujihakikishia hili jambo nimejihakikisha kabisa mpaka nimefika kuandika hapa., ila sasa baada ya kugundua nimepata uoga sana maana ni ndugu wa damu na tunaishi nyumba moja.

Nahofia maisha yangu sina amani, na hapa nilipo nimepigwa kombora mwili wote unauma yaani nimekuwa kama mzee hata kutembea kwa dakika 10 siwezi.

Naomba mnisaidie ushauri japo kwa ufupi.

Wale wa matusi na kejeli naomba mnihurumie mpite kimya kimya
Nenda kwa Mwamposa
 
Mimi sio mchawi wala mshirikina. Namuomba Allah aniweke mbali na mambo hayo kabisa.

Unasema humjui Allah ni nani na humfahamu! Allah ni Muumba wangu na wako na Muumba wa kila kitu, Mwenye Kuturuzuku. Mola wa Walimwengu wote. Yule aliye kipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa. Hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Yeye ni Mmoja tu, hana mshirika. Ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo washirikina. Sifa zote njema zinamstahiki Yeye, na Yeye ni Mwenye Majina mazuri mazuri.

Muabudu Yeye tu Peke yake na umuitikie Mtume wake, hiyo ndio asili yako na maumbile yako ya asili, ukifanya hivyo utaongoka.
Thibitisha kuwa huyo ala kaumba
 
Kuna njia mbili za wew kupata msaada wewe utachagua moja ... jitafakari rudi kafanye ibada mwombe MUNGU tafta sadaka maalum ya kujitakasa hakika MUNGU ni mwenye rehearsal nyingi atakufunika dhidi ya watu wabaya ...adui zako watakuwa adui wa MUNGU.... njia ya pili ni wew kwenda kwa mganga konki MshanaJR atakupa mwongozo ..... ila na sisitiza njia ya kwanza ndo best
Bado unamshawishi mwenzio akatoe alichonacho ampe ambae anacho duhh!!!
 
Wewe mchane ukweli tuu,,"Mwambie nduguu!!kuliko haya mateso unayonipa kwa mauchawi yako ya kinyoko mbili si bora uniue tuu Mamameeehh"huku macho makavuuu!!!
Sure kama mbwai mbwai...kuna kipindi kuna bibi mtaani alikua anasifika kwa ulozi..sasa wtt walikua wakicheza anawaangalia kwa macho makali sana..nikasema huyu dawa yake na mm nikae pale pale nimwangalie direct bila kupepesa jicho...nilimwangalia mpk akageuza macho nikaongea kwa nguvu nikasema nasikia kuna wanga hapa waje vuzuri pande hizi...kumbe sina lolote nilitaka kumpa tuu jamba jamba..mbona sijawahi kuona lolote mpk nikahama hapo..muda mwingine truth heals...sema ukweli kila kitu kitabadilika..
 
Back
Top Bottom