Nimeichukia sana Dar

Nimeichukia sana Dar

Dar es salaam ni kuzuri na kubaya

Mkoani napo ni kuzuri na kubaya! Ila nikiwa mkoani nafurahia sana tofaut na dar,

Dar es salaam Ina heka heka so poa, ukiwaza usafiri, mvua km sasa Kuna dalili zote, jua Kali, kipindi kama Cha funga hivi tunaotegemea mama ntilie hawapiki, wizi, harufu za mitaro

Ila dar ukiwa na akili na ujanja ujanja unatoboa
Nzurii hii
 
WaTanzania wengi ambao hawajaishi nje ya Dar hua wana beza mikoani, lakini once wanapo pata wasaha wa kuishi kidogo mikoani hua wanaichukia Dar
Na mtu yeyote ambae atathubutu kuishi out of the comfort zone, lazima ataona mabadiliko na kufurahia maisha
Hata Dodoma walikataa kuhamia, ila walipohamia kwa kulazimishwa na Magufuli, hawataki tena kurudi Dar
 
Dsm ipi rahisi kutoboa? Em acha kudanganya umma hapa. Lol

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Bora wa msamala mwenzangu umemjibu vizuri. Mwambie sisi tumishi huko lakini bado tunaamini kuishi msamala na kufurahia maisha kunyumba tunaona bora zaidi kuliko hekaheka hizo za Dar.

Kwa ruhusa yako darling mwambie atutembelee nyumbani ajioneee
 
Tangu niondoke huko 2023 nimekuwa na amani sana ,mwaka mzima nilikuwa napambania uhamisho...Kulinishinda kabisa ; kwanza foleni hata uwe na gari ,wezi kila kona, ratiba kwa kazi zetu huko lazima uamke 11 alfajiri ...Huku Tanga ni raha kwenda mbele hakuna vurugu .

Woyoo!
TANGA upo sehemu gani? Au hapo katikati ya Jiji Mabanda ya Papa?
 
Kisa usingizi 😀😀😀

Ila watu wa mikoan wakienda huko wanaona kama wamefika Paris 😂
 
Ule mji ni mgumu sana mkuu hasa kwa mtu anaejitafuta....ili uifaidi daressalam uwe na Ajira au biashara inayoeleweka, uwe na makazi au malazi ambayo kidogo ni standard, nikisema malazi na makazi standard namaanisha maeneo yasiokuwa na kelele,hewa safi, na nyumba nzuri mfano kidogo goba huwa naona ni sehemu kidogo iliyotulia hakuna makelele kama buguruni na tandale...
 
Back
Top Bottom