Nimeibiwa takribani laki 5 na Binti wa duka langu jipya ndani ya miezi miwili. Nichukue uamuzi gani?

Nimeibiwa takribani laki 5 na Binti wa duka langu jipya ndani ya miezi miwili. Nichukue uamuzi gani?

Kwa mshahara wa sh 6000 per day ni haki yako kuibiwa...Tanzania tulitakiwa tuwe na mfumo wa kulipana kwa masaa ambayo mtu amefanya kazi...kiwango cha chini kingekuwa sh 2000 kwa saa
Malipo ya mmfanyakazi zinaingia kwenye cost of production. Kama haingizi 2,000 Kwa siku minus other costs unamlipaje hiyo kwa saa?
 
Usisite kumwambia mdhamini wake eti anaogopa, kabla hujachukua uamuzi wa kumfanyisha kazi kufidia hasara alizokutia,
Waambie kwa uwazi kila kitu na yeye akiwepo ila uwazuie easimpe adhabu au kumdhlilisha ili aamini uwepo wako na staha zako ndizo zimetumika kumstiri,
Ukifanya siri ukampa adhabu hata akija hapa jf kulalamika hujampa mshaala wake, sisi tutakuponda umedhurumu binti wa watu,
Kila la kheri ktk maamuzi yako
 
Hata siku Moja usiamini mwanamke Kwa asilimia 100... Utakuja kulia
Jamaa mi nna mke na namuamini anasimamia ujenzi Dar mi nipo Dodoma memwambia akipiga kajipiga mwenyewe.

Na ana biashara yake namsapoti inaenda poa tu 🙂🙂🙂😄😄
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke anaumia kwa sex)

Ushauri nilioupata na naenelea kupoke.

Auz kashauri vizuri nisimwambie mama yake kwa makubalioano kwamba aendelee kufanya kazi kwa kumkata elf 50 ya mshahara hadi deni liishe, ila pia niongeze ufatiliaji, pia nae Glenn katoa ushauri unaolingana

rikiboy kashauri kwamba alipishwe deni atajifunza, hata speed ya kuiba atapunguza ila nikisema nimfukuze nilete mwingine ntaanza upya kuibiwa, bora mwizi uliewahi kumshika inakuwa rahisi kumcontrol

Nshomile wa Muleba nae kagusia kwamba wahindi wakikudaka hawasamei, unapelekwa polisi utakaa ndani hadi ndugu warejeshe kiasi ulichoiba, funzo hapa ni kurejesha deni ila nimeona urejeshaji wa deni uwe wa kukatwa mshahara sio polisi.
Kama ameomba msamaha, muache aendelee na kazi lakini mwambie aachane na tabia hizo mbovu na watu wote wanaomshauri uovu aachane naye.

Kumpa nafasi ya pili ndio ubinadamu,kikubwa hakikisha unakuwa makini sana kama kuchukua pesa ya mauzo ya kila siku na kukagua mahesabu kila siku ili isije siku akakupiga na kitu kizito zaidi.

Ubinadamu ni mapungufu, na tunafanya uovu sana, kikubwa ni kama amekiri, ni kumsamehe na kumpa nafasi ya pili, huku ukifanya "close surveillance".
 
Nuzu
Wewe ni binti makini lkn hapa sikuungi mkono.

Watu wengi wanatia hasara sio kwa kuiba bali kukosa uzoefu na umakini.
Kuingiza hasara dukani ni sekunde tu.

Huenda hajaiba isipokuwa kukosa umakini, apewe nafasi na asimamiwe
Hasara ya laki tano mkuu ?kama hana umakini mpaka inatokea hasara kubwa kiasi hiki basi hastahili kukaa dukani.
 
mzee hivi unafanya biashara au umeajiriwa? na kama una biashara nahisi ni ndogo tu, ww uinvest zaidi ya 20 million ya kusotea na mkopo mtu anakuiibia almost half a million unasema umoe second chance????

Tabia haichi Asili.

Mtu akiiba hapaswi kupewa nafasi nyingine,

Huwa tunaweka mpya anakaa miezi 6 anakuja mwingine,kabla hajazoea mazingira anaondolewa.

Huo ushauri wako ni batili.Na usithubutu kuufata siku ukifungua biashara ya mamillioni
Kijana shamba boy anayemsaidia bosi mmoja wa serikali kutunza kuku wa mayai juzi kati alimkamata kijana wake ready handed akimuibia chakula cha kuku. Baada ya mahojiano ya hapa na pale, kijana akakiri kosa na kuahidi kukatwa pesa kufidia hasara aliyosababisha. Kwa kweli kijana huyu ni mchapakazi na ametoka naye mbali sana....na wakati mwigine hata humpa bosi ushauri wa kibishara.

