Nimeibiwa vitu vyote vya ndani

Nimeibiwa vitu vyote vya ndani

Pole sana Mkuu.
Piga maombi Mungu atazungumza nao tuu... au kama vipi tafuta mtaalamu haswa awaguse kidogo tuu watembee barabarani yakijikojolea.
Au yakilala yakose usingizi kazi iwe ni kujikuna hadi asubuhi
Au awaoteshe vijipu mwili mzima...
Mpaka kwenye viganja vya mkono washindwe kula..
 
Habari wana jamvi


Naandika nikiwa na jazba na hawa watu wanaoitwa wezi. Nimepanga geto langu nikajibana nikaeka vitu vyote vya ndani sasa hawa jamaa wamenilia time nimetoka wamenisafisha hadi kijiko ila kwenye vitu walivoiba wamebeba hadi king'amuzi

Ila kuna mdau aliyeniambia king'amuzi kinatafutika kama ilivyo kwa simu.

Msaada jamani kwa mwenye ujuzi maana nikimpata mwenye king'amuzi ndio nitamtolea uvivu.

Nawasilisha
Dah kwa huu usawa ulivyo then bado kuna wapuuzi wanakurudisha nyuma,pole sana mkuu,hawa wezi ni hatari kwa maendeleo yetu.

Nakumbuka nikiwa Iringa niliwahi kuibiwa kama wewe hivyo,sikua na namna zaidi ya kumpigia jamaa mmoja Mtaalamu/Fundi,akaniuliza kama wamebakiza kitu chochote kile pale geto. Nikamwambia yeah lipo lile karatasi la godoro,Fundi akasema hilo hilo litatumika.

Mpaka leo sijui alichowafanya b'coz walinitafuta wenyewe tena katika simu wakitaka kurudisha vitu vyangu,wakati huo mimi niko Dodoma.
 
Acha hizo mkuu, wezi wapo kila kona
Wezi wapo ila hii habari ya watu kubeba hadi vijiko huwa inatokea maeneo flani flani sasa kama mji wa kijanja kama Moshi una mambo hayo sijui.Au kuna demu wako kaamu kubeba vitu ahame navyo maana hali ni tete.
 
Nenda kwa mganga, wavimbishe matumbo mpaka wavitapike.
Naunga mkono hoja. Wezi wanaudhi wanakera saana.

Niliibiwa laptop ya kazini nikiwa home kupitia dirishani. Simple nikaenda riport wanipe loss report wee naambiwa hiyo inaweza kua nimecheza deal maana ni mali ya umma. Ishu ilikua nzito kuliko nilivodhani.

Baada ya week narudi home nakuta kuna mwizi anapigwa kachakaa karibu na mtaani. Mi muoga sana kupiga mwizi ila nilikua nasaidia kusogeza mawe.
 
Pole sana chief, wezi wanaboa sana. Kama una tabia ya kuwaalika mademu nyumbani kwako nakushauri uache.
Hii kitu ina ukwel , nikiwa Mwanza Mzee nilikuwa na gheto boss , siku moja nikaopoa manzi , nikamwingiza gheto mara ya Kwanza , nikarudia tena mara ya pili daah..... ma- Mae baada ya sku mbili Mzee nikachapwa deki , ....

Mwamba kuona hvyo nikaona isiwe tabu, nikahamisha kila kitu nikabakiza kitanda Tu , niliahrisha na kununua vitu vingine mpak nilipopata nyumba ya kueleweka a.k.a Geti Kali kuna mbwa mkali..... Nahs Yule manzi aliwaelekeza wajuba aisee
 
Back
Top Bottom