Nimegundua ndugu yangu wa damu ni mshirikina

Habari zenu,

Nina jambo ambalo linanitatiza jamani. Mimi ni mkazi wa Dar na asili yangu ni mkoa fulani ukanda wa pwani. Nimetokea kwenye familia za kiswahili, baadhi wamenielewa familia za namna gani.

Naomba niende straight to the point ni hivi nimegundua ndugu yangu wa damu ni mshirikina yan mchawi au mwanga. Mimi nilikuwa naandamwa na mitihani mingi ya kiswahili magonjwa ya ajabu, vifungo yan kila aina ya nuksi imeniandama. Sasa huyu ndugu yangu alikuwa mstari wa mbele kunipeleka kwa waganga kutafuta suluhu. Na huko tulikuwa tunaambia watu fulani wananifanyia hivi. Sasa kumbe huyu mtu na yeye ni mshirika mkuuu na ila alikuwa ananizunguka kwa hao waganga.

Kisa ni kirefu sana na kuhusu kujihakikishia hili jambo nimejihakikisha kabisa mpaka nimefika kuandika hapa., ila sasa baada ya kugundua nimepata uoga sana maana ni ndugu wa damu na tunaishi nyumba moja.

Nahofia maisha yangu sina amani, na hapa nilipo nimepigwa kombora mwili wote unauma yaani nimekuwa kama mzee hata kutembea kwa dakika 10 siwezi.

Naomba mnisaidie ushauri japo kwa ufupi.

Wale wa matusi na kejeli naomba mnihurumie mpite kimya kimya
Kuna mambo ningeandika. Ila nakunasihi kama wewe ni Muislam, rudi kwa Mola wako utubie na ubadilishe mtindo wako wa maisha kwanza. Niishie hapa.

Pili, mmejikaribisha kwa mashetani, na sasa yanawagombanisha na kuwavuruga.

Niishie hapa.

Kazakh destroyer
 
Asante kwa ushauri ..yan nimechoka sana. Yeye ndio alikuwa mstari wa mbele kunipeleka kwa mashekh na waganga kumbe alikuwa ananizunguka
Kama utakuwa tayari, nicheki inbox nikupe connection ya mganga kwelikweli. Atamwondoa huyo nduguyo, na maisha yataendelea vema.
 
Uchawi si pua ambayo lazima uiache nje ili uvute hewa, hicho uchawi au wachawi wana siri sana, hivyo nikiambiwa lazima ni fuatilie na aliyeniambia lazima anipe sababu sewezi mkatalia kabisa .
Huo utakuwa ni upumbavu. Nimemkumbuka yule mtu aliyemuua mkewe huko Tabora kama sijakosea. Alikwenda kwa mganga, mganga akamuambia kuwa atamuota mbaya wake, akamuota mkewe. Akamuua. Sasa ana kesi ya mauaji. Uzi wa hiyo habari niliuona humu humu.

Yaani uambiwe mama yako mzazi ni mchawi, halafu ufuatilie kama ni kweli!!! Huyo shetani mfitinishaji akikuambia sababu utafanyaje? Na ukifuatilia na mashetani yakakuchezea ukaona ni kweli mama yako mzazi ni mchawi utafanyaje?

Nikiona comments za namna hii huwa namshukuru Allah kwa neema ya Tawheed.
 
Yan kanitia nuksi sasa yeye hana maisha yoyote mimi ndio naisaidia familia nzima.. mpaka pesa ya kula mimi ndio nampa. Nimechoka kisa ni kirefu na kinasikitisha napitia magumu sana
Ungetupa kisa sasa tujifunze hata wenzio tunarogwa hapa na kaka zetu wa damu Mungu tu anasaidia
 
Huo utakuwa ni upumbavu. Nimemkumbuka yule mtu aliyemuua mkewe huko Tabora kama sijakosea. Alikwenda kwa mganga, mganga akamuambia kuwa atamuota mbaya wake, akamuota mkewe. Akamuua. Sasa ana kesi ya mauaji. Uzi wa hiyo habari niliuona humu humu.

Yaani uambiwe mama yako mzazi ni mchawi, halafu ufuatilie kama ni kweli!!! Huyo shetani mfitinishaji akikuambia sababu utafanyaje? Na ukifuatilia na mashetani yakakuchezea ukaona ni kweli mama yako mzazi ni mchawi utafanyaje?

Nikiona comments za namna hii huwa namshukuru Allah kwa neema ya Tawheed.
Huwa sibishani na jamii kama yako maana huenda ni wale wale, hivi ukisikia mchawi unazani anaroga akina nani kwa mfano! Watu wanaokataa na wao huwa wanachama, halafu mie Allah simjui wala kumfahamu.
 
Kabisa mkuu, yaani nikupambana naye kwa IBADA, mi saivi ananiogopa sana na akiwa anakuja kuniloga namuona na anashindwa, nipo vyema kiroho nashukuru sana maombi na Ibada za Kuhani Musa zimenijenga
Sema mkiokoka mnakuwaga kama machizi[emoji28]unaweza kumuona mchawi wewe bila uchawi?
 
Habari zenu,

Nina jambo ambalo linanitatiza jamani. Mimi ni mkazi wa Dar na asili yangu ni mkoa fulani ukanda wa pwani. Nimetokea kwenye familia za kiswahili, baadhi wamenielewa familia za namna gani.

Naomba niende straight to the point ni hivi nimegundua ndugu yangu wa damu ni mshirikina yan mchawi au mwanga. Mimi nilikuwa naandamwa na mitihani mingi ya kiswahili magonjwa ya ajabu, vifungo yan kila aina ya nuksi imeniandama. Sasa huyu ndugu yangu alikuwa mstari wa mbele kunipeleka kwa waganga kutafuta suluhu. Na huko tulikuwa tunaambia watu fulani wananifanyia hivi. Sasa kumbe huyu mtu na yeye ni mshirika mkuuu na ila alikuwa ananizunguka kwa hao waganga.

Kisa ni kirefu sana na kuhusu kujihakikishia hili jambo nimejihakikisha kabisa mpaka nimefika kuandika hapa., ila sasa baada ya kugundua nimepata uoga sana maana ni ndugu wa damu na tunaishi nyumba moja.

Nahofia maisha yangu sina amani, na hapa nilipo nimepigwa kombora mwili wote unauma yaani nimekuwa kama mzee hata kutembea kwa dakika 10 siwezi.

Naomba mnisaidie ushauri japo kwa ufupi.

Wale wa matusi na kejeli naomba mnihurumie mpite kimya kimya

Upo Dar?
 
😁 watz kama nyie ndio mnataka kuandamana Kisa bandari?akilia zetu zipo mat*Koni sijui?Hao waganga ulikoenda kuzunguka nae hawakumstukia kuwa ndugu yako mwanga?Kwa hiyo umempata mganga mwingine konki?Yaani ushuzi mtupu.
 
Chukuwa mafuta ya mwamposaa na maji yake tumia [emoji109]mwaga maeneo yote utatupa mrejesjo Wenda Kaka ako akawa chizi
 
Back
Top Bottom