TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,747
Anna Mghwira,
Lakini pamoja kukubaliana na hii hoja tunatakiwa kutafakari kua ni kwanini wenzetuwalikua wanakimbilia kusaini?
Ni opportunities walizokuwa wanazinyemelea kwetu? Na je, kwa sasa wamerudi nyuma kwakua wenye shamba la bibi sasa wameshtuka?
Hahaa, kama tulikuwa tunafikiri pamoja vile.Mkuu unataka UM_PM
Thank you m'lady.Leo wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali, Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.
Uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii. Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.
Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.
Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi nyingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii.
Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii, wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara.
Ndalama sijakuelewa kama unahoji hoja yangu au lugha niliyotumia!Wanarudia kuutizama? Au wanawasubiri wasiosaini kwa vile ni mkataba kati ya union na union na sio single countries?
luka 10:17-20Furaha uliyo nayo inanikumbusha ile habari ya kwenye Luka 10:
Ndipo wale sabini walipo rudi kwa furaha wakisema, 'Bwana, kwa jina lako hata pepo wanatutii?
Bwana akawaambia, 'Nalimwona Shetani akianguka kama mwanga wa radi toka Mbinguni'... Lakini basi, msifurahi kwa vile pepo wanavyo watii bali kwa kuwa majina yenu yameandikwa Mbinguni....
Kwa sie tulioanza kufuatilia suala la EPA zaidi ya miaka 5 iliyopita inakera sana tena sana kusikia eti "...hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu!" Mtu mwingine anaweza kudhani suala la EPA ni jambo jipya kumbe lina miaka na miaka sasa!! Ina maana hadi leo Waheshimiwa wetu walikuwa hawafanya tathminini kufahamu faida na hasara za EPA?! Nilitarajia kwa ile jana iwe ni YES au NO, PERIOD... kumbe bado tunatafakari kufahamu pros and cons!!!!
Mkataba wa EPA ni mzuri lakini unaonekana ni mbaya na YES, kwetu ni mbaya au hauna manufaa si kwa sababu EPA as EPA ni mbaya bali ni sisi wenyewe ndio tuna akili mbaya! Tusingekuwa na akili mbaya EPA ingekuwa ni opportunity! We have a lot to sell to EU but we don't know which among them! A country like Tanzania with abundant and virgin land ni kufuru kwa Mwenyezi Mungu hadi leo tunalilia kwamba sisi hatuna cha kuuza EU... community iliyojaa junk and inorganic produces everywhere wakati sisi tukiwa na uwezo na kuzalisha organic produces at minimal cost ambazo ni valuable anywhere na kuweza kulisha the whole of EU!!! Hapa napo Watendaji wa Serikali watalia lia kwamba ni ngumu ku-compete na European Farmers kwa sababu wanapewa subsidize... so why don't you offer the same kwa wakulima wenu?!
No ni Economic Partnership Agreement: Makubaliano ya Kiuchumi.
Kuna madai hayo kuwa mkataba umelenga sana maua ya Kenya, ambayo ukichunguza pia ni maua ya Tanzania kwa sababu mengi yanasafirishiwa Kenya na wakati mwingne yananunuliwa na wachuuzi wa Kenya ndipo yasafirishwe Ulaya. Ni hivi kwa bidhaa zingine za mboga mboga, vitunguu, ufuta na bidhaa zingine tunazouziana na Kenya.Lakini hao wanaouza huko Ulaya ni wazungu wakenya wenye connections.
Mwafrika hapati kitu hapo.
Katika hili sitegemei watakuwa wameona kwa niaba ya raia wao ama kwa niaba yao wenyewe. Mikataba ya Kenya inawanufaisha wawekezaji wa Ulaya zaidi ya Wakenya.Kama Uhuru Kenyatta na Paul Kagame wamesaini basi huo mkataba utakuwa uko vizuri tu make hao wawili ndo marais wenye bongo safi na zinazochemka ukanda huu.
Hajakataa kusaini, amesitisha kusaini wakati huu mpaka aridhishwe na maudhui ya mkataba.Kwa Rais wa Tanzania kukataa kusaini mkataba wa EPA anastahili pongezi
EPA ni Mkataba mmoja. Mibovu mingine nayo iekwe. Hata hivyo EPA mkataba ndio ulikuwa unakwenda kuwekwa sahihi, haujakamilika bado. Naona tunachanganya mada. Huu mkataba ndio ungesainiwa kwa mara ya kwanza.Yaani nchi zingine ziifuate Tanzania wakati Tanzania inaongoza kwa kuingia mikataba mibovu?
Hili suala linatakiwa kutuleta pamoja na kupunguza tofauti za Kisiasa.uchumi unatakiwa kuwa juu ya siasa.
Pale tume fanya maamuzi kama wana Africa mashariki. Hata kama TZ ilisha jiridhisha kuhusu Epa. Ni lazima turudi nyuma tujiridhishe pamoja kama wana EAC.Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi?
Kama hakuna faida kwanini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla?
Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?