Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Yote sawa tu hakuna asiejua yote na pia hakuna pia anaejua yawezekana ukawa unajua mengi na pia yawezekana pia mm nikawa najua kidogo
OK. Vizuri.

Tuanze na definitions. Uchawi ni nini? Unajuaje huu ni uchawi na huu si uchawi?

Mababu zetu walivyoona teknolojia ambazo hawakuzijua, kama vile radio, au watu wengine kuweza kutabiri kupatwa kwa jua, waliona huo ni uchawi.

Leo tumeelewa sayansi vizuri, tunajua huo si uchawi ni sayansi tu.

Sasa, utajua vipi kwamba kitu unachofikiri ni uchawi wewe leo ni uchawi tu, na hujaghafilika kwa vitu usivyovijua kama hao mababu zetu?
 
Haiwezekan mkuu Kama hujamshika Mungu au huna nguvu zozote Basi utateswa Sana
Hakika mkuu ila mbali na mambo ya Mungu kuna spiritual world ambayo inahama kidogo na haya mambo ya dini ila iko na nguvu zaidi ya uchawi na ndio maana nikasema ni roho ya kijasiri kukabiliana nao mkuu
 
Kwa nini hawajenda church kumsalia?

Huko makanisani panahitaji imani sana kupokea muujiza otherwise utapoteza muda wako bure kule. By the way, Makanisani nako siku hizi hakuaminiki sana. Kuna wanaoponya kiukweli yaani Yesu kaponya au Uchawi unafanyika huko makanisani.
 
Mtu anaweza kuwa jasiri na shupavu kama Amina Chifupa, lakini bado akalogwa tu. Dawa ya kupambana na ushirikina ni kuwa na ulinzi wa Mola. Mengine yote ni misamiati myeusi.
Hakika kubwa boss.....ila swala hili la ujasiri sio ujasiri wa Kua na nguvu ya kupambana na kitu kimwili mkuu ni ujasiri katika mambo ya kiroho
 
Mkuu kuna nyumba huku inapangishwa, huwa watu hawamalizi week wanakimbia.. njoo na roho ya kijasiri mkuu me unipe hela ya udalali tu
Mkuu maji hayapimwi na kidole [emoji28][emoji28]

Mambo mengine ya kujitakia hata Mungu anashindwa kukusaidia ukihitaji msaada wake
 
Hamna uchawi, ni imani yako!
 
Kwa mujibu wa maelezo yako natoa aina mbili za defn
Ya kwanza uchawi ni elimu ambayo mtu hana uelewa juu ya jambo fulani yaan akili yake inashindwa kutambua nini kimefanyika hapa namaanisha misukule mapepo
Ya pili ni uchawi ni sayansi ambayo huwezi prove kuwepo kwake
 
Kwa hiyo mtu anayejua mienendo ya jua na mwezi, akaweza kutabiri jua litapatwa tarehe fulani, huyo ni mchawi?

Unahakikishaje uchawi upo kweli na si hadithi za watu tu zinazotokana na ujinga wao wa kutojua mambo kama sayansi na saikolijia?
 
"lakini hakuna tofauti"… "tofauti ni jinsi…"!!???

Uchawi ni ushetani, nguvu za giza (superstition); miujiza ni utendaji wa Mungu (supernatural work of God). VERY BIG DIFFERENCE. Leo Shetani aliyekutuma lazima akukule nyama.
 
Poor definition. Eti kitu usichojua ndio uchawi???
 
Huko makanisani panahitaji imani sana kupokea muujiza otherwise utapoteza muda wako bure kule. By the way, Makanisani nako siku hizi hakuaminiki sana. Kuna wanaoponya kiukweli yaani Yesu kaponya au Uchawi unafanyika huko makanisani.
But haiondoi ukweli kwamba church ndipo penye solutions. Usichanganye habari wala kudanganywa na Iblis Shetani
 
Ndio maana ccm wakaamua kuongozwa na mshikirina
 
Aisee!??? Hata ungejaribu "kugugo" basi kidogo upanue maarifa yako.
 
Kwa hiyo mtu anayejua mienendo ya jua na mwezi, akaweza kutabiri jua litapatwa tarehe fulani, huyo ni mchawi?

Unahakikishaje uchawi upo kweli na si hadithi za watu tu zinazotokana na ujinga wao wa kutojua mambo kama sayansi na saikolijia?
What is your definition of "uchawi"??? Maana siyo nadharia, hii kitu ni almost beyond reality.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…