Nimegundua nipo kwenye level ya mwisho kabisa ya Maumivu

Nimegundua nipo kwenye level ya mwisho kabisa ya Maumivu

Mfilisiti

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2020
Posts
460
Reaction score
2,322
Champion popote ulipo Amani iwe nawe.

Level ya mwisho ya Maumivu kwa mwanadamu ni pale unapo achilia kicheko ili kuziba mwanya wa maumivu(demage) na si kuhuzunika.

Kupitia maumivu nimeyatambua haya:

1: Ukiwa hapa Duniani, Ukiwa umepigika jua hiyo ndo jehanamu yako, achana na story za kuna siku utafufuliwa uchomwe moto au kwenda peponi.

2: Kama Mungu yupo, basi nayeye kuna vitu anakua anatamani kuvifanya kwako mwanadamu ila anashindwa.

3: Kuna muda kila kitu utakifanya kwa usahihi na uangalifu lakini bado utafeli.

4: Nimetambua ninapambana vita ambayo wazazi wangu hawakuishinda. Na hapo ndipo ninapokumbuka hata na wao walikua na ndoto but what happened?? Najishangaa ndoto yangu taratibu inabadilika kutoka kuwa mguso wa jamii na sasa kuwa mguso wa kaya!! what a downfall.

5: Wakati wako wa kupigika ukifika acha kutafuta faraja, Maumivu makali ndio yatakunausua hapo ulipo.

Disappointed but not surprised!!
 
Haya mambo imagine mtu mwingine anasoma na hujui anapitia changamoto gani mwisho wa siku ataona kama kuna mwingine anapitia na solution ndio kama hivi hataona shida kufanya maamuzi ya ajabu. Haya mambo yataanza kuonekana ya kawaida hatujui tunategemea jamii ya namna gani.
 
Hivi kwanini mods wana entertain hizi mada. Haya mambo imagine mtu mwingine anasoma na hujui anapitia changamoto gani mwisho wa siku ataona kama kuna mwingine anapitia na solution ndio kama hivi hataona shida kufanya maamuzi ya ajabu. Haya mambo yataanza kuonekana ya kawaida hatujui tunategemea jamii ya namna gani.

Moderator Tafadhali msipuuzie haya.
Ndiyo uhalisia wa watu wengi hasa wanaume ambao wengine wanapambana na changamoto za maisha na zile za afya ya akili na hawana pa kusemea.

Acha waziseme hisia zao, hii tabia ya kuwapangia wengine kipi cha kusema na kipi wasiseme siyo poa!

Soma pia:
 
Haya mambo imagine mtu mwingine anasoma na hujui anapitia changamoto gani mwisho wa siku ataona kama kuna mwingine anapitia na solution ndio kama hivi hataona shida kufanya maamuzi ya ajabu. Haya mambo yataanza kuonekana ya kawaida hatujui tunategemea jamii ya namna gani.
Watu waache kuzaa , binadamu wanalazimisha furaha ila bora kufa ukapumzike
 
Hamna faraja kila siku ni mitihabi mipya

Naona sana replies zako kwenye nyuzi, unaandika kama mtu ambaye amechoshwa na maisha.
Pole sana kwa mitihani unayopitia!

Nbc Hug GIF by New Amsterdam.gif
 
Ningekua mimi ndio nina uwezo kama wa huyu Mungu anaesemwa kila siku ningewapa furaha na mahitaji yenu yote hadi mnitukane.... Hata mkinitukana kwa furaha zenu nazidi kuwapa mema sababu hata mkinitukana sipungukiwi na chochote
Majambazi ningewapa wanachohitaji ili wasiibe, malaya na wanunuzi wake ningewapa wanachohitaji ili wasifanye hayo... Mafisadi ningewajaza mihela hadi waone hamna sababu ya kufanya ufisadi nk
 
Back
Top Bottom