Nimeibiwa takribani laki 5 na Binti wa duka langu jipya ndani ya miezi miwili. Nichukue uamuzi gani?

Yaani unamkabodhi fisi bicha, na bado unamuachia bucha baada ya kuona mali imeliwa...
 
Mtoee weka mwingine tafuta mchaga hutojutia unaibiwa ila faida unaiona make sure unamtoa kijijini fresh awe anajieleewa. Ummri. Miiaka 18__23
 
Nimepata wazo kwamba afanye kazi miezi minne hapa kila siku awe anachukua elf 2 tu hakuna mshahara.
1. Hapa sasa unataka kujipalia mkaa ndugu yangu. Kama kweli ni binti mzuri anayejua biashara na huna namna ya kupata mbadala wake, ni afadhali uwe unamkata Tsh 50,000 kila mwezi kwa muda wa miezi 10 urudishe pesa zako. Naye atakuwa amejifunza kutolaghaiwa na huyo mpenzi wake mandazi anayemfuata hadi kazini.

2. Mpige marufuku huyo mhuni wake anayekuja kumghasi hapo kazini. Kama hatasikia, siku ukimkuta hapo dukani mpe mboko za kutosha hadi liwe fundisho kwake na kwa mpenzi wake.

3. Hata usipomuambia mama mdogo siri itafichuka tu baada ya mapato yake kupungua. Unless amuombe huyo mhuni wake amsaidie kumlipia maana ndiye aliyekuja kumharibu kwa kumpa mbinu za wizi.

Ni hayo tu.
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, kwangu nimeona ni uduanzi tu, nataka nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke anaumia kwa sex)

Mnaweza kunipa mawazo mbadala ama ya ziada wakuu niweze kudeal nae vizuri.
Sema mishahara midogo ndo inafanya mtu uwe mwizi
 
kumbee ameleta mrejesho wa UPUUZI TULIOMKATAZAA KWA NGUVU ZOTE 😀 😀 😀 😀 binti kafanya jambo jemaa sanaa abarikiwee tena kaiba pafupi mnooo ilibdi apige MILION PLUS
huyo yupo kwenye kioski nilichomfunguliaga dogo wa form 4, sio duka langu nalozungumzia
 
sky soldier
Nisikilize kama una sikio ls kiume.
Huyo binti usimzuru chochote.

1. Watu wazuri hutengenezwa
2. Mpe nafasi nyingine tena kwa masharti kuwa umkate mshahara 40k kila mwezi.
3. Mpe utaratibu mpya wa rekodi na ulio wazi zaidi.
4. Huenda alijikopesha au hayuko makini katika kurudisha chenji au vinginevyo...lakini sasa amegundua uko makini naye atamakinika hutaamini.

5. Wanadamu wotr huwa tunakosea
TAFADHALI MPE NAFASI NYINGINE

WEWE HUJUI BIASHARA YOYOTE.

NANI ALIYEKUAMBIA KUWA MWIZI ANAPEWA NAFASI YA 2 NA UMKATE HELA?

UTAPIGWA DOUBLE DOUBLE KUSHOTO NA KULIA

KWA USHAURI HUU INAONYESHA KUWA WEWE HUNA BIASHARA UNAYOMILIKI

UKISHAIIBIWA HAKUNA MBADALA ZAIDI YA KUFUKUZA ILI ULETE MGENI KABLA HAJAZOEA UNAKUWA USHAMAKI MADHAIFU
 
Sisi huwa tuna utaratibu mmoja ukileta hasara tena ya makusudi kama hiyo nakukata mshahara mpaka umalize deni,unaweza pia kusamehe na kufukuza
Tunakubalina na barua ya onyo
 
1. Hapa sasa unataka kujipalia mkaa ndugu yangu. Kama kweli ni binti mzuri anayejua biashara na huna namna ya kupata mbadala wake, ni afadhali uwe unamkata Tsh 50,000 kila mwezi kwa muda wa miezi 10 urudishe pesa zako. Naye atakuwa amejifunza kutolaghaiwa na huyo mpenzi wake mandazi anayemfuata hadi kazini.

