Nimehudhuria ndoa ya single maza, pilau tamuuuuuu

Nimehudhuria ndoa ya single maza, pilau tamuuuuuu

Guys, yaan hapa nimeshiba kitumbo kipo ndi ndi ndi, pilau la harusi ya single maza lilikua tamu hatariii, pilau la mbuzi likatiwa zabibu kavu na tui la nazi kwa mbali oyaaaaaaaa🙌🏻 rosti la mbuzi na nyama za kuku za kuokwa nyie watu wanajua kupika, 😋😋

Sasa nawapa ubuyu kidogo wa huyu single maza aloolewa leo, huyu alizalia nyumbani mwanaume akaingia mitini, hakukata tamaa akaingia mtaani kupambania ugali wa mwanae, kuna mpemba mmoja yupo Germany akaleta salamu kwa wazazi wake anataka mke, wazazi wakamchagua mdogo wake na huyu dada, sijui ilikuaje kuna mtu akamtonya bwana wa Germany kua dada mtu ni kisu zaidi ila ana mtoto, jamaa kaomba picha akadata, akawastopisha wazazi wake akasema anakuja mwenyewe, na kweli akaja akakutana na huyu single mother hajachelewesha ndoa ikapita chaaaaap, hapa single mother na mwanae safari hiyoooooo ya Germany, 🥳🥳🥳🥳

Basi bwana, baada ya kushiba zangu pilau nikajilaza kwenye zulia huku nachokonoa chokonoa meno si ndio napokea meseji eti mualiko wa kitchen party ya single maza mwengine, nikajisemea "aah jamani kwani kuna mashindanoooo," ila huyu bwana wa huyu single maza wa pili kibokoo alivyomvesha pete ya uchumba akamnunulia gari atembee amekaa na sasa ameamua kumuweka ndani jumla, single maza oyeeeeeeeeeeeeeee!

Sasa kuna matahira kila kukicha single maza this, single maza that, wajanja wanaoa,

FAIDA ZA KUOA SINGLE MAZA:
1. Unaoa mwanamke aliyepevuka kimwili na kiakili
2. unaoa mwanamke ambaye una uhakika hana changamoto ya uzazi yaani wewe ukiweka tu imooooo
3. Unaoa mwanamke aliyeamua kwa dhati kusettle down
4. Unapata uzoefu mapema wa kuishi kifamilia, yaani baba, mama na mtoto kabla hamjaanza kuongeza wengine
5. Wanajua mapenzi na mahaba, wasafi sana
6. Ongezeeni zingine nimechoka kuandika

Ngoja niende kwa wapishi waniwekee pilau kwenye kihotpot ninywee chai kesho,
Tchaooooo
Nakubaliana na wewe hususan kama ni asubuhi hadi saa 6. Baada ya saa 6 majanga yanaanza na kufika saa 12 mnaachana sababu kubwa ni huyo mtoto wa kufikia
 
Muoaji nae nyegeboy tu, imagine unawaomba wazazi wakutafutie mke wametafuta wakapata gafla unatumiwa picha ya mwanamke mwingine unabadili gia angani.

Mtaji wa single mother ni wanaume dhaifu, wanaume wasio na option na wageni wa mambo ya mahusiano....chunguza popote select wanaume watano waliooa single mother.
 
1. Nikisema ndoa zinafungwa namaaninisha ndoa zote, hao wasiokuwa na tatizo na SM ni wanaume au sio wanaume? Ndoa ya mke wa pili ni ndoa ama sio ndoa?
2. Ukisema single mothers ni wengi mtaani maana yake na single fathers wapo pia au wao wanawake wanazaa na wanawake wenzao? Kama ninavyomuona single mother ni mwanamke kama wanawake wengine ndivyo hivyo hivyo nawaona single fathers ni wanaume kama wanaume wengine. Unaposema 'labda waislamu' , 'labda aolewe na single father' unamaamisha wao ni mabaki ya wanaume au unamaanishaje?
3. Mwanaume asiye na akili hata yeye akiwa na mtoto bado atataka kuoa asiye na mtoto. Yaani kwao tatizo la single parenting lipo kwa wanawake tu.
Single father huwa hawathiri kama vile single mother maana uchungu wa mtoto anao mama zaidi kuliko baba na Ndio maana tunahasa mwanadada asizae na mwanaume ambaye hajaolewa nae tukifumbia hili maana yake tutazidi kuzalisha single mothers wengi zaidi
 
Muoaji nae nyegeboy tu, imagine unawaomba wazazi wakutafutie mke wametafuta wakapata gafla unatumiwa picha ya mwanamke mwingine unabadili gia angani.

Mtaji wa single mother ni wanaume dhaifu, wanaume wasio na option na wageni wa mambo ya mahusiano....chunguza popote select wanaume watano waliooa single mother.
Naunga mkono hoja yako
 
😀
Wapo ambao walizinguliwa na wanaume ndoani na kuachana lakini wao ni wema...

Wapo ambao walizaa tu kwa nia ya kupata watoto na ha2a time na baba watoto...

Wapo ambao wamepata watoto kwa mazingira kama kubakwa, mimba zisizotarajiwa...
Mwanamke aliye achwa na mwanaume huyo ni wa kuogopwa kama ukoma
 
Mafanikio makubwa sana hayo , tushangilie kwa pamoja🍻
Screenshot_2026-06-12_190228.jpg
 
Kila mwanamke ana mtu wake, ukiona mwanamke ameshindana na mtu, ujue huyo sio mtu wake kuna namna walijaribu ku force mambo. Hakuna mambo ya tamaa sijui umalaya, issue ni kwamba anakutana na mtu wrong siku akija kutana na mtu wake ( type yake ) anatulia fresh huwezi ona heka heka zozote ingawa haina accuracy ya 100% ila kwa sehemu kubwa watu hawana compactbility kwenye mahusiano yao
Hivi dating pool yenye watu milioni 30+ umpate huyo mtu wako unafikiri ni rahisi rahisi. Acheni kudanganywa na tamthilia. Mwenza wako lazima awe na mapungufu, na ndipo unakuja wajibu wa kila mmoja kumfanya mwenzake awe mtu bora zaidi.
 
Kuna wakati kuwa "mjanja" ndio huwa Ujinga wenyewe.

Bila kuingilia Uhuru wa mtu kimaamuzi BUT Mwanaume kuoa mwanamke mwenye mtoto sio jambo jema sana.

SIWALAZIMISHI, ila vijana wenzangu kama mkiweza OENI wanawake ambao hawana watoto.
Na mwanamke akishakupa sifa nzuri nzuri ujue ni kinyume chake. Anakujaza upepo akutumie kimasilahi. Kudhiirisha ilo huo ujanja wa kuoa single mother hawezi kuufurahia ukifanywa na kaka ake asiekua na mtoto
 
Hivi dating pool yenye watu milioni 30+ umpate huyo mtu wako unafikiri ni rahisi rahisi. Acheni kudanganywa na tamthilia. Mwenza wako lazima awe na mapungufu, na ndipo unakuja wajibu wa kila mmoja kumfanya mwenzake awe mtu bora zaidi.
kufanana haiondoi udhaifu, maana hakuna mkamilifu ili kuna kubebeana udhaifu kwa moyo safi na maisha yanaenda
 
Back
Top Bottom