Nimeibiwa vitu vyote vya ndani

Nimeibiwa vitu vyote vya ndani

Habari wana jamvi,

Naandika nikiwa na jazba na hawa watu wanaoitwa wezi. Nimepanga geto langu nikajibana nikaeka vitu vyote vya ndani sasa hawa jamaa wamenilia time nimetoka wamenisafisha hadi kijiko ila kwenye vitu walivoiba wamebeba hadi king'amuzi.

Ila kuna mdau aliyeniambia king'amuzi kinatafutika kama ilivyo kwa simu.

Msaada jamani kwa mwenye ujuzi maana nikimpata mwenye king'amuzi ndio nitamtolea uvivu.

Nawasilisha
download%2B%25282%2529.jpg

Namna ya kumrudisha mwizi aliyekuibia​

kumkamata au kumrudisha mwizi aje mwenyewe
unamchukua kinyonga akiwa mzima,
unaponda majani ya kisamvu,
unachukua na changarawe za njiani
huyo kinyonga unamuweka kwenye hayo majani ya kisamvu pamoja na hizo changarawe unafunga kwa kwenye kitambaa cheusi
halafu unafunga jikoni kwenye sehemu inayopata moshi
utamuacha hapo kwa muda wa siku7 baada siku 7 unamtoa hapo kwenye moshi unamsaga ukiwa umefumba macho halafu unaenda kufunga kwenye mti kwa muda wa siku7
kabla siku7 hazijaisha mwizi wako atarudi mwenyewe na kama mwizi yupo humo ndani atajisalimisha mwenyewe mara moja Tumia dawa kisha uje utupe Mrejesho wako.
chanzo.Herbalist MziziMkavu.
 
Pole sana mkubwa ndio hasara za kuishi na majizi nyumba moja,sasa sijui itakuaje kama baby wako akija ghafla leo usiku
 
Huko kwa waganga nilipelekwa bunju huko ndanindani, kumbe magumashi tuu mara hela ya kuku, mara hela ya sanda, kazunguka wee mwisho ananiambia kazini kuna wanaokuloga ufukuzwe, nikajua huu upigaji sikurudi tena.
 
Pole mkuu
Ita mtaalamu wa mitishamba aje achukue finger print
 
Aseme tu hivyoo inatoshaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Sem pole sana mkuu hao majirani zakoo wanaonaga ukiingiza mademu tuu ilaa Kuibiwaa geto zima hawajaona. Mwizi wako hayupoo mbalii tena hata hatua kumi ni nyingii.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
Wenyewe wanasema "kikulacho ki nguoni mwako".

Inawezekana kabisa wezi hawatoki mbali mkuu.
 
Pole sana Mkuu

Piga maombi Mungu atazungumza nao tuu... au kama vipi tafuta mtaalamu haswa awaguse kidogo tuu yatembee barabarani yakijikojolea.

Au yakilala yakose usingizi kazi iwe ni kujikuna hadi asubuhi.
Mshauri afanye moja kama ni kumwachia Mungu atende,iwe hivyo,ila kuchanganya na mwanadamu ni kupungukiwa imani
 
Wenyewe wanasema "kikulacho ki nguoni mwako".

Inawezekana kabisa wezi hawatoki mbali mkuu.
Mshkaji wangu aliiibiwa PC na mtungi wa gas wale majirani wakakana kabisaa yani kuwa hawajauona mwizi...!! Baada kama ya siku mbili akampa mdada flani 10K amwambiw mwizi wake yule dada akagoma ila baadae akamfata jamaa maana njaa kali sana mzee...akamwambia aliemuibia[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kweli wakaenda mpaka alipoviuza.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Habari wana jamvi,

Naandika nikiwa na jazba na hawa watu wanaoitwa wezi. Nimepanga geto langu nikajibana nikaeka vitu vyote vya ndani sasa hawa jamaa wamenilia time nimetoka wamenisafisha hadi kijiko ila kwenye vitu walivoiba wamebeba hadi king'amuzi.

Ila kuna mdau aliyeniambia king'amuzi kinatafutika kama ilivyo kwa simu.

Msaada jamani kwa mwenye ujuzi maana nikimpata mwenye king'amuzi ndio nitamtolea uvivu.

Nawasilisha
Pole mkuu hawa watu wanatia hasira asikuambie mtu, wamekuibia moshi sehemu gani mkuu
 
Pole sana Mkuu Polisi watakuambia lete elfu 50 tuifuatilie no ktk kampuni za simu. Jiandae sana kuliwa hizo hela 50-50
 
Mshkaji wangu aliiibiwa PC na mtungi wa gas wale majirani wakakana kabisaa yani kuwa hawajauona mwizi...!! Baada kama ya siku mbili akampa mdada flani 10K amwambiw mwizi wake yule dada akagoma ila baadae akamfata jamaa maana njaa kali sana mzee...akamwambia aliemuibia[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kweli wakaenda mpaka alipoviuza.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
Duh! Noma sana
 
Back
Top Bottom