Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Uchawi ungekuwepo:-

Wakoloni wasingewanyanyasa Babu zetu kiasi kile mpaka wanaume wanne wakiwa nusu uchi wanambeba mwanaume mmoja wa kizungu juu kuanzia Kigoma mpaka Kilimanjaro

Wasingechapwa mijeledi kiasi kile na waarabu

Wanaume wa kinijeria wasingechukuliwa watumwa na kupelekwa America kutumikishwa wazee wao waangalie tu

Timu za Simba na Yanga zingekuwa club bingwa za dunia

Wachezaji wa kibongo wangechezea Barca, Real Madrid, Liverpool etc

Mwisho kabisa hao wachawi wenyewe wangekuwa ni matajiri wakubwa mno sio wa kuomba kuletewa Kuku mweusi
Labda hao wazungu nao wachawi kuliko mababu zetu!? Who knows!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe wachawi wanaenda majuzi eeh!! Me nilidhani kwa situation Kama hiyo akikukuta anakuua kabsa,Kama ndo hivyo back uchawi ni upuuzi
Ni kweli uchawi ni upuuzi; lakini pia ni nguvu za giza zenye madhara na uharibifu mkubwa na mauti.
 
Hata mm nimekubali kwa unayosema wala sipingi kwangu mm uchawi hauna nguvu wala hauniwezi kwa lolote siwezi kurogwa mpk nife kwa uchawi hiko kitu hakuna kwangu
Ila kwako uchawi upo tena una nguvu na tena una nguvu na unaweza kukuroga ww na ukafa mara moja
Basi tumeelewana, hakuna ubishi tena. Unakubali uchawi ni halisi; ndivyo ninavyoamini pia. Ninachoamini kingine ni kuwa kuna nguvu nyingine kubwa ambayo inatufanya tuwe salama na tuendelee kuwa hai. Ndiyo maana nikasema, mshukuru sana Mungu kwa ulinzi mkubwa alokupatia ili aendelee kukulinda maisha yako na shughuli zako.
 
Tatizo kuamini Katika Mungu hakuondoi wewe kupata majaribio to the fullest extent ya uchawi au ushetani na nguvu zake.

Ref. Ayubu!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Jana usiku nimeota inapiga radi ya kwanza,ya pili...ya tatu nikashtuka usingizi ukakata sikulala mpaka mida ya waislamu
 
hujaelewa,sijasema confidence ilizuia uchawi nilichosema kwamba huyo bibi aliamua kumpotezea kutokana na confidence yake kuonesha hana ubaya.
Kwani kuwa na urafiki na mtoto wa mchawi ni kosa?halafu ukizingatia wote ni watoto tu,akitaka kuthibitisha kama huyo bibi kweli ni mchawi au sio mchawi akishakuwa mkubwa aende kumdhulumu kiwanja au kitu chochote chenye thamani ndio ataona.
Uchawi huwa hautumiki kwa michezo ya kitoto
Hiyo sentensi ya mwisho ondoa, aisee!
 
Kama hivyo vitu havipo basi ujue uchawi hauna nguvu
Uchawi ni imani kama vitu vingine kijana acha kuogopa lakn siwezi kukulazimisha kukubali endelea kuugopa uchawi mm nadunda duniani lkn kuhusu uchawi siwezi kurogwa wala kufa kwa uchawi kwangu mm hiko kitu hakitotokea never
Ila kwako kinaweza kukutokea ila sio lazima ukubali navyosema
Aisee! Una mawazo finyu sana juu ya nguvu za giza, ndiyo maana unabisha sana. Usidhani uchawi lengo lake ufe tu basi. No! Never! Ni pamoja na kifo, inapobidi, lakini ni pale inapokuwa kwenye mpango wa yule mkuu wa giza mwenyewe. Hawa wachawi, wasihiri, walozi, waganga, waaguzi, washirikina na watu wa ndumba ni watumwa na vibaraka tu ambao kazi yao ni kutekeleza maelekezo na masharti ya mkuu wa mapepo. Ukijua hili, basi utakuwa na mwanzo mzuri wa kuelewa. Sasa lengo kuu ni kuzidi kuujenga ufalme wa huyu Iblisi mwasi. Kumbuka kuna nguvu mbili zinapambana duniani -- nguvu ya Mungu na nguvu ya Shetani. Mashetani yatatafuta kila namna ili kukuangamiza pale tu unapokinzana na ufalme wao, unapokuwa tishio kwa maslahi yao, unapokiuka masharti yao kama tayari wewe ni mfuasi, au wanapoona huna tena faida kwao, basi unadhalilishwa kwa fedheha, mwisho wake mauti. Habari imeishia hapo! Wao wana taimu na wale wenye kuwaletea manufaa, na hao ndio wanalindwa na kuhudumiwa na kupewa heshima na uwezo na ushawishi na kadhalika.
 
