Nimegundua wanawake wengi wanaolewa na watu wasiokuwa wa ndoto zao!

Nimegundua wanawake wengi wanaolewa na watu wasiokuwa wa ndoto zao!

Mimi nadhani suala la mapenzi ni "illusion" tuu hakuna mtu anaempenda mwenzake. Sio mwanaume wala mwanamke. Wote tuko ki maslahi na mara nyingi siku hayo maslahi yakikoma na shughuli nzima inaishia hapo.
 
Kiranga amesema juu hapo ndoto ni kwaaajili ya kuota tu 😁

Naona watu wanahoji huyu kuota hiki.

Ndoto ni haki ya kibinadamu, kwa hiyo ukihoji kwa nini huyu anaota hiki kitu kikubwa sana ni kama unakuwa mkatili kumnyima mtu haki yake ya kuota.

Yani kitu mtu hawezi kabisa kukipata maishani, halafu unatakaje kumnyima hata nafasi ya kujifariji kwa kukipata ndotoni?

Mwanetu alikuwa na ndoto ya kumuoa mtoto wa Obama hapa, wakati hata kukutana naye tu mzozo.

Wengine hatukutaka kumnyanyapaa tulimuangalia tu anafaidi haki yake ya kuota.

Baadaye kakua kaiacha ile ndoto mwenyewe 😂😂😂
 
Back
Top Bottom