Basi wakawa wameelewana na hadi sasa kijana yupo anachapa kazi kama kawaida. Unajua wakati mwingine hawa wasaidizi huingiwa na shetani, tamaa au hupata ushauri mbovu kutoka kwa watu waovu. Lakini ukimpa second chance anaweza akawa makini na kufanya vizuri zaidi. Hawezi akakuibia tena kibwege kwa kuwa anafahamu umeishang'amua mbinu zake za wizi.
 
usimfukuze kazi mkuu ni demu wangu huyo ukimfukuza mi nitaishije? hapo ndo sehem pekee ninayo itegemea
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke anaumia kwa sex)

Ushauri nilioupata na naenelea kupokea

Hadi sasa nimeshauriwa na wanajamii forums hawa na nikiri nimenufaika na mawazo yao, rikiboy Auz Nshomile wa Muleba Glenn wameshauri kwamba arejeshe deni na si kuondoka sawa na kumsamehe, Binti atabaki kwa makubaliano kwamba simwambii mama yake ila ntakuwa namkata mshahara elf 50 kila mwezi, nikisema nimfukuze nilete mwingine ntaanza upya kuibiwa, bora shetani unaemjua kuliko malaika usiemfahamu, na hii ndio mbinu inayotumika hata na wahindi japo lengo ni moja kurejesha pesa ila mbinu yao ni ya tofauti wanakupeleka polisi utakaa huko hadi ndugu zako warejeshe hasara uliyosababisha. ushauri 1 ushauri 2 ushauri 3 ushauri 4 ushauri 5
Wewe kweli zwazwa yaani vilaki vitano ndiyo unavifingulia uzi. Sisi tunaowapa wanawake wetu 1m ya kuendea saloon au tunawahonga range rover vogue ya 400m mbona hatupigi kelele
 
Bora ya wewe laki 500,000 Mimi nina biashara na wife ,tumemuweka shemeji yangu,utaratibu wa urejeshaji wa pesa unafahamika na kuna akaunti ya nmb tulimpa kwa ajiri ya kuingiza pesa ya mauzo.

Biashara ipo nje ya mji ,mda wa masaa mawili kufika huko toka tulipo.
Kwa mda wa mwezi mmoja kama na nusu hivi amekuwa akisumbua sana kuingiza pesa kwenye akaunti ila mauzo yanaendelea na baadhi ya bidhaa kupungua sana .

Madai yake biashara anauza ila anahisi kuna chuma ulete,yaani anaibiwa pesa kichawi.
Na kuna watu amewakopesha bila kujua ni kina nani,yaani ameshawishika kukopesha watu kisha kawasahau hata detail hakuandika.

Nikaamua kwenda kufunga duka mwenyewe kwa hasira.Nashangaa usiku wa siku niliyo funga kijana anaandika meseji kwa dada yake kuwa mimi nilikuwa naenda dukani nachukua hela na hivyo kupunguza uwekaji wa pesa kwenye akaunti ya biashara.
Jumla ya pesa ni 750,000 nilizochukua na hasara kwa ujumla ni 1,400,000.

Kwa hiyo ikawa mzozo pesa imepotea dukani kichawi na na mimi nimechukua pesa kwa duka bila taarifa(kitu ambacho si kweli).kumbuka biashara ni ya pamoja.

Yule kijana tumemfukuza ila nimebaki na risik ya kulipa hela alizodai alinipa mimi mkononi .

Vijana niwapumbavu sana ,nimemwambia wife kama hanielewi kuwa sikuenda kuchukua pesa dukani basi na mimi sielewi kama mdogo wake kaibiwa kichawi pesa dukani.ninapo lipa mimi hiyo laki 7 na nusu na yeye alipe hiyo hasara ya mdogo wake over.

Nimepeleleza nikaambiwa dogo alisha kuwa kit*0 mbi mzuri sana maeneo hayo na mhongaji mzuri tu.

Nilicho uzika zaidi si kupoteza pesa tu,ila kusingizia kuwa shemeji alikuja kuchukua pesa 750000[emoji849] harafu namuuliza aseme ukweli kama nilienda kuchukua anakubali kuwa ni kweli na nilikuwa nimelewa eti mida ya saa moja jioni .
Mi natumia masanga ila si kwa kiwango cha kulewa niende sehemu umbali wa msaa mawili kufika nishindwe kuelewa[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kwamba ana soma vitabu vya dini ina bidi uki mdaka na boyfriend yake uwa bananishe wote
 
Kumfukuza ni rahisi hata kwake, ishu ni kwamba huo wizi unafidiwaje ?

So unaona suluhisho afanye kazi miezi minne bila mshahara sio?
Anaweza kukubali ila nakuhakikishia mwezi wa mwisho utapigwa million na zaidi!!
 
Back
Top Bottom