Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo


Mshana,alisha wahi sema kwamba"mchawi awezi kukupata kama auja ingia kwenye mtandao wao.

Alimaanisha kwamba kitendo cha wewe kwenda kwa mganga kutatua matatizo yako,apo ndio unaingia kwenye mtandao pia.

kwa maelezo hayo basi kama na wewe ilisha wahi kuwa mshilikina basi,lazima wachawi wata kunanasa kiraisi.

Mshana Jr.
 
Weka chanzo mkuu sio unaongea tu maana mdomo unaumba 😁😁

Watu kibao tu wanarogwa hawajawahi kumjua hata mganga, watoto wachanga tu wanasumbuliwa na wachawi sembuse mtu mzima.
 
Mpaka sasa duniani hakuna anaujua uchawi kama upo na unafanya kazi au la habari za uchawi zimekuwa za siri kwakuwa uchawi hauna nguvu yoyote na matokeo ya uchawiuchawi ili uweze kufanya kazi lazima wewe unaerogwa lazima ukubali kuwa uchawi upo na una nguvu usipo kubali haurogeki hata kwa bakora

Kuna safari moja katika maisha yangu nilikuwa na uhusiano na mtoto mmoja mweupe mzuri huyo aisee pale mtaan watu walikuwa wanomuogopa kipindi hiko niko form 4 kwakuwa bibi yake alikuwa eti mchawi

Mh kwa ule uzuri aisee nilisema siwezi kumuacha maana kwanza alinifata mwenywe eti nimfundshe hesabu

Mtaa mzima ulikuwa unamuogopa huyo bibi ila yule bibi nikienda kumuulizia mjukuu wake ananikaribisha tu vzr kwake watu achana na huyo mtoto huyo bibi mchawi atakuroga watu mtaani waninipa ushauri

Mm nikasema uchawi hauna nguvu that's why wachawi wengi maskini hawawezi kujisaidia kupitia huo uchawi

Tukadumu na yule mtoto kwa miaka kama 3 na wala sikurogwa
Ningewasikiliza watu wa mtaani nisingempata
Na haya ndio maneno ya watu kila siku uchawi uchawi ulishawahi kuuona au kuhushudia ?
Na kama umeona umejuaje kama huu ni uchawi?
 
Siyo lazima "kwenda kwa waganga" ndipo uwe umeingia "kwenye mtandao" wa kishetani. Kwenda kwa waganga ni mfano mojawapo tu miongoni mwa sampuli zisizohesabika za mtandao wa Iblisi kuwanasia watu wajiunge kwenye ufalme wake wa giza. Kuna very clear physical, mental, spiritual & psychological "frequencies na anga" za mapepo ambazo ukikatiza, lazima tu rada ya adui ikunase.
 
Najifunza kwamba haukubali uchawi au ushirikina upo kwa sababu hujarogwa wewe. Je hiyo unaona ni sababu ya msingi ya kutowepo uchawi???
 
Hao mabeberu si mmewaita wenyewe na mkasainiana nao mkataba kwani waliwalazimisha?wewe kama ni mzungu mchawi hana time na wewe kwa sababu hata ukivuna pesa ukatajirika utaenda kutumia kwenu Ulaya ila ukimpora shamba lake kinguvu hapo ndipo utakapojua kwa nini muuza kahawa ana chombo cha moto lakini hana leseni au ndipo utakapojua kwa nini draft lina vyumba lakini havipangishwi
Kwahyo wachawi wanawapotezea boko haram,IS, Al shabab etc kwasab ni wageni na hawana bifu nao,wanawapotezea mabeberu yanayotunyonya waafrica kwenye madini na rasilimali zetu nyingine kwasab ni wageni na hawana beef nao,[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Kumpata huyo mtoto sio kigezo kwamba uchawi hauna nguvu,inawezekana huyo bibi hakuona sababu ya kukudhuru kwa sababu hauna kibaya ulichomfanyia alichukulia wewe ni rafiki wa mjukuu wake.

Na kingine pia confidence yako ilikusaidia kwa kuonesha kwamba wewe si mtu mbaya,ila ungekuwa unaenda kwa kuvizia hapo angekutilia mashaka.
 
Hiyo huwa inatokea usiku wa manane unaisikia inafunguka na asubuh ukiamka unaikuta iko wazi.
Na kuna nyingine unasikia nyayo za mtu anatembea nje ya dirisha ukifungua pazia kuchungulia hakuna kitu hii nayo utasemaje?
Sasa ushasema vyumba havitumiki unashangaa nn sasa??ushawah kutoka kutoka na kuangalia LIVE jinsi milango inavyofanya mauzauza??
 
