Nimeiba ama ndo zali la mentali

Mrudishie pesa yake mkuu Kumbuka wengi ni waajiriwa mwisho wa siku boss wake akipiga hesabu akakuta hiyo hasara atamkata kwenye mshahara wake hapo ukute kijana/binti wa watu ndo anategemea mshahara wake wa laki mbili awatumie wazazi wake kijijini
Inafikirisha mkuu. Ila pesa itarudi kwa mhusika
 
Hao mawakala mishahara yao haizidi laki 2, nadra kukuta analipwa zaidi ya hiyo na boss wake.

Jikaze kiume umrudishie tu ili kunusuru mshahara wake wa lak na nusu. Mimi niliwahi kurejesha laki ya wakala, binti alizidisha na alikuwa mgeni hapo ofisin.
 
Hautakuwa wizi mpka pale utakapoamua kuto mrudishia wakala kiasi ambacho si cha kwako.
 
Hao mawakala mishahara yao haizidi laki 2, nadra kukuta analipwa zaidi ya hiyo na boss wake.

Jikaze kiume umrudishie tu ili kunusuru mshahara wake wa lak na nusu. Mimi niliwahi kurejesha laki ya wakala, binti alizidisha na alikuwa mgeni hapo ofisin.
Umeeleweka vzr ndugu.
 
Wakala aliwahi kunizidishia 512,000/=, Mimi nilipofika ofisini baada ya kumaliza hesabu zangu nikajikuta Nina zidi ya 512,000 nikajua tu ni wakala kajichanganya nikaiweka kwenye bahasha.alivyokua anafunga hesabu zake usiku Akakuta ana short ya 512,000/= akanipigia simu saa nne usiku anaongea sauti haitoki vizuri πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ" dada samahani eti Kuna hela ilizidi kwenye hela niliyokupa"?.Nikamuambia tu nitakuletea asubuhi, nilitamkiwa baraka siku hiyoπŸ˜ƒπŸ˜ƒ nilivyompelekea hakuamini.
 
Huu ni wizi, rudisha fedha za watu.
Huu sio wizi,bali ni makosa ya mhudumu wa miamala.

Sasa cha msingi ni kuwa na utu tu,hiyo pesa arudishe,kuna amani ya moto itapatikana baada ya kurudisha.

Yaani hata asiwaze eti hatajua,sawa yawezekana asijue kama ni mzembe ila uaminifu ni kitu kizuri hata kama hakuna anayekuona ukifanya uaminifu.
 
Hongera mammy. Ulionesha uungwana. Me pia nlipompatia ela ake hakuamini. Alinipa 10k, nikamwambia hana haja ya kunipa hio yote. Alitulia kwa dk kama 10 akatoka na kurudi na nyama choma kama kilo hv. Akaomba nisiisusie. Tukakaa tukala hadi ikaisha. Tukabadlshana namba na akawa rafk angup
 
Pesa ilirudi mkuu. Nlimwendea mida ya saa tatu usiku nikamwambia nahtaj kufanya muamala wa laki 1. Akaniruhusu. Nikaona huyu hana kumbukumbu. Ikabidi nimwombe atoke nje tuongee. Nikaomba anioneshe mesej za miamala ya jana, akagoma akiwa na wasiwasi mwingi. Ikabid nifunguke tu. Alitoa chozi akaniita BRO.

Nlikula nyama wazee... sahv tunawasiliana as brothers.
 

Nice[emoji106]
 
Safi sanaa!

Uaminifu unalipa,Ile amani ya moyo baada ya kurudisha inakupa kujiamini nafsi yako kwenye hili.

Natamani CCM wawe hivi waaminifu tungefika mbali kama nchi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…