Nimeipenda falsafa ya Rais Samia ya Watendaji kutumia akili badala ya nguvu. Je, CCM wamemuelewa?

Nimeipenda falsafa ya Rais Samia ya Watendaji kutumia akili badala ya nguvu. Je, CCM wamemuelewa?

Aisee mmedata, si bure. Kifo cha "mungu" wenu kimeleta ukungu kwenye ubongo naona.
Ufipa mko busy na hayati Magufuli wenzenu CCM wanasonga mbele kwa mbele wembe ni ule ule.

Chadema wamejazana vifutu watupu!
 
Ufipa mko busy na hayati Magufuli wenzenu CCM wanasonga mbele kwa mbele wembe ni ule ule.

Chadema wamejazana vifutu watupu!
Achana na Chadema - hawana serekali wale. Ukifika wakati wao nao tutawabamiza vile vile.

Sasa hivi sisi tuko na huyu anayepokea kodi zetu ndiye tunakula naye sahani moja.
MATAGA naona mko kwenye maombolezo maana inaonekana soon mama atawazamisha mapipa ya choo cha shimo huko!
 
Mama hajawajua wa Tz vzur....nchi hii imeshaharibika..tutubu tulipokosea..
 
Miguvu mwisho Ufipa.

Tanzania Daima oyeee!
Leo ndiyo tunakamilisha siku 21 za maombolezo na pia siku 21 za kuuzika rasmi Udikteta wa awamu ya tano!

Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa majaribu yote aliyo tupatia ndani ya hii miaka mitano na miezi kadhaa! Hakika Mungu ni mwema sana.
 
Achana na Chadema - hawana serekali wale. Ukifika wakati wao nao tutawabamiza vile vile.

Sasa hivi sisi tuko na huyu anayepokea kodi zetu ndiye tunakula naye sahani moja.
MATAGA naona mko kwenye maombolezo maana inaonekana soon mama atawazamisha mapipa ya choo cha shimo huko!
Yaani unaamini Chadema kuna siku itaunda serikali?

Wewe ni bure kabisa.
 
Majitu kama Chalamila, Sabaya, hawajui Mama yetu kasema, fukuzaaa hawa makatili, wahuni serikalini
 
Nimeielewa sana falsafa ya Rais Samia kuwataka watendaji wote kutumia akili badala ya nguvu wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

Kwa mfano kumfukuza Tundu Lissu bungeni ni matumizi ya nguvu badala ya akili.

Kumsimanga Prof Assad ni matumizi ya nguvu

Kuwaingiza akina Nusrat Henje bungeni ni matumizi ya nguvu badala ya akili.

Nk.....nk....nk!

Hakika awamu ya 6 na mambo mapya hakuna kuoneana.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu umebadili gia angani [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Muhimu sisiemu wasikie inatosha

Swala la kuelewa linaweza kuwa juu ya uwezo wao ila muda ukifika wataelewa

Muhimu MATAGA wamesikia
 
CCM wakirudi kwenye misingi ya kutumia akili kwenye Siasa kuliko ubabe na pia Wabobezi wa hiyo falsafa wapo kina Kinana Msekwa Jaji Warioba wapo

Fukuza Polepole na Unafiki wake weka wabobezi
 
Mwanzo mzuri.

Tujenge taasisi imara,sheria na katiba nzuri,bunge na mahakama ziwe na uwezo wa kumdhibiti Rais,tusije kutumbukia shimoni Miaka ijayo.
 
Sheria za zingine unaziacha unafuata busara.
Mfano ba mkwe wako kaja bank kapanga foleni wewe upo mbele yake,si utampisha awe mbele yako ili achukue fedha asepe.
Kumbuka neno la Rais ni sheria pia.
Na kasema kuna mambo ya Barick yamalizike means sheria zitarudi nyuma ila za kujali maslahi.
Kwani kama inajulikana kabisa kuwa sheria za uwekezaji ni kandamizi na zinafukuza wawekezaji, sasa ugumu wa kuzifuta unatoka wapi?
 
Back
Top Bottom