Nijifunza kwamba haukubali uchawi au ushirikina upo kwa sababu hujarogwa wewe. Je hiyo unaona ni sababu ya msingi ya kutowepo uchawi???
Mkuu nitaogopaje kitu ambacho hakina nguvu kama wewe uogope kwa sasa hivi karanga watu wakwambie karanga zinaua
Uchawi ni imani ambayo haiwezi kufanya kazi pasipo na ww kuikubali
Moja ya principle kubwa ya uchawi ni kukubali kuwa upo na una nguvu ya kufanya chochote juu yako ukikubali principle hii umekwisha
Sasa mm siwezi kuogopa kitu ambacho hakinan uwezo
 
Mbona wabunge na mawaziri ni matajiri na wanapishana kwenda kwa waganga kuroga hapo utasemaje?
 
Umeongea points sana ya kujiamini uchawi una principle zake ukizijua huwezi kurogwa
 
Umeongea points sana ya kujiamini uchawi una principle zake ukizijua huwezi kurogwa
hujanielewa vizuri nafikir.
Hakushindwa kukuroga kama angehitaji ila confidence ilikusaidia uonekane hauna lengo baya nao.
Ni sawa sawa unspotembelea kwenye nyumba inayofuga mbwa mkali ukiingia getini yule mbwa huwa hakurupuki kumng'ata mtu from nowhere bali huwa anaisoma saikolojia yako ukienda kwa kujiamini anakuacha anajua wewe ni mgeni salama ila ukienda kwa kubabaika huku unatetemeka atakuona wewe ni mhalifu na kukudhuru.
Ndio sawa sawa na huyo bibi mchawi saikolojia aliyoitumia ila hao wenzako wa mtaani walikuwa wanashindwa kwenda na kukosa confidence kwa sababu tayari wanajulikana ni wahuni sio watu wazuri.
 
Nimekuelewa sana ila mm navyoamni uchawi hauna nguvu kama hutokubali kuutii wengi wenu mnaabudu uchawi ndio maana mnarogwa
 
ukitaka kujua uchawi upo au haupo nenda vijijini kama usukumani halafu uwaambie wazee kwamba hakuna kitu kinaitwa uchawi na kama kipo kitu kinaitwa uchawi wakuoneshe
Ndio maana nikakuambia uchawi lazima uukubali kwanza kuwa upo na una nguvu ndio utafanya kazi huko usukumani wengi wanaabudu ushirikina that's why uchawi upo na ndio maana wachawi wengi maskini kwakuwa uchawi hauna nguvu kama una nguvu wafanye uchawi waweze kujikwamua na umasikini.

Pili kuwepo uchawi haimanishi kuwa una nguvu kushinda vitu vyote duniani kila kitu kina mipaka yake.

Kama kweli uchawi upo na una nguvu kwanini serikali isingetumia njia rahisi kuwatumia huo uchawi wapinzani wote wafe waende huko kijijini kukusanya wachawi na wawatumie kuwaua wapinzani.

Na hivyo hivyo wapinzani waende huko kijijini kutafuta uchawi na kuwatumia viongozi wote wa CCM wafe
Badala yake hayo yote yanashindikana why unadhani jibu uchawi hauna nguvu
 
Kuna kitu unachanganya kidogo.
Kila kitu kina madhumuni yake na dhumuni la wachawi sio kuleta maendeleo ya nchi.
Kanuni na lengo za wachawi ni kumkomoa ndugu,jirani asifanikiwe kimaisha na kuwachezea usiku basi hiyo ndio furaha yao.
Mchawi wala hawazi kama wewe kujenga nyumba kubwa au kununua gari yeye hana muda huo.
Sasa kutowaloga chadema haiwezi kuwa justification kwamba uchawi haupo,au kukosa maendeleo kwa nchi sio sababu kwamba uchawi haupo.
Na ukizingatia uchawi ni kitu cha siri sasa utaenda kuwaita wapi hao wachawi wakakurogee wakina mbowe
 
Mara ngapi walimu wana lalamika huko kigoma kufanyiwa vitendo vya kishirikina kama kujikuta wame lala nje , kuchapwa viboko na matukio mengi ya ajabu ajabu
Mwenyewe nimeckia ila kumbe nyuma ya pazia walimu walikuwa wanatafuta sababu ya kupewa uhamisho waende maeneo ya mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…