Dawa ya mchawi ni ndogo sana, sio kuokoka wala kumuita yesu. Japo ni kweli kuokoka inasaidia kwa kiasi fulani.
Ukishaziinua nguvu zako za kiroho kwa KUJITAMBUA kuwa wewe ni ZAIDI YA MWILI, basi UMESHASHINDA VITA ZOTE.
Wachawi wanafanya kazi kupitia ujinga wetu, lakini nguvu zao ni ndogo sanaa ukiwavalia njuga.
Kuna mmoja alinijaribu alikiona cha mtema kuni, siku hizi ananiamkia shkamoo japo amenizidi umri.
USHAURI WANGU KWAKO:
1. Achana na mawazo yote HASI ya kushindwa, kuharibikiwa, sijui nuksi. KUWA CHANYA.
Unapokuwa CHANYA, yale manguvu ya kichawi yanaanza kudondoka moja baada ya nyingine. Na kama kuna MAJINNI ameyatuma yakuvuruge yataanza kukimbiaa maana hayataweza kustahimili MAWIMBI CHANYA ya ushindi, mafanikio, furaha na amani ya moyo.
Nimeyaita MAWIMBI kwa sababu kwa hakika ni MAWIMBI ambayo yanakuja kwako kutoka kwenye ULIMWENGU. Ni kama UMEME fulani ambao wewe hauuoni kwa macho lakini ni UMEME haswaa!
Unapokuwa CHANYA, unavuta MAWIMBI CHANYA, and vice versa is true.
MAJINNI na mauchawi yanapenda nguvu HASI za huzuni, kukata tamaa, unyonge na kushindwa. Unapokuwa katika hii halii, yanapata nguvu maradufu.
Unapokuwa mnyonge unavuta MAWIMBI HASI kutoka kwenye ulimwengu, na hapo ndipo MAJINNI yanazidi kukutafuna kwa sababu yanapenda sana yale MAWIMBI HASI ya unyonge nyonge. Ni kama CHAKULA CHAO.
Hii inaitwa SHERIA YA UMEME WA KIROHO.
2. Amka uache kujiweka kizembe zembe. Wewe ni MKUU kuliko WACHAWI.
Unajiona mdogo kwa sababu uko ndani ya MWILI, lakini laiti ungalijua wewe ni MUNGU tena MKUU, ungeanza sasa kuwasambaratisha hao vigagula kwa moto wa radi.
3. Unaweza kuumba chochote unachotaka. Jifunze KUTAMKA kwa sababu ulimwengu wa roho unaendeshwa KWA MANENO YAKO na HISIA ZAKO. Unalolitamka na unalolihisi ndilo linalotokea.
Hii inaitwa SHERIA YA UUMBAJI.
Kama MATAMSHI yako yanaweza kuunda jambo lolote kwenye ulimwengu wa roho, na kwa kuwa wewe unatumia NGUVU CHANYA ZA ULIMWENGU, basi nadhani umeshanielewa la KUFANYA.
KAZI KWAKO.