Nimehamia Yanga Rasmi

Nimehamia Yanga Rasmi

Sitaki kuzeeka mapema kisa timu ya mpila. Hela nitafute kwa shida pia hata timu ya mpila nayo inipe stress??
Wana Simba mtanisamehe sana, kwa Yanga hii tutasubiri sana.
Kama huwezi kushindana nao basi ungana nao..

Nipo tayari kuitwa msaliti........
Njooni Yanga, Supu mutakunywa na na siku za kuishi zitaongezeka kwa raha na furaha mutakazopata.
 
Anohama team kwa maslahi sio sawa na kuhama team kama shabiki. Upenzi kitu chengine wee. Mie simba hata ifungwe magoli 100 siwezi kwenda Yanga hata kwa bahati mbaya
Baki na mipresha yako..!! Na leo hii mkitolewa tafuteni kwa kuishi..!!
 
Binafsi sijaweza, nitakufa nikiwa shabiki wa Simba SC haijalishi tutakuwa nafasi ya ngapi
Sawa mkuu, mimi ndio nimeshamove on ivoo. Na nimefollow page yao Instagram. Natarajia mambo makubwa kwa hii timu ambayo hayakuweza kufikiwa huko nilipokuwa, nawaona wanaenda kuteka soka la vilabu barani Afrika, labda itokee ajali za kimpira maana mpira unakuwaga na suprize zake
 
Watu wanavua gamba tuuuu
 

Attachments

  • 20240331_042633.jpg
    20240331_042633.jpg
    113.6 KB · Views: 1
Tunatarajia mbumbumbu wengine wengi kukufuata baada ya Al Ahli Tripoli kupiga kwenye mshono
 
Huwa hakuna shabiki wa aina hiyo. Mashabiki wanaweza wakaiacha timu yao na kwenda kuanzisha timu zao au huenda kuchukua timu iliyo dhaifu na kwenda kuiongezea nguvu, lakini huo ushabiki wa kuhama timu kisa inafanya vibaya haupo.
Timu inapofanya vibaya maana yake ni wakati wenu wa ku feel challenged kuingia kuongeza support, siyo kukimbia.
Mfano mzuri ni wale walioiacja Yanga mwaka 1936!wakaenda kuanzisha timu yao ikaitwa Queens, baadaye Sunderland na baadaye tena Simba, wengine tena wakaiacha Yanga na kwenda kuanzisha timu yao wakaiita Pan African.
Mwingine akaiacha Simba na kwenda kuanzisha Azam
Azam uongo ni nyota nyekundu.
 
Azam uongo ni nyota nyekundu.
Upo sahihi, Nyota Nyekundu ilijimega kutoka Simba ila Azam pia ilianzishwa na aliyetoka Simba baada ya kutoridhishwa na mwenendo ndani ya Simba.
 
Back
Top Bottom