Mpaka sasa duniani hakuna anaujua uchawi kama upo na unafanya kazi au la habari za uchawi zimekuwa za siri kwakuwa uchawi hauna nguvu yoyote na matokeo ya uchawiuchawi ili uweze kufanya kazi lazima wewe unaerogwa lazima ukubali kuwa uchawi upo na una nguvu usipo kubali haurogeki hata kwa bakora

Kuna safari moja katika maisha yangu nilikuwa na uhusiano na mtoto mmoja mweupe mzuri huyo aisee pale mtaan watu walikuwa wanomuogopa kipindi hiko niko form 4 kwakuwa bibi yake alikuwa eti mchawi

Mh kwa ule uzuri aisee nilisema siwezi kumuacha maana kwanza alinifata mwenywe eti nimfundshe hesabu

Mtaa mzima ulikuwa unamuogopa huyo bibi ila yule bibi nikienda kumuulizia mjukuu wake ananikaribisha tu vzr kwake watu achana na huyo mtoto huyo bibi mchawi atakuroga watu mtaani waninipa ushauri

Mm nikasema uchawi hauna nguvu that's why wachawi wengi maskini hawawezi kujisaidia kupitia huo uchawi

Tukadumu na yule mtoto kwa miaka kama 3 na wala sikurogwa
Ningewasikiliza watu wa mtaani nisingempata
Na haya ndio maneno ya watu kila siku uchawi uchawi ulishawahi kuuona au kuhushudia ?
Na kama umeona umejuaje kama huu ni uchawi?

Ukisoma vizuri hii article yako paragraph ya pili unakili uchawi upo hapo unapo sema" ili ufanye kazi lazima wewe uane rogwa ukubali" ajabu bado una bishi uchawi haupo
 
Jana usiku nimeota inapiga radi ya kwanza,ya pili...ya tatu nikashtuka usingizi ukakata sikulala mpaka mida ya waislamu
Labda hiyo ni ndoto tu ya kawaida. Hakuna haja ya kuhofu lolote kama ukiwa na Mungu. Ndoto zipo tu. Najua pia wakati mwingine ndoto ni ishara ya mambo mbalimbalimbali maishani mwa mtu au watu wengine. But all in all, take it easy!
 
Ukisoma vizuri hii article yako paragraph ya pili unakili uchawi upo hapo unapo sema" ili ufanye kazi lazima wewe uane rogwa ukubali" ajabu bado una bishi uchawi haupo
Amekiri, anakubali kabisa. Ameeleza hapo juu.
 
Mtu unaitwa Iblis Bin Shetan halafu bado unatuambia uchawi haupo. Wewe ni mmoja ya hao wenye kufanya shirki/uchawi.

Na wachawi wote huwa mna tabia ya kukana uwepo wa uchawi kwenye mijadala mbalimbali.
Soma posti zake taratibu, utanielewa, aisee! Hapo mwisho anakiri wazi hii kitu ipo. Tatizo tu anadai yeye hawezi kurogwa. Ameambiwa amshukuru Mungu kwa sababu ndiye amempatia huo ulinzi wa kutowangiwa na washirikina. Hilo jina inabidi sasa afanye mchakato wa kubadili, itakuwa poa. I hope umeelewa!?
 
Mkuu mbona mgumu kuelewa, naona una tatizo la kuelewa vitu kwa haraka inabidi ueleweshwe mara nyingi ili uelewe (kilaza).

Ushaambiwa uchawi unahusisha nguvu za giza wewe unaanza kuleta tena hoja za mapolisi, Duh ipo kazi, Labda utafute mtu mtaekaa nae siku nzima akueleweshe, Mbona wengine wanaelewa fasta tu, wewe siku ya pili hii huelewi tu 😁😁
Twende kwa facts.

Fact 1.

Huja define uchawi ni nini.

Hutakiwi kumshutumu mtu kwamba ni mgumu wa kuelewa, ikiwa hujafanya kitu cha kwanza kabisa cha kumuelewesha.

Hujatoa hata definition ya uchawi, unanishutumu mgumu wa kuelewa.

Wewe si tu hujaelewa, wewe hujui kufikiri.
 
Soma posti zake taratibu, utanielewa, aisee! Hapo mwisho anakiri wazi hii kitu ipo. Tatizo tu anadai yeye hawezi kurogwa. Ameambiwa amshukuru Mungu kwa sababu ndiye amempatia huo ulinzi wa kutowangiwa na washirikina. Hilo jina inabidi sasa afanye mchakato wa kubadili, itakuwa poa. I hope umeelewa!?
Nimekuelewa Mkuu.Na kwakweli hilo jina alibadili maana lina walakini.
 
Hizo ni imani tu na wenge lenu usiku

Hakuna kitu kama hicho (uchawi) uyo mtoto aliyekuwa kipofu, kiziwi nk apelekwe hospitali utapewa chanzo na nini kifanyike
Hawa wanao pinga vikali hua ndio wahusika wakuu,sa'bu maranyingi watu wanao jihusisha na mambo haya huwezi kawa zania kbs hua ni wacha Mungu sana na ktk ibada never miss,iweje ww ubishe wkt mtu ame simulia yalio mkuta...na hum pia mpoo tuu 😀😀😀
 
Mpaka umeselect Nigeria manake kua unasadiki wao ni magwiji wa hizo kazi
Hapana inaaminika kuwa wao ni wachawi zaidi barani Africa, kama inavyosadikiwa ni kweli wangekuwa mbali sana katika dunia hii
 
Back
Top Bottom