Nimeingiza faida ya 1,092,600 baada ya siku 90 za biashara yangu

Nimeingiza faida ya 1,092,600 baada ya siku 90 za biashara yangu

hapo unapata kama elfu 12,000/= kwa siku hio sio haba ila inategemea na opportunity cost yako mwenyewe..
Je unaweza kupata zaidi ya hio kwa kufanya kingine.., kama hapana basi this is the best scenario kwa situation yako..

Pili je ni lazima wewe uwepo kwenye hio biashara 24/7 kama hapana basi hata kama faida ingekuwa ni Tshs 500/= kwa siku sio mbaya kabisa sababu (its better to get 5% of the profit with 0% energy input kuliko 100% of the profit with 100% energy input)

Hapo umeongelea overheads za umeme na chumba tu..., je ukiongezea TRA, Fire, Taka na Service charges hesabu zitasomekaje....

Mwisho how hard is it kwa mwingine kuiga biashara yako..., sababu wabongo wakiona tu mzigo unauza usishangae keshokutwa ukakuta kila mtu anafanya unachofanya kwa bei ya kipuuzi hence kukutoa kwenye mstari...

Mwisho hakuna biashara mbaya wala nzuri (uzuri na ubaya ni wewe mwenyewe uwezo wako au utayari wako wa kufanya kinachotakiwa kufanyika), hapa I mean kufanikiwa kwa mwingine sio necessarily kwamba wewe utafanikiwa and vice versa...
 
Asante sana Mkuu kuna wakati Nilidhani nafanya mchezo tu lakini kumbe ninapiga hatua ipo hivi

Nilikua nafanya kazi ofc moja kwa mwezi nilikua nalipwa laki moja tu imagine japo kulikua na deals za hapa na pale lakini ilikua hailipi
Biashara yako iko vizuri sana ukizingatia umepata faida ndani ya siku za mwanzo za biashara. Cha kujazia jikite kwenye ukuzaji wa mtaji kila mia irudi kwenye biashara utafika mbali. Asikushauri mtu kuanza kufanya dead investiment kwa wakati huu.
 
Nilijua tu atasema ni business yachupi. Uweke na bikini
Hahaha ndo ninayoifanya bikini zipo mkuu Karibu
IMG-20190926-WA0009.jpg
8
 
Hapo umeongelea overheads za umeme na chumba tu..., je ukiongezea TRA, Fire, Taka na Service charges hesabu zitasomekaje....
Hapo TRA ndo Nataka kuanza kulipa mwaka huu Fire Sijaenda mpaka wapite na kuhusu kuwepo Ndio ninaifanya mwenyewe Biashara maana mtaji naujua nilipoutoa nisipoulinda nani mwingine wa kunilindia?
 
Hii ni kitu gani nifafanulie please
Kutoa pesa kwenye mzunguko wa biashara yako na kununulia vitu visivyoingiza pesa mfano kujenga nyumba au kununua kiwanja kwa wakati huu ambao biashara inatakiwa ikuwe.
 
Hapo TRA ndo Nataka kuanza kulipa mwaka huu Fire Sijaenda mpaka wapite na kuhusu kuwepo Ndio ninaifanya mwenyewe Biashara maana mtaji naujua nilipoutoa nisipoulinda nani mwingine wa kunilindia?
Tena ukienda TRA ukawapa hizo hesabu za hizo faida; unaweza ukazimia..., kumbuka wenyewe wanaangalia mauzo na sio faida kwahio ukiwapa hesabu za mauzo unaweza ukajikuta kafaida kote mnagawana pasu kwa pasu..., kwahio kama bidhaa zako ni nguo unazowapelekea wateja unaowajua personally mahali walipo huenda hio ikakupunguzia overheads
 
Si mbaya chati yako inaenda vizuri,kuna eneo la masoko ukiboresha tu..faida itaenda kwa kasi zaidi,ingawa itategemea na mtaji ulionao.
 
Kutoa pesa kwenye mzunguko wa biashara yako na kununulia vitu visivyoingiza pesa mfano kujenga nyumba au kununua kiwanja kwa wakati huu ambao biashara inatakiwa ikuwe.
Oh Asante kwa ufafanuzi
 
Mkuu kuhusu mkoa mi niko Kanda ya Ziwa na nafanya biashara ya Chupi. nilianza na Chupi na wakati Naendelea nikawa naongeza vitu kidogo kidogo na still Naendelea kupambana nione Duka likifika umri wa mwaka itakuaje
Mkuu ni mwanzo mzuri usikate Tamaa cha msingi unavyopata faida inabid uongeze bidhaa toafuti tofauti kutokana na mahitaji ya wateja ili kuongeza wigo mpana Wa biashara yako kwa kufanya hivyo pia faida itaongezeka na Kama utaendelea kua na heshima na saving nzuri ya pesa nakuhakikishia baada ya muda utakua mbali sana.
Achana na maneno ya hao wakatisha tamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku tisini (90) baada ya kufungua Biashara.