2. Mpige marufuku huyo mhuni wake anayekuja kumghasi hapo kazini. Kama hatasikia, siku ukimkuta hapo dukani mpe mboko za kutosha hadi liwe fundisho kwake na kwa mpenzi wake.

3. Hata usipomuambia mama mdogo siri itafichuka tu baada ya mapato yake kupungua. Unless amuombe huyo mhuni wake amsaidie kumlipia maana ndiye aliyekuja kumharibu kwa kumpa mbinu za wizi.

Ni hayo tu.
Ushauri mzuri sana,
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, kwangu nimeona ni uduanzi tu, nataka nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke anaumia kwa sex)

Nimepata wazo kwamba afanye kazi miezi minne hapa kila siku awe anachukua elf 2 tu hakuna mshahara.

Mnaweza kunipa mawazo mbadala ama ya ziada wakuu niweze kudeal nae vizuri.
Ukimwacha afanye kazi bila mshahara ataendelea kukuibia kufidia gepu kwenye mapato yake. Jingine la kufikirisha ni biashara gani unafanya ya bidhaa za kwenye box ambayo mauzo yake yanakusanywa kwenye droo ndani kusubiri kupelekwa bank? Hapo si kitoa pesa kwenye mzunguko? Au ndo kuendesha biashara ki-TRA TRA?
 
Yaani ngozi nyeusi sijui tuna shida gani mtu unamlipa vizuri,kula juu yako ila afikilii biashara anawaza jinsi gani akupige.Mimi kuna mmoja nilimuweka police kwa week maana alinipa hasara kubwa 😬
 
UKITAFUTA MWINGINE UKAMUWEKA HAPO HATA KAMA NI NDUGU ATAKUIBIAA TU...!! either ukae wew au akae mkeo lasivyoo biashara bila kusimamia kwa karibu Andaa maumivuu utakuwa unatoa hela kwenye mshahara unaiweka dukani inaliwaaa hasa biashara ya duka ni hatari maana huwezi kufanya stock kila siku kama una mzigo mkubwa.
Hata mke anaweza kuwa mwizi
 
WEWE HUJUI BIASHARA YOYOTE.

NANI ALIYEKUAMBIA KUWA MWIZI ANAPEWA NAFASI YA 2 NA UMKATE HELA?

UTAPIGWA DOUBLE DOUBLE KUSHOTO NA KULIA

KWA USHAURI HUU INAONYESHA KUWA WEWE HUNA BIASHARA UNAYOMILIKI

UKISHAIIBIWA HAKUNA MBADALA ZAIDI YA KUFUKUZA ILI ULETE MGENI KABLA HAJAZOEA UNAKUWA USHAMAKI MADHAIFU
Alete mpya ili aanze kuibiwaa upyaaa... yani huyu akomae na huyu wa zamani ila amfatiilie kwa ukaribu sanaa
 
Yaani ngozi nyeusi sijui tuna shida gani mtu unamlipa vizuri,kula juu yako ila afikilii biashara anawaza jinsi gani akupige.Mimi kuna mmoja nilimuweka police kwa week maana alinipa hasara kubwa 😬
Ni asili yetu mama .... Kuanzia ngazi za juu hadi ngazi za kifamilia
 
Alete mpya ili aanze kuibiwaa upyaaa... yani huyu akomae na huyu wa zamani ila amfatiilie kwa ukaribu sanaa

mzee hivi unafanya biashara au umeajiriwa? na kama una biashara nahisi ni ndogo tu, ww uinvest zaidi ya 20 million ya kusotea na mkopo mtu anakuiibia almost half a million unasema umoe second chance????

Tabia haichi Asili.

Mtu akiiba hapaswi kupewa nafasi nyingine,

Huwa tunaweka mpya anakaa miezi 6 anakuja mwingine,kabla hajazoea mazingira anaondolewa.

Huo ushauri wako ni batili.Na usithubutu kuufata siku ukifungua biashara ya mamillioni
 
Back
Top Bottom