Nimeichukia sana Dar

Tangu niondoke huko 2023 nimekuwa na amani sana ,mwaka mzima nilikuwa napambania uhamisho...Kulinishinda kabisa ; kwanza foleni hata uwe na gari ,wezi kila kona, ratiba kwa kazi zetu huko lazima uamke 11 alfajiri ...Huku Tanga ni raha kwenda mbele hakuna vurugu .

Woyoo!
 
Sema joto la mapumbu sio poa🤔😂usiombe hiyo siku combination ya joto na mbu pale umeme Unapokuwa umekatika alafu unaishi kwenye nyumba zile fupi zenye madirisha madogo Kigogo, ubungo😂, manzese
 
Mkoani njaa nakataa
Ila mzungukonwa Hela pia hauwezi fanana na dar kutegemea na mkoa uliopo
 
Magufuli alisema atakayebaki Dar atakuwa Mwanaume.

Acha sisi wanaume tupambane.
 
Saa mbili?
 
Iko tofauti kubwa tu kati ya Dar es salaam na mkoani. Siku sita nilizokaa mkoani zilithibitisha kuwa mikoani maisha yanakwenda kwa kasi ya 2-3G hii nimeiona Bukoba, Kigoma, Tabora na Dodoma
Kasi ya maisha Dar nadhani inakaribia au kupita 5G 😂
 
Karibu duniani..!
 
Si kweli kwa ASILIMIA zote
Ni vipaumbele binafsi vya mtu vinamfanya apende au kuchukia Dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…