Habari wana JamiiForums, leo nimekuja kwenu kupata maoni kuhusu mwenendo wa biashara yangu hii niliyoianza siku 90 zilizopita.

Nilifikiria kuanza biashara hii baada ya kazi niliyokuwa naifanya kufa. Wakati nafikiria kufungua biashara nilikuwa sina mtaji na sikujua nitaupata wapi lakini niliamua kutafuta wapi wanauza bidhaa hizo kwa jumla ili nikifanikisha kupata pesa nisiangaike kutafuta mzigo unapopatikana.

Badaye niliamua kuuza kiwanja changu kwa shilingi 2,000,000/= baada ya makato ya dalali na wakili (wakili tulichangia na mnunuzi) nikabakiwa na 1.9 ku-cut story short, nilikwenda kununua mzigo baada ya kulipia chumba, nauli, nilifanikiwa kuanza na mzigo wa 900,000+

Baada ya kufungua biashara nilianza kwa taabu maana wanasema mwanzo mgumu, lakini nilipambana nikawa kila shilingi ninayouza naagiza mzigo Dar, hivyo hivyo baada ya siku kadhaa mahitaji ya wateja (wanaoulizia) bidhaa fulani ikawa kubwa ikabidi nitafute sehemu nikope pesa niongezee mtaji nikapata 800,000 nikaongeza mtaji dukani.

Ikumbukwe kwamba hapa dukani sitoi matumizi zaidi ya matumizi ya kulihudumia duka kama umeme, mlinzi nk.

Hivyo mpaka leo siku tisini nimeingiza faida ya 1,092,600/= .

Swali langu kwenu: Je, ninakwenda vizuri na biashara hii au napiga mark time tu?
Kama hutoi hela dukani zaidi ya umeme na mlinzi sasa hela ya kula na vitu kama hivyo hela yake unatoa wapi?;au ni mwendo wa deshi tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo faida ya kama 12500 per day si mbaya kwa biashara yako upo vizuri sana,ila tu hiyo faida iwe ya dukani nikimaanisha inunue mzigo mwingine na kuongeza mtaji wa duka lako.

yani nasema hivi hiyo 12500 iwe faida baada ya kutoa kodi ya frem,matumizi ya ofisi,matumizi binafsi (kama unapategemea hapo)nk kisha mkononi ukibaki na 12500 asee una bonge moja la biiashara.

ila sasa kama hiyo faida yako bado hujatoa matumizi ya ofisi,hujatoa kodi ya frem,hujatoa makorokweche mengine Asee don't count it kama faida.

Nakupongeza kama Hyo faida ni baada ya Kutoa kila ktu asee ndugu hongera sana sana sana maana kwa siku unaweka kwenye kibubu zaidi ya 10k ukiwa umeshakula umeshafanya kila kitu na jioni unahifadhi ka 10k kako asee uko vizuri sana sana.

Hongera sana kwa hilo.


ila kama ni tofauti na hapo mkuuu una safari bado kazana kazana mno,jiongeze weka vi huduma tofauti hapo ofisini kwako wawekee tgo pesa wateja watoe na kuweka,wawekee vocha wakati akinunua vocha ataona ki chupi ataulizia bei,wawekee FRIJI la dsplay linauzwa 500k kale kadogo wawekee maji na juice.

Ongezea pato lako na vibiashara vya kijinga jinga,na kwakua unauza Chupi na Bikini sio mbaya ukienda town ukanunua

Vikuku vya miguuuni na Cheni za kiunoni ukawawekea

Vikuku town wanauza jumla sh 1000 kwa kimoja vizuri mpk 1500-2000,so ukiweka vikuku na cheni hapo aaaha utauza sana mkuuu nakuhakikishia,mwanamke anaevaa bikini huyo hashindwi vaa cheni ya kiunoni,trust me you will make a deal through it.

Weka vi hereni hereni vi pete pete vya urembo aaaaah mkuuuu nasema hiviii usikubali wakuite muuza bikini/chupi duka lako lipe huduma zote zinazoendana na BIDHAA KUU (chupi/bikini)

Utanikumbuka siku 1.
 
Usiwe kama wale anauza vocha za kukwangua,ukimuuliza una vocha za kurusha anakwambia HANA,bidhaa yako ya bikini hiyo bila kutia na cheni za kiunoni aaah unakosa hela mkuu zinakupita nyingi.

ukishaamua kuuza bikini ujue kuna wateja umewalenga na hao wateja wa bikini 80% wanavaa cheni kiunoni,vikuku,nk hao n madada duuuh sio kina maza mchungaji.
 
Back
Top Bottom